msafwa93
JF-Expert Member
- Jul 2, 2011
- 4,840
- 6,148
Nilipoingia katika mahusiano naye nilimuamini,nikampa kila kitu nilichoweza. Nakumbuka enzi zile nyumbani tulikuwa tuna ngombe, niliiba maziwa kila siku na kumpelekea kwao.
Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi,Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake,Akanifany a nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe.
Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini
nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata
nilipokuwa katika siku zangu.
Kweli nilikuwa msomi na niliyajua
madhara ya kufanya hivyo lakini
sikutaka kumuudhi huyo
niliyeamini kuwa ni mume
wangu. Nilipenda tututmie kinga
lakini aliipinga sana. Nikapata
mimba ya kwanza!! Hakuwa na
pesa lakini alinilazimisha niitoe.
Nikaiba pesa nyumbani
nikafanyaalivyo taka. Kwa mara
ya kwanza nika toa mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa
ni yeye atakuja kunioa na
atanifichia aibu hii. Nilitegemea
sasa tutaanza kutumia kinga.
Lakini hapana haikuwa hivyo.
Aliendelea kunilaghai. Tayari
aliujua udhaifu wangu. Alinishika
hapa na pale. Nikishtuka tayari
amefanya anavyojua. Pombe
kidogo na nyingine kidogo.
Nikazoea lakini nikawa na wahi
kulewa. Akautumia udhaifu huu
kunifanyia jambo baya
lililonifanya niandike haya
kwako. Akaniingilia kinyume na
maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa
mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea
eti hataki nipate mimba tena,
hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo
alikuwa mume wangu. Miaka
ikapita, ule urembo wangu
niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa
mara kutoka kwake zikatoweka,
akawa mkali sana kwangu.
Hakutaka niende kwake. Wakati
huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa
ya mkopo ikitoka ananitafuta na
tunakuwa marafiki tena.
Anasema ananipenda na atanioa.
Ananilewesha na kunitumia
kinyume na maumbile. Pesa
ikiisha na mapenzi yanaisha
nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha
wasichana waziwazi. Ningesema
nini mimi? Ninajua alishindwa
kusema neno moja tu. Tuachane!!
Nilijua tayari ameniacha!!! Afya
yangu ikadolola sana,
nikalazimika kwenda kupima
hospitali. Sikuwa na virusi.
Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata
mwanaume mwingine. Huyu
alikuwa ananijali sana. Nikaanza
kumsahau yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo
akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa. Akanioa kweli.
Maisha yakaanza. Mwaka wa
kwanza, mwaka wa pili na hadi
wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu
sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua
kwenda hospitali. Nikaambiwa
kizazi changu kiliharibiwa kwa
kutoa mimba mara kwa mara. Pia
mapenzi ya kinyume na
maumbile yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka
yule aliyeuleta uchungu huu
kwangu. Dunia haikuwa mahali
pangu sahihi. Nimekuandikia
barua hii mdogo wangu.Uisome
mwenyewe!! Lakini uwasimulie
wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka
wasichana wa kileo
wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao. Waambie
watakufa kwa mateso kama
mimi. Wasipokusikiliz a usijisikie
vibaya maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia
lolote kuhusu yule mume
mdanganyifu . Sitajiua lakini
nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa
u mwandishi. Japo kwa sasa u
mtoto mdogo najua utaipata
nafasi siku moja ya kuwafikishia
wasichana hawa. Usilie kwa
sababu nitakufa. Lia kwasababu
mwanaume mwenzako
AMENITENDA HIVI!!! TAFADHARI
TAFAKARI'' MWANAUME SIO
NDUGU YAKO
Akanenepa!! Penzi letu likawa huru alipoanza maisha yake mwenyewe. Sikuwa najua lolote kuhusu mapenzi,Alinifundisha. Nikaegemeza maisha yangu yote kwake,Akanifany a nikawa mtumwa wa ngono kila nikienda chumbani kwake.
Kama haikutosha sasa akaanza kunifundisha kunywa pombe.
Niliamini kuwa ndiye mume wangu mtarajiwa, kwa nini
nikatae? Nilimkubalia kila kitu.
Alinilazimisha ngono hata
nilipokuwa katika siku zangu.
