Mapenzi ni Uwekezaji

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Wivu ni kipimo cha mapenzi. Na mapenzi ni uwekezaji. Hivyo kuna uhusiano wa karibu sana kati ya wivu na uwekezaji. Usipowekeza hisia zako kwa mtu huwezi kuwa na wivu na wale huwezi kumpenda kimapenzi. Kama utawezeza kidogo basi wivu utakuwa mdogo. Ila ukiwekeza kupita kiasi wivu utakuwa mwingi na utateseka sana na kumsumbua mno mwenzako. Suluhisho ni nini basi? Jibu lipo katika uwiano na mizani. Mtu anapaswa kuwekeza hisia, huba, muda na matarajio katika mizani yenye uwiano thabiti. Tahadhari: Kutingisha mizani ya uwekezaji katika mapenzi ni hatari. Kuwa na kiasi. Ujumbe huu umekujia kwa hisani ya Tafakuri ya Alasiri ya Komredi Kompanero.
 
kweli mwana...unawekeza vingi mmno kiasi cha kwamba mie kusema kweli kama wife au gf wangu atamegwa na jamaa mwengine sitasita kumuua huyo mwanamke.
 
kweli mwana...unawekeza vingi mmno kiasi cha kwamba mie kusema kweli kama wife au gf wangu atamegwa na jamaa mwengine sitasita kumuua huyo mwanamke.

du, mwenye hekima suleimani aliwahi kughani kuwa mapenzi yana nguvu kuliko kifo!
 
Unachaguaje sasa kuwekeza hisia?

hisia hukolea mno pale unapoziendekeza kupita kiasi, kwa mfano unaweza kujizoesha kuongea na mwenzi wako aliye safarini kila siku hivyo kujenga tabia ya kutarajia na kusubiria huo muda, siku ukikosa kuongea naye basi unakuwa na hamu sana naye - huko kuongezeka kwa hamu nako kunajenga hisia kali zaidi, na kadri unavyozidi kuendekeza kumkosa mwenzako ndivyo hisia zinavyozidi kujikita na zikifika pomoni unakuwa mtu unayejiona huwezi kumaliza siku bila kumuona au kutuongea na mwenzako achilia mbali kuishi bila yeye!
 
Oooh, now i get it! Kama mapenzi ni uwekezaji, basi competition inabidi iwepo ili kuendelea kukua sokoni eh? Kuna haja ya kuangalia peer investors na hata walio juu wanafanya nini ili kujua unajoungezaje.
Asante kaka. Nitakutafuta kwa ushauri, naona kuna kijana hapaofisini ananiangalia kwa jicho la paka alieona samaki wa kichina.
 
mmmh mie wakwangu huwa simuelewi ni wivu au nn. Anaweza kuwa na hasira na mm na hasemi whats wrong. Ukimuuliza anasema niko sawa. King'asti mzabzab hv hiyo hali nayo ni wivu au mapendo.? Eti Companero
 
Last edited by a moderator:
mmmh mie wakwangu huwa simuelewi ni wivu au nn. Anaweza kuwa na hasira na mm na hasemi whats wrong. Ukimuuliza anasema niko sawa. King'asti mzabzab hv hiyo hali nayo ni wivu au mapendo.? Eti Companero

kha!! pole sana maana ata mie sipendi kabisa mpenzi wa namna hiyo...sasa wataka mie nianze kukisia wewe unafikiria nini aua una emotions gani...mbaya sana bora uongeee. wivu bwana kupenda kubaya jamani acheni tuu
 
Uwekezaji katika mtazamo wa Uchumi huambatana na hisa. Pande tofauti humiliki mali na mapato yatokanayo na mali husika kwa uwiano tofauti wa asilimia.
Sasa kwa jinsi nijuavyo dhana nzima ya uwekezaji na nijuavyo namna mapenzi yashirikishavyo pande mbili zenye nia moja, sidhani kama kuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mapenzi na uwekezaji. Mkuu napinga hoja yako
 
Back
Top Bottom