Mapenzi ni huruma....tafsiri isiyo na shaka

Mapenzi ni huruma....tafsiri isiyo na shaka

Askarimaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2016
Posts
276
Reaction score
692
Habari zenu ndugu zangu,

Leo nimejisikia kuwapa tafsiri halisi ya neno mapenzi, wadogo zangu mliokuwa humu na watoto zangu pia kwa ujumla, kokote ulipo ukiulizwa nini maana ya neno MAPENZI, Jibu hivi " mapenzi ni huruma".
Yoyote anaekupenda lazima akuonee huruma, Je unataka kumjua mtu anaekupenda anakuwaje ? Jibu ni rahisi sana...ni yule anaekuonea huruma.

Mwanamke akikupenda sana hataki kukuomba pesa hovyo ni kwasababu anakuonea huruma.
Mwanamke msome mwanaume juu ya huruma yake kwako, ukiona hakuonei huruma jua hakupendi anakutumia tu. Ingawa yupo mwanaume anaekupa pesa sana kwa huruma yake kwako sababu amekuona una shida zinazohitaji pesa,

Pia yupo mwanaume anaekupa pesa sana kwasababu ya kutaka urahisi wa kukutumia, sababu wanaume wanajua penye uzia penyeza rupia.
Mwanamke kuwa makini kuchunguza ilo.

Je kuna mtu mwenye mapenzi na wewe kuliko mzazi wako ? Jibu ni rahisi. ..hakuna,
Je kuna mtu mwenye huruma na wewe kuliko mzazi wako? Jibu ni rahisi....hakuna, ivyo bas anaekupenda sana ndio anaekuonea huruma sana ( Mapenzi ni huruma)

Mtazame mama aliyenunua chungwa moja la mia mbili, anapolikata kati ale na mwanae, kipande kikubwa anampa mtoto wake yeye atakula kipande kidogo, hii ni kwasababu ya huruma kubwa aliyonayo kwa mtoto wake.

Je unampenda sana mwanao ? Akiumwa na wewe unaumwa pia,
Je unampenda sana mumeo ? Akiumwa na wewe unaumwa pia.
Ata jilani anaekupenda ni yule anaekuonyesha huruma ya hali ya juu,

ANAEKUPENDA LAZIMA AWE NA HURUMA NA WEWE.

Screenshot_20230221-001231.jpg
 
mapenzi ni nyege nyinyi hizo nyengine ni mbwembwe
 
Back
Top Bottom