Mapenzi ya Kibongo

Mapenzi ya Kibongo

jrmlaurence

Member
Joined
Dec 2, 2010
Posts
80
Reaction score
57
Mapenzi ya Kibongo ni ya aina yake duniani, hivyo nimeona leo nitoe somo ili kuwasaidia mayanki namna ya kuishi kwa furaha katika mapenzi ya Kibongo.

Kwanza mapenzi ya Kibongo hayashughuliki na mambo madogomadogo kama eti kupeana maua au eti kutembea beach mmeshikana mikono, hizo ishu ni za kwenye sinema tu au labda Ulaya.

Hapa watu wako bize wana hangaika na maisha, mambo hayo ni ya wazungu. Wapenzi wa kibongo wa ukweli huwa hawahangaiki kuelezana eti I love you au nakupenda sana , aaa wapi, mdada akiwa na mapenzi ya ukweli utaona anampikia mpenzi wake chakula cha ukweli, jamaa anapokula msosi anajua kuwa kweli huyu mdada ananipenda, hapo hata kama amewakaribisha mabest wake, utasikia ‘Aisee huyu demu anakupenda sana kakupikia chakula kitamu hivi'.

Katika mapenzi ya Kibongo bili zote mwanaume lazima ulipe. Mkiwa mmekaa baa mmeshakula na kunywa sana hata kama mwanaume unaona mdada kaanza kushika pochi kama vile anataka kulipa jua ni geresha tu, anajua unampenda hivyo utalipa tu. Hata wale wadada waliowahi kuishi Ulaya wanajua system ya Bongo ni mwanaume kulipa.

Katika mapenzi ya ukweli ya Kibongo, mdada hata amkute bwana wake na binti mwingine, hata kama wamekaa kihasara ili kuonyesha mapenzi ni muhimu kumezea, tena unafanya kama hujaona chochote, hii itamfanya jamaa ajue unampenda sana, japo kuwa mapenzi ya Kibongo yana mipaka mdada huruhusiwi kukutwa amekaa kihasara na mkaka.

Ili mwanaume wa Kibongo aonyeshe ana mpenda sana mpenzi wake wivu huwa muhimu, mwanaume yoyote, hata kama ndugu marufuku kumsalimu au kutuma mesej au kuchat kwenye simu, hasa giza likianza kuingia.

Jambo lingine muhimu katika mapenzi ya Kibongo, mwanaume wa Kibongo marufuku jikoni, kwa sababu mdada anakupenda hata ukirudi saa kumi za usiku na unamkuta ana malaria kali, lazima ajikongoje aingie jikoni, mwanaume ukikosea tu uanze kuingia jikoni kupika ujue umeanzisha mtindo utakaokukosti akipona atadai uendelee kupika na kuosha vyombo na kadhalika a.k.a mme -----

Hahahahaha Chunga sana kijana
 
Ila hilo la msosi wabongo wengi ndio kipimo cha upendo kipindi cha u junior Bachelor
 
Mi napika! Nangoja apone halafu anileteee huo upuuzi wa kudai eti endelea kupika i think yeye ndo ataenda kushtaki ukweni ntakachomfanya mfyuuuuuuuuuuuuuuuuuu
 
Aiseee hilo lakufanya haujaona wakati umeona ni unafiki.Mie siwezi lazima niulize whats going on here?Ila siwezi kupretend kuwa sijaona
 
Mengi uliyosema yana ukweli na tunaweza sema ni social norm ya kibongo lakini sidhani kama ni busara kufikiria kama mapenzi yote ya kibongo yapo hivyo. kwa mfano mimi binafsi sioni tatizo hata kidogo au kujisikia inferior kumpikia wifey na kids, nilivyokuwa kwenye ujana nilikuwa insecure kuonyesha hisia zangu kwa wapenzi wangu ili mradi tu nisionekane nimependa sana,kutembea beach na mpenzi wako mmeshikana mikono kuna raha yake na inaleta ukaribu sana na confidence kwa wapenzi. Kwa kifupi mapenzi hayana formula
 
mengine yanakubalika hilo la kuingia kumpikia mume wakati naumwa hoi no kama hawezi kupika aje na takeaway
Hayo ni mapenzi au ubinafsi uliopitiliza, hakuna raha kama kumhudumia your lady akiwa mgonjwa. napika mwenyewe, ye aseme tu anataka kula nini
 
aisee.....hapo kwenye kupika kwangu kupo tofauti. siku nikiwa home basi tunapika pamoja. yeye akipika chakula huku mi napika mboga. na nimeshazoea hivyo sioni kama kuna tatizo. ni mapenzi tu.
 
aisee.....hapo kwenye kupika kwangu kupo tofauti. siku nikiwa home basi tunapika pamoja. yeye akipika chakula huku mi napika mboga. na nimeshazoea hivyo sioni kama kuna tatizo. ni mapenzi tu.
Washkaji au ndugu wakitokea vipi unaogopa kuonekana unapika au upo comfortable tu na maamuzi yako?
 
hata kama kukiwa na wageni. nitaingia jikoni na tutapika pamoja. isitoshe ndugu na marafiki wanajua kuwa me ni mtu wa aina gani. ni kawaida sana.

Dizain flan hivi kumpikia wife halafu likiiva umlishe inapendeza sana mkuu,

Ubaya unakuja pale wife anaacha kuapreciate msosi wako...duh!!! Kaaibu flan kanakujia,unaskia bora niingie jikoni mwnyw pata picha kuna wageni ???
 
Dizain flan hivi kumpikia wife halafu kikiiva umlishe inapendeza sana mkuu na ajue kudeka sasa....raaaaha tupu mkuu,

Ubaya unakuja pale wife anaacha kuapreciate msosi wako...duh!!! Kaaibu flan kanakujia,unaskia bora niingie jikoni mwnyw pata picha kuna wageni hapo ???
 
Dizain flan hivi kumpikia wife halafu likiiva umlishe inapendeza sana mkuu,

Ubaya unakuja pale wife anaacha kuapreciate msosi wako...duh!!! Kaaibu flan kanakujia,unaskia bora niingie jikoni mwnyw pata picha kuna wageni ???

teh! hata kama bahati mbaya kikatoka vibaya,hawezi tamka maneno hayo. tena mbele ya wageni! labda tukiwa peke yetu.
 
Hivi mapenzi bado yapo eeeee.......

Aiseee........ Sikuwa nafahamu kama mapenzi bado yapo.....

Nafahamu usanii wa mapenzi ndio upo.
 
Hahaa wakikalili kusaidiwa kumbe hatari eeee....

Bushoke noma
 
Back
Top Bottom