Mapenzi yaliondoa maisha ya ndugu yangu

Mapenzi yaliondoa maisha ya ndugu yangu

mkuu Mr Rocky neno haki kwa dunia ya sasa ni msamiati,hakuna sehemu unyoweza kukimbilia ili upewe haki yako hasa ikiwa wewe ni maskini,ni kweli inaumiza lakini wakati mwingine tunamuachia Mungu mwenyewe ndo ataamua kwani hata muuaji afungwe maisha uhai uliopotea hauwezi kurudi kamwe,ila daaahhhh so sad aiseee inauma kiukweli:crying::crying:.
KAma ni habari ya ukweli mkuu kwa nini usiende Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu watakupa msaada wa kufuatilia jambo lako maana ni kesi ya mauaji mkuu na uhai umepotea wa mdogo wako kwa visa vya ajabu
Na hata Tume ya haki za Binadam na Utawala Bora unaweza kupeleka shauri lako mkuu Maana wako pale kusaidia watu kama wewe ambao mna madai ambayo yameacha yaishe bila msaada wowote
Usikae kimya wakati kuna uwezekano wa haki ya mdogo wako kupatikana kwani huwezi kuuondoa uhai wa mtu kisa hutaki binti yako apendane na mtu mfungie ndani basi asitoke kabisa aishi kwenye ulimwengu wa peke yake
 
Last edited by a moderator:
Pole sana mkuu that's all i can say,inuma saannnna i cant' even explain,mbaya zaidi kwa huyo mama yake jamani uchungu wa mwana jamani sijui ana hali gani mama wa watu masikini,dahhh this world is so unfair.
(ANGALIZO HII NI STORY YA KWELI) ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa tisa mnamo saa tatu na nusu usiku taraitibu napiga hatua kuelekea nyumbani mara ghafla simu ikaitwa kuangalia ni ya dada yangu aliyepo morogoro, nikapokea kwa furaha maana sijawahi kuwasiliana kwa muda murefu, maskini kuona tu dada anaongea kinyonge furaha ikaniisha ghafla, kumsikiliza ndo akaniambia habari za kuhuzunisha kuwa mdogo wangu amekutwa amekufa.

ninayemwongela hakuwa mdogo wangu tumbo moja bali alikuwa mtoto wa kwanza wa mama yangu mdogo anayeishi huko kigurunyembe morogoro. baba wa mdogo wangu huyo alifariki miaka mingi iliyopita hivyo mama yangu mdogo ndo alihangaika kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji yake yote ya msingi ikiwepo elimu. mdogo wangu huyo mauti yalimfika huku zikiwa zimebaki siku tatu kuriport chuo cha mzumbe tawi la mbeya alikokuwa amechaguliwa kusomea masomo ya sheria kwa ngazi ya degree.

MAZINGIRA YA KIFO
mdogo wangu siku ya tukio aliaga anaenda kwa bibi yake kuchukua baadhi ya mahitaji kwa ajiri ya safari ya kwenda chuoni, inavyosemekana alipokuwa akirudi ndipo alipotekwa na vijana ambao hatujui idadi yao na kwenda kumuua na kisha kumtupa barabarani.
KWA NINI ALIUWAWA
Inavyosemekana mdogo wangu alikuwa ana uhusiano na binti mmjoa lakini baba yake kumbe hakufurahishwa na uhusiano huo wa mwanawe na mdogo wangu huyo hivyo basi akaamua kumtumia vijana ili wayatekeleze mauaji yale

NANI ANATUHUMIWA
mtuhumiwa wa mauaji yale bila kuficha ni ni DIWANI MMOJA KATA NIMESAHAU PALE MOROGORO MJINI AMBAYE NIMEFANIKIWA KUTAJIWA JINA LAKE MOJA ANAITWA KIMARO ( KWA WALE WAKAZI WA MOROGORO WATAKUWA WANAMFAHAMU HUYU)

