Mapenzi yamebeba vifo vya watu wengi sana

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,828
2,000
Mapenzi ni neno zito sana kwa sababu ndani yake mna mambo chungu mzima kama trust, upendo, watoto, furaha, kusaidiana, maisha ya watu, kuunganisha familia ndugu jamaa na marafiki n.k

Iwapo mapenzi yatakwenda vizuri basi ni neema ila mapenzi yasipokwenda vizuri humo tuna vina mifarakano, mauaji, magonjwa, vita, visasi. Hayo mengine yanazuilika au ipo tiba yake lakini KIFO hakizuiliki.
Mapenzi ni KIFO kwa maana nyingine kwa hiyo ukiona mtu kajimaliza kwa sababu ya mapenzi usishangae sana hiyo ni kawaida na sio kwetu sisi wanaume kwa kuwa tumeumbiwa mioyo migumu kama Mathayo 19:8-9 NOOO bali hata wanawake ni wahanga...
Mara nyingi inashauriwa msiowe ili kueuka matatizo yote hayo ukiendelea kusoma hiyo Mathayo 19:8... nakuendelea utaona wale waliokuwa wanamuuliza Yesu hilo swali waliona ni bora tuu kukaa bila kuoa sababu ni mateso.

Ushauri wangu.
-Kama unajijua umedhulumu mchuma/mke wa mtu ni bora umuombe msamaha kwa maana ulichotenda ndicho kitakacho kurudia wewe na uzao wako. Uwe una amini MUNGU au huamini. Ile dhambi ya KUZINI nayo inawatafuna watu mdogo mdogo pasipo wao kujijua.

-Kwa wale ndugu zangu wanasiasa na wanaoikosoa serikali nawashauri tuu msiowe au kama mna wake zenu basi mjiandae KISAIKOLOJIA/KIROHO NA KIMWILI kwani wabaya wenu wanagonga hapo hapo. Yani namanisha wanatembea na wake zenu na kuvuruga kabisa kila kitu na mnauwawa kabisa. Kama mlijisahau naomba niwakumbushie tuu. Udhaifu mkubwa wa mwanaume upo kwa mwanamke kwa hiyo wao wana deal na mkeo tuu. Najua wengi wanaugulia kimya kimya na wengine wamejitanguliza mbele ya haki ila mtumainie MUNGU tuu maana ndie faraja yenu kwa sasa. Binadamu kitu gani bwana wakati tunapita tuu halafu hata huwa hawajifunzi kwa sababu mioyo yao imejaa KISASI.
So ni bora kukosa mke na watoto kuliko kuishi kwa mashaka na siwashauri mkatembee na wanawake kwa sababu pia wanaambukiza ukimwi watu. Yanayotokea huku ni mengi ila ni vyema kuwasaidia watanzania wenzangu.
 

KANYIMBI

JF-Expert Member
Nov 6, 2011
638
1,000
Mapenzi yana raha zake hasa ukioa mtu mnaeshabihiana kwenye mambo mengi. Ili ufuraie mapenzi nawashauri muoe- binti ambae ni rafiki yako.
 

Upepo wa Pesa

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
14,732
2,000
.

-Kwa wale ndugu zangu wanasiasa na wanaoikosoa serikali nawashauri tuu msiowe au kama mna wake zenu basi mjiandae KISAIKOLOJIA/KIROHO NA KIMWILI kwani wabaya wenu wanagonga hapo hapo. .
Kuikosoa serikali ya JIWE kuna uhusiano gan na kutembea na mwingine? Au jiwe kawatuma mtishe watu?
 

tamuuuuu

JF-Expert Member
Mar 10, 2014
13,919
2,000
Ila mapenzi ni kifo kabisa.Kwa dalili hii nayoiona Kwa huyu dada mwenye Pete mkononi!!Na hili penzi linalotaka chipua baina yetu hakika sijui nikwepe vip.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom