Mapenzi sio pesa, Wala kuvumiliana ni kupendana

Mapenzi sio pesa, Wala kuvumiliana ni kupendana

kimpe

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Posts
910
Reaction score
862
Kumekuwa na msisimko mkubwa katika vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Kenya kuhusu taarifa ya msichana wa Kihindi aliyekiuka mila na tamaduni za jamii yake na kuolewa na kijana Mwafrika.

Msichana huyu wa kihindi anaitwa Sarika Patel, na ameolewa na kijana wa kabila la Bukusu Timothy Khamala, jambo ambalo ni nadra sana kwa watu wa jamii ya kihindi. Kilichowashangaza wengi ni kwamba Sarika ametoka katika familia tajiri na kuamua kuishi maisha ya walalahoi kijijini Kwa Sarika maisha ya umaskini ambayo Timothy anaishi sio kikwazo hata kidogo bali kwake hapo ndipo anapata raha na mapenzi ambayo anasema yamemridhisha na kumtuliza nyumbani kwa kijana Timothy.

Timothy alikuwa anafanya kazi nyumbani kwa kina Sarika kama mjakazi lakini akafutwa kazi na baba ya Sarika baada ya kupendana na msichana wake.Kwa sasa yeye ni tarishi katika ofisi hii ya jimbo.Sarika hana kazi Wawili hao sasa wapo katika pilka pilka za kuanza maisha mapya ila kwa pingamizi kali . Sarika Patel anasema kulingana na mila yao si sawa kuolewa na mtu asiyekubaliwa au kuchaguliwa na wawazi wako. Wachumba kwa kawaida hutoka jamii sawa. Mbali na tofauti ya rangi zao za ngozi , Sarika anatoka katika familia tajiri kinyume na mumewe Timothy ambaye ni mlalahoi. Licha ya tofauti hiyo, Sarika anasema wazazi wake hawangeweza kumzuia kumpenda amtakaye

Chanzo BBC Swahili





attachment.php




attachment.php





attachment.php

 

Attachments

  • Screenshot from 2014-08-07 15:54:19.png
    Screenshot from 2014-08-07 15:54:19.png
    70.5 KB · Views: 6,314
  • Screenshot from 2014-08-07 15:54:47.png
    Screenshot from 2014-08-07 15:54:47.png
    180.9 KB · Views: 6,740
Uyo muhindi duuuh......alikosa soko nni??
 
jamaa atakua na dushe la ukweli kwnye mgegedo anasimamia kucha... chezea urithi wewe!!! toto la kihindi limezoea kibamia kwanini asiweke kambi
 
interesting...yule aliegopa mdada wa Blackberry asome hii
 
Wote wana haki ya kuchagua na kuchaguliwa, pia haki ya kupenda na kupendwa
 
Niliwahi kupata motto wa kihindi pale A town tukaanza malavidavi kama mara mbili hivi kaka zake wakastukia walinikimbiza kama mbwa na huyu dada alifokewa sana siku hiyo hadi hivi leo sijamuona tena na simu yake haipatikani sijui walimpeleka wapi.
 
Huyu ni binti au mbibi?? Mbona kazeeka??
 
Ninavyo wajua wahindi ipo siku wataenda kumchukua huyo binti kikongwe wao,maana jamaa wana roho mbaya sana hapa bongo sijawahi kiona mswahili kamuoa muhindi,ila wao kuoa dada aaah,poa tu.
 
Niliwahi kupata motto wa kihindi pale A town tukaanza malavidavi kama mara mbili hivi kaka zake wakastukia walinikimbiza kama mbwa na huyu dada alifokewa sana siku hiyo hadi hivi leo sijamuona tena na simu yake haipatikani sijui walimpeleka wapi.

Yaani hapa hapa bongo unakubali kukimbizwa na mhindi !!!! Je ungekuwa india ingekuwaje
 
Back
Top Bottom