JE KESI INAENDELEAJE
Baada ya kutuhumiwa kwa haya mauaji huyu diwani alikamatwa lakini aliachiwa baada ya muda mfupi bila sababu maalum, ndugu zangu waliopo morogoro walipojaribu kuhoji walipewa vitisho na askari polisi hivyo basi kama familia walikaa kikako wakaamua wamwachie mungu maana wao kama wao hawakuwa na uwezo wa kushindana kipesa na diwani huyo ambaye inasadikika alitumia pesa kutoka

KWA NINI ATUHUMIWE DIWANI KIMARO
diwani huyo alituhumiwa baada ya kutajwa na wale vijana ambao wanasemekana walitekeleza mauaji hayo, kumbuka damu ya mtu ni nzito maana siku ile ile ya msiba kuna kijana alikuja kufuatilia mauaji waliyoyafanya, kijana huyo alikamatwa na akawataja wenzie ambao kwa pamoja walimtaja diwani kimaro.

HIVYO NDIVYO MAPENZI YALIVYOMTOA UHAI MDOGO WANGU, BABA WA BINTI KWA SABABU ALIKUWA HAMTAKI MDOGO WANGU NDO AKAAMUA AMTUMIE WAUAJI AMBAO BILA WOGA WALIMUUA NA KUMTUPA BARABARANI
MUNGU AMLAZE MDOGO WANGU HUYO MAHALA PEMA PEPONI AMENI
 
mkuu Mr Rocky neno haki kwa dunia ya sasa ni msamiati,hakuna sehemu unyoweza kukimbilia ili upewe haki yako hasa ikiwa wewe ni maskini,ni kweli inaumiza lakini wakati mwingine tunamuachia Mungu mwenyewe ndo ataamua kwani hata muuaji afungwe maisha uhai uliopotea hauwezi kurudi kamwe,ila daaahhhh so sad aiseee inauma kiukweli:crying::crying:.

Blue G najua kabisa mkuu haki haiwezi kupatikana duniani haswa kwa wale wa hali zetu za chini huku. Ila muhimu hapa ni kwa yule mhusika au wahusika hata kama watakamatwa na kukaa ndani kwa muda ijulikane na waonekane isiwe kwa kuwa wana pesa wanaweza kufanya lolote. Wameondoa uhai wa mtu na hilo halina ubishi na hawawezi kuondoka hivi hivi wakajitape mtaani kuwa wana pesa na hakuna wa kuwafanyia lolote hilo ni kosa. Uhai umeshapotea na wahusika wapatikane walipie makosa yao na matendo yao ya ajabu.
Najua uhai wa mtu kuurudisha ni ngumu na hakuna malipo ya uhai wa mtu ila angalau kukamatwa kwao na kuwekwa ndani hata kutumikia maisha huko jela inawafaa watu walioondoa uhai wa mtu
 
Last edited by a moderator:
Inauma sana aisee, usikubali kuwa eti kwa sababu huna pesa ndo unyanyasike, kuwa masikini jeuri. Fata ushauri wa Mr Rocky
 
Last edited by a moderator:
Simulizi yenyewe inatia simanzi hadi basi, Duh poleni wafiwa, ila chukueni hatua, hizo pesa zake mwisho wake upo tu, na sheria itachukuwa mkondo wake.

Ushahidi wa kwanza ni vijana waliotekeleza kitendo hicho cha mauaji, wasakwe wote na mengine yatafuata.
 
Nimekusoma vizuri mkuu,ila daaaahhh acheni tu jamani huu ulimwengu huuu.
Blue G najua kabisa mkuu haki haiwezi kupatikana duniani haswa kwa wale wa hali zetu za chini huku. Ila muhimu hapa ni kwa yule mhusika au wahusika hata kama watakamatwa na kukaa ndani kwa muda ijulikane na waonekane isiwe kwa kuwa wana pesa wanaweza kufanya lolote. Wameondoa uhai wa mtu na hilo halina ubishi na hawawezi kuondoka hivi hivi wakajitape mtaani kuwa wana pesa na hakuna wa kuwafanyia lolote hilo ni kosa. Uhai umeshapotea na wahusika wapatikane walipie makosa yao na matendo yao ya ajabu.
Najua uhai wa mtu kuurudisha ni ngumu na hakuna malipo ya uhai wa mtu ila angalau kukamatwa kwao na kuwekwa ndani hata kutumikia maisha huko jela inawafaa watu walioondoa uhai wa mtu
 
