prettydiva
Senior Member
- Feb 19, 2014
- 101
- 39
Habari wana jamvi...kuna siku niliwah kupost kuhusu kuwa na jamaa ambaye nlmpenda lakin yeye hakuwa na mapenzi ya kweli kwangu.Leo nmekuja kwenu kuwashuhudia kuwa wapo wanaume wenye mapenzi ya kweli na wenye kujua thamani ya mwanamke,kuna kijana nipo nae kwa sasa ambaye alionyesha kunipenda toka tuko wote chuo kikuu japo tulikuwa kozi tofauti hakuonyesha kuchoka kunipenda n hata nlipokuwa naumizwa na maisha yeye alikuwa nami kwa zaidi ya miaka miwili alinivumilia,hakupenda aone machozi yangu lakini mimi sikuwa tayari kumpa moyo wangu.Toka nimpe moyo wangu amekuwa furaha kwangu,yan ananijali hadi nashangaa nlkuwa wapi siku zote,ananipa chochote hata bila kuomba nami zawadi kubwa ni kumpa penzi la dhati na la kweli. USHAURI: Wasichana mnaotendwa kwenye mapenzi msife moyo ipo siku mtakutana na wanaume sahihi kwa maisha yenu,endeleeni kuomba Mungu.