Duh! Nimecheka kufa! Huyu babu ana vituko! Kwanza pozi lake la uhakika. isitoshe naona amenyanyua "inkosikazi" juu kana kwamba anatangaza vita kwa yeyote atakayetaka kunyemelea mrembo wake: kwamba atakiona cha mtema kuni. Loh!
Haswa ukiongezea na kutembea vichupi vimetokeza nje ya suruali makalio yanaonekana pamoja na kuvaa "ear rings" na kusuka nywele, Ile nguvu ya ya uume kwishilia mbali wanafanana. Lakini angalia mzee alivyo poose! Nampa heko! Anahakika na jinsianavyotimiza wajibu mpaka wengine wanadhani kimwana kalewa kumbe karidhika mno!!!