Mapenzi siyo chanzo cha kipato chako

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,037
Hanari za asubuhi wapendwa. Ni matumaini yangu kwamba haujambo wote humu ndani.

Napenda kutumia wasaa huu kuwajulisha, kuwashauri na kuwasihi dada zetu, wadogo zetu wa kike kwamba mapenzi siyo chanzo cha kipato chako.

Unapoingia katika mahusiano ya kipampenzi na mwanaume jaribu kuweka mbali shida zako au umasikini wako mbali na mapenzi.

Msipende kugeuza mapenzi kama chanzo cha kujipatia kipato. Ukileta shida zako au umasikini katika mahusiano hayatudumu kamwe na pia ndiyo mwanzo wa kudharaulika na thamani yako itashuka.

Najua mpo ambao mtanipiga mawe sana kutokana na huu uzi ila ukweli ndiyo huo.

Umasikini wa baadhi ya wanawake umesababisha mwanaume ambaye hana hela katika jamii kuonekana hana thamani hata kidogo.

Umasikini wa baadhi ya wanawake umesababisha mahusiano yamekuwa magumu sana mtaani kwa sababu wanaamini kuwa kupewa pesa na wanaume ndiyo upendo wa dhati wakiwa wanajificha katika kichaka cha kuhudumiwa. Kama mwanaume hana pesa au kipato chake ni cha kusuasua huwa anapata taabu sana katika mahusiano. Utanyanyaswa na kuitwa majina ya kila aina.

Dada yangu, mdogo wangu wa kike hata wewe unaweza kupambana na ukapata hizo pesa zako kama ambavyo wanaume wanapambana kuzisaka.

Siku nikipata mtoto wa kike. Jambo la kwanza nitakalomfundisha mambo yafuatayo:-
a) Namna ya kuwa jasiri na mpambanaji katika kutafuta pesa zake yeye mwenyewe bila kutegemea kupewa na wanaume.

b) Nitamuelewesha kuwa kupewa pesa na mwanaume hicho siyo kigezo cha upendo hata kidogo bali hushusha thamani yako.

c) Mahusiano ya kimapenzi hayana uhusiano wowote na kupewa pesa na wanaume.

d) Ukipenda pesa za wanaume uchi wako utateseka sana hapa Duniani.

Mwisho, raha ya mahusiano mwanaume akuhudumie mwenyewe na siyo mwanamke kuwa ombaomba mpaka kero mfano umekutana na mwanaume leo kesho unamwambia sina hela ya kusuka, mara nitumie hela ya mafuta ya gari, mara mama yangu kule nyumbani anaumwa n.k

Nawatakia asubuhi njema na sikukuu njema kwa ndugu zetu waislamu.

Ahsanteni.
 
Ukizaliwa mwanamke Kuna ka upendeleo fulani hivi katika mahangaiko ya kutafuta maisha, miili yetu ilivyo laini na ndivyo nature inatupunguzia maumivu ktk utafutaji, tangu enzi za kale wanawake walipigana vikumbo kuwa na wanaume wenye nyadhifa, wafalme, mitume na manabii ili kuokoa jamii zao,

Sema siku hizi imezidi lakini huo ndio uhalisia
 
Wanaishia huku, ila naamini mwanaume halisi lazima amlee mwanamke aiseee. Siiamini haya mambo ya 50/50

IMG_20211002_084829.jpg
 
Ukizaliwa mwanamke Kuna ka upendeleo fulani hivi katika mahangaiko ya kutafuta maisha, miili yetu ilivyo laini na ndivyo nature inatupunguzia maumivu ktk utafutaji, tangu enzi za kale wanawake walipigana vikumbo kuwa na wanaume wenye nyadhifa, wafalme, mitume na manabii ili kuokoa jamii zao,

Sema siku hizi imezidi lakini huo ndio uhalisia
Sawa lakini huwa mnatoa wapi nguvu za kudharau wanaume ambao wanapambana kusaka pesa wakati nyie wenyewe hamna kitu chochote?
 
Yaani iko hivi hela zetu tunatafuta na zenu tunazitaka pia.
Nikiwa na 20,000 haimaanishi 2,000 yako siitaki.
Naitaka vizuri ili niwe na 22,000
Na uJiandae nyeti zako kua za moto muda wote, mwisho wa siku unakongoroka mapema tu.
 
Mkiwa ndani ya ndoa kuhudumiana kiuchumi, kihisia, n.k. ni jambo la kawaida.

Tatizo linakuja mnapofanya mambo haya nje ya ndoa na utaratibu wa Mungu na jamii.

Lazima mje kulialia humu.
 
Yaani iko hivi hela zetu tunatafuta na zenu tunazitaka pia.
Nikiwa na 20,000 haimaanishi 2,000 yako siitaki.
Naitaka vizuri ili niwe na 22,000
Tukisema tuapply 50/50 mnayo ipigania kila siku, hapo kwa mujibu wa harakati zenu kila mtu anapata 11,000.

Ila ndio vile hamjui hata mnachokipigania mnataka 50/50 ila chako chako na changu chako.

Au 50/50 yenu ina chagua baadhi ya maeneo.
 
Na uJiandae nyeti zako kua za moto muda wote, mwisho wa siku unakongoroka mapema tu.
Ndiyo maana siku hizi asilimia kubwa ya wanawake wanaingiliwa kinyume na maumbile kwa sababu ya kupenda pesa.
 
Back
Top Bottom