Mapenzi ya dhati katikati ya umasikini.

Mapenzi ya dhati katikati ya umasikini.

IAmShedeOne

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2015
Posts
202
Reaction score
385
MAPENZI YA DHATI KATIKATI YA UMASIKINI.

SIKU moja wakiwa wamejilaza kitandani, mke alimwomba mumewe amnunulie chanuo kubwa kwa ajili kuchania nywele nyingi ili kuzipendezesha. Kiuchumi, hali ya mume ilikuwa dhoful'hal, asingaliweza kugharamia chanuo aliloombwa.

Kwa simanzi na huzuni kubwa, mume alimjibu mkewe, "Mpenzi wangu, si kama sitaki upendeze, la hasha. Hali yangu kifedha ni mbaya sana. Hebu tazama, ni zaidi ya mwezi sasa tangu mkanda wa saa yangu ya mkononi ikatike, lakini nimeshindwa hata kununua mkanda mwingine."

Kama ameshindwa tu kujinunulia mkanda wa saa ulioharibika, ataweza kununua chanuo kubwa? Siku ikapita ilhali mke akiwa mnyonge kabisa. Lakini kwa kawaida, wanamume si watu wa kukubali kushindwa na kuonesha udhaifu mbele ya wake zao. Kwa kuumizwa na kitendo cha kushindwa kumnunulia mkewe chanuo tu, siku iliyofuata baada ya kutoka kazini, mume alipita mjini akaiuza ile saa yake, na fedha aliyopata akaenda kumnunulia mkewe chanuo.

Jioni ya siku hiyo, mume aliingia ndani akiwa na shauku ya kumshangaza mkewe kwa kumletea zawadi ya chanuo alilohitaji, lakini katika hali asiyotegemea alimkuta mkewe akiwa amenyoa nywele zake zote. Kuona chanuo alilonunua kwa gharama ya saa yake, likiwa halina kazi tena, kulimuumiza sana mume.

Alipomuuliza mkewe kwanini aliamua kunyoa nywele zake, akiwa ametabasamu mke alijibu: "Nimeuza nywele zangu ili kukununulia mkanda mpya wa saa yako!"

Mume aliupokea mkanda wa saa huku akibubujikwa machozi ya furaha, wakati huo mke naye akipokea chanuo lake huku machozi yakitengeza mifereji mashavuni mwake. Kila mmoja alikubali kuuza kitu chake cha thamani ili kumridhisha mwenzi wake.Ooh! Mahaba ya sayari gani haya.
 
Safari ya pluto
 
Huo uzembe wa kupenda sana Dar haupo!
Tasnia hiyo imekosa washiriki, njaa za wabongo zimefanya mapenzi ni mradi wa kibiashara.
 
Back
Top Bottom