MAPENZI YA FEZA & O'NEAL ndani ya BBA: UNASHAURI NINI?

SSH2025_2030

JF-Expert Member
Joined
Jul 9, 2012
Posts
9,661
Reaction score
9,814
Wadau natumaini baadhi yenu mnafuatilia Reality Show ya Big Brother Africa (BBA) season 8 inayoendelea huko South Africa. Mshiriki mmojawapo toka Tanzania FEZA ameanza mahusiano na O'Neal kutoka Botswana kusema ukweli walianza vyema lakini hivi karibuni kumekuwa na misuguano ya kila aina hususani O'Neal kuwa Insecured na Melvin (Nigeria) na kumlaumu kila mara Feza. kila mara Feza amekuwa mhanga na kuishia kulia. Je uonavyo unafikiri kuna mapenzi ya Kweli kati yao (Feza & O'Neal?). Unashauri nini kifanyike kumsaidia Dada Feza kushinda 300,000 USD (Tsh. 480,000,000/=)?
 
Feza ameharibu kuanzisha uhusiano na huyu O'Neal amepoteza direction ya GAME maana jamaa anamchanganya tu. Mi nafikri Feza aachane nae tu a-concentrate kwenye game ili a-win hizo pesa. JAMAA (O'Neal) ana wivu na tabia za kike za kususa pia hajali (hana caring at all). natabiri Feza atakuja kuanzisha uhusiano na BIMP (Mshiriki kutoka Ethiopia) maana huyu mu-Ethiopia very understanding, caring tofauti na na hili zee O'Neal.
 
siku zenyewe za kukaa huko ni 90
sasa sijui kama muda huo unatosha kumfahamu mtu, background yake na mambo mengine muhimu
...labda tusubiri wadau waamke
 
Muacheni aambulie japo kupata penzi maana ashaona uwezekano wa kuchomoka na zile za jina lake ni ngumu.
 
.......msisahau kwamba, it is only a Game hiyo BBA. Watu ukiwafungia bila outside influence wanafanya maamuzi tofauti ku "survive!" Ile boredom!
 
FEZA has been boring kwakweli..amesahau kabisa kuwa yuko kwenye game. Next eviction she is out.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…