Mapenzi ya "ningefanyeje" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi ya "ningefanyeje"

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by tindikalikali, Jun 24, 2011.

 1. tindikalikali

  tindikalikali JF-Expert Member

  #1
  Jun 24, 2011
  Joined: Jan 14, 2011
  Messages: 4,883
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 135
  Huwa inatokea watu wanakuwa wapenzi kwa kujilazimisha/kuhofu asipokubali itakuwaje. 1.Chukulia mfano, dada aliye katika matatizo makubwa, mkaka akatokea akamsaidia kwa kila hali 2. Chukulia watu waliosoma pamoja/waliishi mtaa mmoja, leo wanakutana mbali baada ya miaka mingi. Siku zote mapenzi ya ningefanyeje huendana na utetezi wa "Mungu ametupangia", je mapenzi ya "ningefanyeje" yasiyo na option ya kukataa nayo ni mapenzi ya kweli? Nawasilisha
   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Yana maisha marefu kama ya nzi!
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,670
  Trophy Points: 280
  Yana maisha marefu kama ya nzi!!!!
   
 4. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #4
  Jun 25, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...mambo ya shingo upande hayo,...kujilazimisha hakudumu!....ipo siku utachoka ku pretend, hapo hata ufanyeje huwezi rudisha moyo nyuma.

  Hiyo "ningefanyeje," iwapo mtumiaji atalitumia hilo neno kukwepa responsibility ya maamuzi yake sidhani kama ni mapenzi ya kweli, Unless mtumiaji anamaanisha "ningefanyaje nami nilimpenda/nampenda!"
   
 5. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #5
  Jun 25, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Hayo maneno wanayo wanawake walioolewa na mijitu ya ovyo

  utasikia ningefanyaje sasa....
  Arrgh,,,,,,,,,,,,
   
 6. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #6
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Nafikiri hii huwatokea sana watu wanaokutana mbali na makwao, hasa wanaoenda nje ya nchi kusoma, mnajikuta mko wawili, mmetokea nchi moja, basi mnajiingiza kwenye mapenzi bila kujiuliza mioyo yenu inasemaje, mwisho wa siku mmoja akiwahi kurudi anaendelea na mahusiano yake ya zamani huku bongo.....hii ipo sana mkuu, hata kwenye misaada, mtu anapata kusaidiwa na kuona njia pekee ya kutoa shukrani ni kuwa na huyo mtu bila kuangalia kama anampenda kidhati
   
 7. Tutor B

  Tutor B JF-Expert Member

  #7
  Jun 25, 2011
  Joined: Jun 11, 2011
  Messages: 6,405
  Likes Received: 2,111
  Trophy Points: 280
  Hayo ndo mapenzi ya kweli kwa kuwa yana sababu ya msingi ambayo ndo hiyo inamfanya mpendwaji aseme "ningefanyaje"
  Wengi wa hivyo ni kama wale walopeana mimba wakalazimika kuoana - ikitokea mmoja akamiss behave mwenzake humkumbusha walikotoka.
   
 8. Shantel

  Shantel JF-Expert Member

  #8
  Jun 25, 2011
  Joined: Feb 7, 2011
  Messages: 2,021
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu hii logic ya wapi
   
 9. Mwanakili90

  Mwanakili90 JF-Expert Member

  #9
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 1,571
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  hua wanasema mapenzi huoata popote,namaanisha hamna mahali maalum pa penzi kuchipuka,kufahamiana kabla ni moja ya sababu shawishi inayopelekea wawili hawa kua karibu na kujenga penzi lao,kujuana kabla kunakua kama CATALIST ya penzi.

  Swala la penzi la kua wanapendana kiukweli au la ni mambo ya mioyo yao.hatuweZI hukumu mwenendo wa penzi kwa kutizama kujuana kwa wahusika.
  Si vema kuusemea mioyo ya wapendanao.


  My take:mapenzi popote.
   
Loading...