Mapenzi yamesababisha urafiki wetu uvunjike

Aiseeee jiandae kutokewa na yaliyomtokea mwenzio, kama aliweza kukutongoza mbele ya mpenzi wake ujue the same itatoke siku moja, itatokea siku moja nakuapia, na utamia kama jama aalivyoumia na pengine utaumia zaidi maana huyo Anna atakua na mwanao, kama kweli ni mwanao
 
Mimi binafsi sioni kosa la mleta mada, Mungu aliamua kukupa mke kwa staili hiyo, shukuru Mungu endelea na maisha, sababu hakuwa mchumba wake rasmi aliyejulikana home. Mwana usiogope kutishiwa akizingua na wewe mzingue na ukizidiwa nicheki PM nikupe msaada.
Duuuh, we jamaa Mungu gani anaruhusu watu kuzini, mleta mada bado hajaoa kwa maelezo yake, hii vita ni shetani kwa shetani, shortly jamaa kazingua
 
duh namwonea huruma rafiki yako aisee ...........kuna mambo mawili kweli alikupenda na hata kufanyia kama alivyomfanyia rafikio .. au na wewe akimpata wa kukuzidi atakukimbia ...
ombeni msamaha ila kumla inawezekana pia
 
Smart911 sweetheart Mwanaume wa kweli haibiwi

You know vile unanimarrliza eeeeeh!!!
Hata mwanamke mwenye msimamo haangaiki ovyo huku na huko... Hapo mwanamke hana msimamo kabisa, na jamaa anaweza fanyiwa same kwa sababu ni kama tabia yake...

Vitu vinavyoleta chuki duniani ni, Pesa na mapenzi...


Ndiyo maana mara zingine i do what a man gat to do kwa mahondaw wangu...
 
Kwa hiyo unatakaJohn akusamehe ili umgongee na mwanamke mpya atakayekua nae hilo LA kutokutaka kuonana na wewe ni msamaha tosha unless hata angetumia msumeno kukuhasi maana ndo msamaha pekee ambao Mimi ningeutoa kwako ili siku nyingine ukitambulishwa shemeji zako uombe na Zawadi ya sidiria kabisa
 
mbona sijaona shida katika hili, wala john hana haja ya kunoa kisu sijui shoka ye atulie atawalipa kwa staili sawa na wao.

ilinitokea mwanamke wangu akachukuliwa na rafiki na kuzaa nae kama ivi ivi sikuwahi sema chochote huku huyu rafiki akijitetea kwamba yeye ndo alianza kumtongoza.

nikaingia kazini na mimi, nikamtongoza mdogo wa rafiki aliemtia mimba demu wangu nikamtia mimba na mimi.sikuishia hapo nikamtafuta dada wa demu wangu nae nikatia mimba, watajua wataitanaje hao watoto.

hapa niko taratibu nanyatia siku za hatari yele x wangu nae nimtie mimba.(mechi za mchangani zinaendelea)

john fanya kulipa kisasi wote tu shee maumivu,maana nakumbuka baada ya mdg wa mdogo wa rafiki yangu kujifungua na kuambiwa mtoto wangu alilalamika sana hadi kunitumia meseji (hatukuwahi kuwasilina 2yrs) akilaumu

kisasi ni lazima mambo ya kusamehe ni utoto
acha bana unatesa watoto mkuu acha bana
 
Wadau ni matumaini yangu kuwa wote ni wazima

Nikiwa na huzuni kubwa naandika uzi huu kwa lengo la kumuomba msamaha rafiki yangu wa utotoni na wa muda mrefu John (Ni jina lake halisi) kwa yote yaliyotokea kati yetu, kwa kauli yako ya mwisho wakati tunaongea kwenye simu ulisema hutokaa unisamehe maisha yako yote, kwa kile unachodai kuwa nimekunyang'anya mwanamke wa maisha yako, lakini kauli yako hiyo bado hainifanyi mm nisiendelee kukuomba msamaha.

Kila nikifanya Juhudi za kuonana na wewe ili tuzungumze face to face umekuwa ukikataa kuonana na mm. Najua hupo humu Jf na ukipata muda naomba soma uzi huu ili uelewe kilichotokea kati yangu na shemeji (Demu wako)

Unakumbuka mwanzoni mwa mwaka jana nilivyokuja kukusalimia ulipokuwa unaishi mwanzo Mbezi Kimara, Nilipofika kwako, baada ya stori za hapa na pale ukapendekeza tutoke home kwako twende bar moja hivi, kwa jina nimeisahau ila haikuwa mbali sana na mahali ulipokuwa unaishi.

Tukiwa njian tunaelekea kwenye ile Bar.. Ulimpigia simu shemeji ili nae aje kuungana na sisi. Kwa wasiojua ni kuwa John na Shemeji yangu walikuwa wakiishi mtaa mmoja.