Kweli nilikuwa msomi na niliyajua
madhara ya kufanya hivyo lakini
sikutaka kumuudhi huyo
niliyeamini kuwa ni mume
wangu. Nilipenda tututmie kinga
lakini aliipinga sana. Nikapata
mimba ya kwanza!! Hakuwa na
pesa lakini alinilazimisha niitoe.
Nikaiba pesa nyumbani
nikafanyaalivyo taka. Kwa mara
ya kwanza nika toa mimba.
Haikuniuma sana!! Niliamini kuwa
ni yeye atakuja kunioa na
atanifichia aibu hii. Nilitegemea
sasa tutaanza kutumia kinga.
Lakini hapana haikuwa hivyo.
Aliendelea kunilaghai. Tayari
aliujua udhaifu wangu. Alinishika
hapa na pale. Nikishtuka tayari
amefanya anavyojua. Pombe
kidogo na nyingine kidogo.
Nikazoea lakini nikawa na wahi
kulewa. Akautumia udhaifu huu
kunifanyia jambo baya
lililonifanya niandike haya
kwako. Akaniingilia kinyume na
maumbile. Alinilawiti!!
Nilishindwa kumshtaki popote.
Nikavumilia kwa kuwa alikuwa
mume wangu mtarajiwa. Mume
asiyejulikana hata kwa wazazi.
Mchezo ule ukaendelea. Akajitetea
eti hataki nipate mimba tena,
hivyo hiyo ni mbinu mbadala.
Najuta kumuamini!! Lakini huyo
alikuwa mume wangu. Miaka
ikapita, ule urembo wangu
niliozoea kuuona katika kioo
ukatoweka, simu za mara kwa
mara kutoka kwake zikatoweka,
akawa mkali sana kwangu.
Hakutaka niende kwake. Wakati
huo nilikuwa nasoma chuo. Pesa
ya mkopo ikitoka ananitafuta na
tunakuwa marafiki tena.
Anasema ananipenda na atanioa.
Ananilewesha na kunitumia
kinyume na maumbile. Pesa
ikiisha na mapenzi yanaisha
nabaki mwenyewe katika msoto.
Sasa akaanza kubadilisha
wasichana waziwazi. Ningesema
nini mimi? Ninajua alishindwa
kusema neno moja tu. Tuachane!!
Nilijua tayari ameniacha!!! Afya
yangu ikadolola sana,
nikalazimika kwenda kupima
hospitali. Sikuwa na virusi.
Nikapewa ushauri nikautumia.
Siku zikasonga nikampata
mwanaume mwingine. Huyu
alikuwa ananijali sana. Nikaanza
kumsahau yule aliyenitenda.
Nilipomaliza chuo
akajitambulisha nyumbani na
alitaka kunioa. Akanioa kweli.
Maisha yakaanza. Mwaka wa
kwanza, mwaka wa pili na hadi
wa tatu. Sikuwa nabeba mimba.
Mume wangu alikuwa mvumilivu
sana, hakuwahi kunilaumu. Lakini
niliumizwa na mawifi. Nikaamua
kwenda hospitali. Nikaambiwa
kizazi changu kiliharibiwa kwa
kutoa mimba mara kwa mara. Pia
mapenzi ya kinyume na
maumbile yamenivuruga kabisa.
Nililia sana huku nikimkumbuka
yule aliyeuleta uchungu huu
kwangu. Dunia haikuwa mahali
pangu sahihi. Nimekuandikia
barua hii mdogo wangu.Uisome
mwenyewe!! Lakini uwasimulie
wengi baada ya kifo changu.
Uwasimulie bila kuchoka
wasichana wa kileo
wanaodanganyika na kufanya
mambo magumu kuwaridhisha
wapenzi wao. Waambie
watakufa kwa mateso kama
mimi. Wasipokusikiliz a usijisikie
vibaya maana hata mimi nilikuwa
siwasikilizi watu waliponambia
lolote kuhusu yule mume
mdanganyifu . Sitajiua lakini
nitakufa kabla ya wakati!!!
Nimekuandikia wewe kwa kuwa
u mwandishi. Japo kwa sasa u
mtoto mdogo najua utaipata
nafasi siku moja ya kuwafikishia
wasichana hawa. Usilie kwa
sababu nitakufa. Lia kwasababu
mwanaume mwenzako
AMENITENDA HIVI!!! TAFADHARI
TAFAKARI'' MWANAUME SIO
NDUGU YAKO