Mapenzi ya mzazi kwa mtoto!!

Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,469
281
Nimeona, hasa miaka ya karibuni...

Wazazi wengi.. hasa wenye ukwasi... wanajitahidi kuwapa mazingira 'bora' watoto wao... watawafanyia kila kitu kiasi kwamba mtoto anakua kila kazi ya mikono anafanyiwa, shule ana gari la kumpeleka, chapaa ndo usiseme. akirudi nyumbani, kila kazi afanyiwa na shambaboi, hausigeli au ahata ndugu zake(binamu,wapwa n.k)!!!

Hapewi hata mara moja nafasi afanye mambo yatakayomfanya asiwe tegemezi ana aweze kusimama pekee..

Mwisho wa yote... mtoto anatia aibu ukubwani!! Uongo?!:smile:
 
hiyo kweli! badala ya kuwatengeneza watoto wazee wengine wanawaharibu

mfundishe mtoto kuwa na responsibilities nyumbani za familia au japo zinazomhusu yeye.
 
wazazi tunaona kama tunawasaidia watoto kumbe tunawaharibu..Kuna binti alilelewa katika mazingira hayo hajui kufua,kupika wala kazi yoyote ya mkono.Bad lucky ile anamaliza chuo wazazi wote wakawa wamefariki ghafla .anapata tabu sasa na kuwalaumu wazazi wake kwa nn hawakumfundisha toka mwanzo
 
hiyo kweli! badala ya kuwatengeneza watoto wazee wengine wanawaharibu

mfundishe mtoto kuwa na responsibilities nyumbani za familia au japo zinazomhusu yeye.

Mathalani jr @ 3yrs anajua akishamaliza kula ama kunywa lazima ahamishe vyombo alivyotumia na kunawa mikono yeye mwenyewe!
Sasa ni lazima asuuze vyombo hivyo na vitu kama soksi anafua hiyo ni 5 yrs (hata kama mtu mzima atarudia baadaye ) he gets the message ni jukumu lake!

Kumpenda mtoto na kutomfundisha kuwa responsible ni kumwangamiza kama sio kumuua!
 
tatizo la wazazi wengi hawajui/hatujui ya kwamba mtoto analelewa na wazazi,
daima yuko kwenye transitional kuelekea kule anakoenda ambako huko
hakutakuwa na mama wala baba zaidi ya kuwa na mme/mke wake
na kutengeneza nyumba yake, yaani tunawachukulia kana kwamba tutazeeka nao
mikononi mwetu, tujifunze kuwaandaa wanetu na kuwapa nafasi ya kujifunza kwa ajili ya miji waiendeayo baadae
 
wazazi tunaona kama tunawasaidia watoto kumbe tunawaharibu..Kuna binti alilelewa katika mazingira hayo hajui kufua,kupika wala kazi yoyote ya mkono.Bad lucky ile anamaliza chuo wazazi wote wakawa wamefariki ghafla .anapata tabu sasa na kuwalaumu wazazi wake kwa nn hawakumfundisha toka mwanzo

My self i found one lady in Nation service she doesn't even kuwasha karabai hajui kiberiti kinawashwaje lakini baadae alikuja kujua baada ya suruba za JKT
Lakini nawakiharibika wanaharibika vibaya.....kama niwakiume watu wanpua mgongoni kwake!!!amini usiamini hawa mimi nimekulia DC USA, baba H.E Amb,Prf Dr..............kwasana tu mbona wengi tunao!!:shock:
 
Back
Top Bottom