Nakumbuka Baada ya kama dk 30 hivi toka tufike pale bar, shem aliwasili. Ulinitambulisha kwa shemeji, kuwa anaitwa Anna. kisha vinywaji vikaendelea. Wewe ulikuwa unakunywa Safari. Mm na Shem tukinywa Soda.

John usichokijua ni kuwa sekeseke lilianza baada ya wewe kutoka pale mezani kwenda Chooni. Tukiwa tumebaki wenyewe mezani mm na shemeji. Shemeji alivunja ukimywa kwa kuanza kunisifia kuwa kati ya rafiki zako wote uliowai kumtambulishwa, mm tu ndo ambae ameona sinywi pombe.

Aliendelea kusema naonekana mpole na mtaratibu, mwisho shemeji aliniomba namba yangu ya simu ila alinisihi sana kuwa nisikwambie ww.

So i want to make a record clear that, mm sio wa kwanza kumuomba Anna namba. Yeye ndo alianza.

Nilimpa Anna namba yangu ya simu huku nikiwa na maswali kadhaa kichwani..Kwa nn alisubiri mpaka ww uondoke mezani ndo aniombe namba? Alishindwa nn kuniomba mbele yako? Kwa nn hataki ww hujue? Lakini sikujali sana nikampa namba.

Baada ya muda kidogo ulirudi mezani na kutukuta kimya kabisa kila mtu yuko busy na simu yake kana kwamba toka uende chooni hakuna mazungumzo yoyote yaliyofanyika kati yangu na Anna.

Ulivyorudi stori zikaendelea mpaka mida ya saa tatu usiku nilipoamua kuwaaga na kuanza safari ya kurudi kwangu Kigamboni. Nilichogundua wakati wote tukiwa pale Bar, Anna alikuwa mtu wa kuniangalia sana.

Nikiwa naendesha gari narudi nyumbn.. niliwaza vitu vingi sana.. Vipi endapo ww utagundua kuwa shem ana namba yangu? Kuna wakati niliwaza nikwambie kuwa shem aliniomba namba yangu ya simu ila nikawaza utachukuliaje? Sitawagombanisha kweli?

Kwa kifupi maswali yangu yote kwa wakt ule yalikosa majibu. Nilibaki kujiambia tu moyoni ngoja nione lengo la Shemeji kuomba namba yangu kwa kificho. Nilijipa moyo wenda hana nia mbaya. Na hapo ndo nilipokosea, bora ningekwambia ukweli kuwa shem kachukua namba yangu ulivyokwenda chooni ili kama kugombana mngegombana au kama ungechukulia kawaida sawa.

Nikiwa bado nipo njiani, sms iliingia kwenye simu yangu. Kucheki ni Anna. Sms ilikuwa inasema 'it was nice meetin u shem'.. i just replied 'Thank you'.

And she was like 'Hope to see u again shem' Nikamjibu 'Wornot shem'

Siku iliyofuata nakumbuka ilikuwa Jumatatu.. Tuliendelea kuwasiliana na shem, mawasiliano yaliendelea kuimarika hadi kufikia hatua tukawa hatuwezi kulala bila kuwasiliana.

Na kwa kuwa wote, mm na Anna tulikuwa tukifanya kazi Posta tulipata muda mwingi wa kuonana. Hilo ni kosa jengine ambalo niliruhusu, lakini wakati mwengine najiambia sikuwa na kosa sababu Anna alilazimisha sana kuonana na mm. Nadhani kwa wiki nilipata muda mwingi wa kuonana nae kuliko wewe.

Kuna wakati ulimpigia simu akiwa na mm alikuwa hapokei. Nilimuuliza kwa nn hapokei simu zako hakuwa na jibu la kuridhisha alilonipa.

Sisi tukaendelea kuwasiliana asubuhi, mchna na usiku, Lakini wakati wote huu wa mawasiliano yetu, Anna alisisita sana usijue.

Ukweli kama binadamu taratibu nilijikuta naanza kumzoea Anna. Ilifika hatua Anna alikuwa hataki kuonana na ww, nilikuwa najua hilo na nilimsisitiza asifanye ivo lakini hakuwa tayari tena kuwa na ww.

Taratibu mm na Anna tukawa wapenzi.Ushemeji tukauweka pembeni.hata ile siku ambayo mligombana sana kwa sababu ulitaka akupe Password ya simu yake lakini hakufanya ivo. Anna alinieleza kila kitu. Baada ya ugomvi alikutumia sms kuomba muachane.

Nakumbuka ulinipigia simu mm na kunieleza kuwa Anna amebadilika sana na ukanitumia namba yake ukaniomba niwapatanishe. Nilikujibu kuwa 'Sawa nitafanya ivo'

Ukweli hakuna nilichoongea nae Anna. Kwa upande wetu mapenzi yalipamba moto, hadi kufikia hatua Anna akitoka kazin straight kwangu, hata kwake alikopanga mbezi alikuwa haend tena, alisema mbezi mbali na kazini kwake. Ni kama alihamia kwangu kiaina maana hata nusu ya nguo zake zilikuwa kwangu.