Nimekusoma vizuri mkuu,ila daaaahhh acheni tu jamani huu ulimwengu huuu.

mkuu unajua inatia hasira, hebu fikiria mama kamhangaikia mwanaye mbaka level za kuanza chuo, mama mwenyewe maisha magumu afu ndo alitegemea labda dogo akisoma atakuja kuwasaidia wenzie afu ghafla tu mtu anamkatisha uhai wake, inauma sana, najua ni ngumu sana kupata haki nitajitahidi ila mbinu mbadala za kuujulisha ulimwengu juu ya huu udhalimu ni kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku ndiko ambako roho yangu itasuuzika japo najua sitapata haki
 
Ingawaje na mimi nilipitia huku,LAKINI KADIRI UMRI UNAVYONICHUKUA naanza kukubali kwamba MUNGU alikua na maana kubwa sana alipotoa amri zake...si uasherati na uzinzi tu,bali uongo,tamaa na mengine mengi huleta matatizo makubwa katika jamii...Eeeh..menyezi mungu utujalie vipawa vya kuweza kuzikimbia dhambi..AAAMEN...POLE SANA,TAFUTA USAIDIZI WA KISHERIA...
 
Inauma sana aisee pole tena mkuu,pole sana kwa mama wa kijana.
mkuu unajua inatia hasira, hebu fikiria mama kamhangaikia mwanaye mbaka level za kuanza chuo, mama mwenyewe maisha magumu afu ndo alitegemea labda dogo akisoma atakuja kuwasaidia wenzie afu ghafla tu mtu anamkatisha uhai wake, inauma sana, najua ni ngumu sana kupata haki nitajitahidi ila mbinu mbadala za kuujulisha ulimwengu juu ya huu udhalimu ni kutumia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, huku ndiko ambako roho yangu itasuuzika japo najua sitapata haki
 
Nikupe pole sana mkuu, najaribu kukumbuka akili inaniambia hii kitu ilitokea mwaka juzi, wakazi wote wa kigurunyembe na bong'ora wanajua A - Z ya mkasa huu, maana hata mimi niliambiwa kilichotokea nilivyorudi weekend mapumzikoni nyumbani.
KUTOKA KWA BIBI
Niweke ufafanuzi zaidi wa kilichotokea siku ya tukio, Marehemu alitoka kwa bibi yake akiaga anaenda town fanya shopping (ya kwenda chuo), hakwenda kwanza shopping, alienda kwao na girlfriend wake mkazi wa kigurunyembe pia (less than a kilometer kutoka kwa bibi yake), ilikuwa jioni na nadhani hakuwa hata na mpango wa kwenda shopping siku hiyo hiyo as it was late tayari.

MAUTI YALIVYOMKUTA
Inside the house walikuwa watu wawili tu, girlfriend na Marehemu. Sasa alivyorudi baba mzazi wa girlfriend akiwa na kaka wa girlfriend ndio utata ulianza, walifunga milango yote ya nyumba na kudhibiti funguo, walimfunga Marehemu kamba na kuanza kumtesa. kelele zilisikika kwa majirani (ila no one bothered), ilifikia kipindi Marahemu alikuwa anapiga kelele msiniue msiniue but they never cared, ikafika hatamu akawa hapigi kelele, majirani walianza sikia sauti ya girlfriend akiomba boyfriend wake asiuliwe, haikufua dafu, baba na kijana wake waliendelea mtesa marehemu hadi walivyompiga na kitu kizito kichwani ikawa ndio mwisho wa maisha yake.

KUTELEKEZWA MWILI WA MAREHEMU

Giza lilikuwa lishaingia muda huo, walichofanya ni kuita dereva pikipiki, wakampakia marehemu huku akishikiliwa na kaka wa girlfriend na kwenda kuutelekeza mwili wa marehemu katika viwanja vya shule ya sekondari ya st. Peters (not more than 1.5kilometer toka eneo la tukio).

KUGUNDULIWA MWILI WA MAREHEMU
Nyumbani kwa bibi hawakumuona marehemu usiku huo akirudi home (nadhani kuwa na ndugu wengi wa karibu hakukuwapa hofu yeyote), hadi kesho yake jioni mwili wa marehemu ulipogunduliwa na wanafunzi wa st. Peters waliokuwa wameenda uwanja wa mpira kwa ajiri ya michezo ya kila jioni.

All in everyones mind kwa haraka haraka waliassume marehemu aliporwa ela na kuuawa as alikuwa na zaidi ya laki sita alizopewa na bibi, wakaamua kumzika kesho yake. Up to that point hakuna mtu aliyejitokeza kusema lolote juu ya kilichotokea.

UPELELEZI WA POLISI
ilikuwa kazi rahisi sana kumpata mtuhumiwa, polisi waliwasiliana na tigo, wakapata namba ya mwisho marehemu kuwasiliana nayo, wakamtafuta muhusika kwa ajiri ya mahojiano, muhusika ambaye ni girlfriend wa marehemu alionyesha ushirikiano ambao haukutegemewa kwa kuwapa polisi full data ya kilichotokea.

MUUAJI KUKAMATWA
Hii ilipelekea baba wa girlfriend kukamatwa kwa ajiri ya mahojiano ( akiwa prime suspect), alihojiwa na akakubali alichokitenda, siku mbili/tatu baada ya kuhojiwa alihojiwa tena na akakana kila kitu, ilikuwa kazi ngumu kumconvice binti kukana maelezo yake, lakini naye alikuja kana (nadhani alibananishwa na family members or alitishiwa maisha pia ikabidi a-surrender), ikawa ndio mwisho wa kesi.

BAADA YA TUKIO
Yakabaki maneno mtaani, baba wa girlfriend akapotea for some time mtaani, dereva wa boda boda naye akapotea mtaani for sometime pia, familia ya girlfriend ikabadili njia na kuanza kuzunguka as njia rahisi kufika kwao ilikuwa ni kupita kwa bibi wa marehemu (nyumba yake ipo barabarani)

HINTS:
  • Hii inatosha kwa leo. Huu ndio ukweli wa mkasa huu, si kwamba marehemu aliuawa na watu waliokodiwa but aliuawa na baba wa girlfriend wake.
  • Bibi alumuachia Mungu kesi hii, si kwamba baba wa girlfriend ana hela au uwezo zaidi ya bibi, naamini huyu bibi is much wealthier than baba wa marehemu, ila bibi ali-let it go, hakutaka mambo ya kesi.
  • Kigurunyembe ni mtaa ambao watu wake wanaushirikiano wa kimafungu, nyumba ya hii ina ushirikiano wa karibu na nyumba ya saba, nyumba ya kumi, n.k ndio maana hadi marehemu anazikwa no one knew the truth even when majirani wa girlfriend walisikia mikiki mikiki yote
  • Girlfriend yupo chuo pia, bado hajamaliza mwaka wa pili, ilikuwa waingie wote chuo na marehemu though vyuo tofauti.

(ANGALIZO HII NI STORY YA KWELI) ilikuwa mwaka 2011 mwezi wa tisa mnamo saa tatu na nusu usiku taraitibu napiga hatua kuelekea nyumbani mara ghafla simu ikaitwa kuangalia ni ya dada yangu aliyepo morogoro, nikapokea kwa furaha maana sijawahi kuwasiliana kwa muda murefu, maskini kuona tu dada anaongea kinyonge furaha ikaniisha ghafla, kumsikiliza ndo akaniambia habari za kuhuzunisha kuwa mdogo wangu amekutwa amekufa.

ninayemwongela hakuwa mdogo wangu tumbo moja bali alikuwa mtoto wa kwanza wa mama yangu mdogo anayeishi huko kigurunyembe morogoro. baba wa mdogo wangu huyo alifariki miaka mingi iliyopita hivyo mama yangu mdogo ndo alihangaika kuhakikisha mtoto wake anapata mahitaji yake yote ya msingi ikiwepo elimu. mdogo wangu huyo mauti yalimfika huku zikiwa zimebaki siku tatu kuriport chuo cha mzumbe tawi la mbeya alikokuwa amechaguliwa kusomea masomo ya sheria kwa ngazi ya degree.

MAZINGIRA YA KIFO
mdogo wangu siku ya tukio aliaga anaenda kwa bibi yake kuchukua baadhi ya mahitaji kwa ajiri ya safari ya kwenda chuoni, inavyosemekana alipokuwa akirudi ndipo alipotekwa na vijana ambao hatujui idadi yao na kwenda kumuua na kisha kumtupa barabarani.
KWA NINI ALIUWAWA
Inavyosemekana mdogo wangu alikuwa ana uhusiano na binti mmjoa lakini baba yake kumbe hakufurahishwa na uhusiano huo wa mwanawe na mdogo wangu huyo hivyo basi akaamua kumtumia vijana ili wayatekeleze mauaji yale

NANI ANATUHUMIWA
mtuhumiwa wa mauaji yale bila kuficha ni ni DIWANI MMOJA KATA NIMESAHAU PALE MOROGORO MJINI AMBAYE NIMEFANIKIWA KUTAJIWA JINA LAKE MOJA ANAITWA KIMARO ( KWA WALE WAKAZI WA MOROGORO WATAKUWA WANAMFAHAMU HUYU)

JE KESI INAENDELEAJE
Baada ya kutuhumiwa kwa haya mauaji huyu diwani alikamatwa lakini aliachiwa baada ya muda mfupi bila sababu maalum, ndugu zangu waliopo morogoro walipojaribu kuhoji walipewa vitisho na askari polisi hivyo basi kama familia walikaa kikako wakaamua wamwachie mungu maana wao kama wao hawakuwa na uwezo wa kushindana kipesa na diwani huyo ambaye inasadikika alitumia pesa kutoka

KWA NINI ATUHUMIWE DIWANI KIMARO
diwani huyo alituhumiwa baada ya kutajwa na wale vijana ambao wanasemekana walitekeleza mauaji hayo, kumbuka damu ya mtu ni nzito maana siku ile ile ya msiba kuna kijana alikuja kufuatilia mauaji waliyoyafanya, kijana huyo alikamatwa na akawataja wenzie ambao kwa pamoja walimtaja diwani kimaro.

HIVYO NDIVYO MAPENZI YALIVYOMTOA UHAI MDOGO WANGU, BABA WA BINTI KWA SABABU ALIKUWA HAMTAKI MDOGO WANGU NDO AKAAMUA AMTUMIE WAUAJI AMBAO BILA WOGA WALIMUUA NA KUMTUPA BARABARANI
MUNGU AMLAZE MDOGO WANGU HUYO MAHALA PEMA PEPONI AMENI
 
nashukuruni sana wanajf kwa ushauri wenu, mungu awabariki sana
 
kisheria hii kesi ngumu, kwa kuwa aliye andika akijiita ndugu wa marehemu inaonekana hawajui kwa undani ishu nzima ilivyokwenda. Amemzungumzia diwani lakini katika andika lililo fuata hakuna diwani aliyetajwa. katika andiko la kwanza amezungumzia vijana walio kamatwa ambapo mmoja wao alijileta mwenyewe msibani na akakiri kuhusika akawataja wenzake, lakini habari hii kwenye chapisho la pili haipo. Kuna mchanganyo mwingi wa kitaarifa. Labda ni ishu mbili tofauti
 
Back
Top Bottom