Kama utakumbuka, ndo mana kila ulivyokuwa ukitaka kuja kwangu nilikuwa sihishi sababu, nakujibu sipo, mara nakwambia nimesafiri kikazi.

Mapenzi yalinizidi..Mara na Anna tumekwenda Bagamoyo, Mara Mikumi, mara Movie mlimani city, mara Shopping Mkuki House. Na mambo mengine mengi.

Hatimae Anna akanitambulisha kwa mama yake. Kwa dada zake, kwa kaka zake, kwa rafiki zake.
Nakumbuka mwaka jana mwezi wa sita, Anna alishika ujauzito wangu na mwaka huu mwezi wa Pili mungu ametupatia kijana niliyempatia jina la Marehemu Baba yangu, Denis.

Kwa kipindi chote hiki nimekua mtu wa kukukimbia na kukuhepuka sio kwa sababu sitaki kuonana na ww ila kwa sababu sura yangu itashindwa kukuangalia usoni.

Juzi ulivyonipigia simu na kuanza kunitukana na kuniita msaliti na kunitishia maisha wala sikushangaaa sana, najua wapi ulipopata habari.

Juzi Anna alivyoweka picha yetu Dp whatsapp na kupost facebook, tukiwa tumembeba mtoto, nilimwambia kuwa umefanya makosa. Anna alichonijibu ni kuwa tutakuficha mpaka lini.

Kwa hiyo nataka uelewe kuwa , uhusiano wangu na Anna ulianza siku ile pale bar na sio kama unavyodhani ww kuwa, ulivyonitumia namba yake ili niwasuruhishe ndo nikamtongoza Anna. Sio hivyo hata kidogo.

Lakini yote ya yote ni kuwa makosa yalishafanyika na nakuomba msamaha. Mpaka naandika hapa tulishajadiliana na Anna na wote wawili tunakuomba msamaha na tumepanga kuja kwako kukuomba msamaha zaidi.

Ni Mm RTM
Wee jamaa FISI MKUBWA sana umekula shemejio??? mtu hatari sana.
 
Kuna wakati unaweza kuwa na mtu ilimradi tu, alafu akatokea yule mtu wa ndoto zako sasa, inakuwa haina jinsi, life isnt fair just like that. Wakati mwingine inabidi tuelewe tu japo ngumu kumesa.
 
acha bana unatesa watoto mkuu acha bana
wateseke na nini tena, watoto wote nawahudumia na hata nkishindwa hawa wasaliti watahudumia maana nimepiga kwenye familia zao.

kubwa zaidi ukoo wetu tuko wachache wacha niongeze vijana asee
 
wateseke na nini tena, watoto wote nawahudumia na hata nkishindwa hawa wasaliti watahudumia maana nimepiga kwenye familia zao.

kubwa zaidi ukoo wetu tuko wachache wacha niongeze vijana asee
wanakosa mapenzi ya baba yao.. mkuu sijui ni kiasi gani uliumizwa lakini nakushauri bora uwatie tu uwavuruge utakavyo ila usiwatie mimba viumbe hivyo wanataka kuita baba mapenzi ya baba plz kama mwanamke na pia mama naomba badilisha adhabu please.... na uhakika hata hao unaowazalisha wakijua ni part ya adhabu hawatakuwa na mapenzi na watoto wale ya kweli... ushapata wawili inatosha mkuu ni ombi tu badilisha adhabu
 
Kama Anna alikupenda Kwa kuwa mpole mtaratibu na hunywi pombe atatokea mwingine zaidi yako atampenda pia.


Ila uliharibu toka mwanzo aisee kuchukua namba ya shemeji yako na kuruhusu akuzoe kupita kiasi
 
Unapotongoza msichana hadi unafikia kukubaliwa ujue kuna mtu anaachwa taratibu
Hiyo ndio principal ya mapenz kwhyo relax tu
Hata John saiz atakuwa kashapata mwingine ambaye bond imevunjika somewhere
 
Huu unaofanya hapa ni unafiki, wa kumkandamiza huyo mwanamke uliyemwiba (kuonesha kosa ni lake ilihali ulikubali kutumia nawe kitanda maana yake mna makosa nyote) ili upatane na rafiki yako kirahisi. Mwisho wa siku unamrejea Mwanamke(yule uliyembebesha lawama, najua hutosema zigo ulilomtwisha ili usamehewe) na kumwambia maneno mengine mnapoenda kutaka kusamehewa, ili mwenzako aonekane mjinga.

NIMEAMINI RAFIKI WA KWELI NI YULE ANAYEKUTHAMINI NA KUKUHESHIMU NA SI KUKUA PAMOJA.


WEWE NI SAWA NA PANYA ANAYEMNG'ATA MWANADAMU ALIYELALA BILA KUOSHA MKONO HUKU ANAMPULIZA ASISIKIE MAUMIVU.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom