Mapenzi ni asali, ni shubiri, vaa moyo imara

Mapenzi ni asali, ni shubiri, vaa moyo imara

kwamtoro

JF-Expert Member
Joined
Nov 15, 2010
Posts
4,922
Reaction score
3,245
Kwa nini mapenzi ni tata? Unaweza kujiuliza swali hilo. Ni kwa faida ya kila mmoja kwa sababu yanamhusu kila mmoja wetu. Ni matamu lakini ndani yake hutokea kuwa na ukakasi kama siyo maumivu.
Jiulize tena, kwa nini mapenzi yanasumbua? Mapenzi ni maumivu ya kichwa na moyo. Watu wengi waliomo ndani yake wanaweza kukupa ushuhuda wa mateso wanayoyapata kwenye uhusiano wao. Je, baada ya kuteseka huwa wanajiapiza kutorudi tena? La hasha! Wanajaribu mara nyingi, hawakomi. Unaweza kujiuliza ni kwa nini lakini ukweli ni kwamba pamoja na maumivu ambayo mtu anaweza kuyapata kwenye mapenzi, bado yanabeba hisia kubwa kabisa katika maisha ya kila binadamu.Maisha bila mapenzi hayajakamilika.
Kutokana na hilo, uwanja upo wazi kwako kujiuliza ni kwa nini kitu kitamu namna hiyo kikafanywa kuwa tata, jumlisha na maumivu ya hapa na pale. Uvumilivu ukizingatiwa, huyeyusha utata unaojitokeza hapa na pale.Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa nusu nusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo uhusiano unavyotaka.Mapenzi yanahitaji akili, utashi na fikra zako bila kusahau nguvu zote katika kuzalisha matunda ya kila siku kwenye uhusiano ulionao. Utata unaoonekana ni ule unaotokana na wenzi kutotimiza matarajio ya kila mmoja.Imetokea kuamini kuwa maneno ni mhimili wa kudumu kwa uhusiano na ngono husuluhisha migogoro ya muda mfupi.
Wapenzi wanaponuniana, endapo watakutana faragha, hasira zote hupotea. Hata hivyo, kwa bahati mbaya, ni zaidi ya kutosheka kimwili na utamu wa maneno mazuri.Kwa mfano, ndoa nyingi zinakumbwa na matatizo ya watu kushindwa kuwa wakweli. Mwanaume au mwanamke anaweza kusema ni kiasi gani mwenzi wake anamuumiza. Lakini mwisho wa mazungumzo hawezi kukiri kasoro zake ambazo pengine ndiyo chanzo cha kila kitu.Utata zaidi katika mapenzi ni kuwa inapotokea watu wanajuana kwa undani mno, hasa baada ya kuishi muda mrefu, ni hapo ndipo maneno hayawezi kufaa kitu, wala mchezo wa faragha hautaleta maelewano kwa maana hakuna kitu kigeni.Lingine la utata katika mapenzi ni kwamba huwezi kuficha tabia yako muda wote. Ukishazoeana na mwenzi wako hasa baada ya kuwa pamoja muda mrefu, utaanza kujiachia. Ni kipindi ambacho mmoja anaweza kuhisi amesalitiwa kwa sababu mwanzoni hakuona hivyo vitabia vya kuudhi, alifichwa.
MAPENZI NI KARATA TATU
Kuna msemo kuwa mapenzi hayashindwi ila watu ndiyo hushindwa na mapenzi. Tunarukia kwenye uhusiano bila kuwa na uhakika ni kiasi gani tunawapenda wenzetu na ni kwa kiwango kipi tumejiandaa kubeba majukumu.Mwisho wa siku tunafeli. Tatizo ni kwamba tunaanzisha uhusiano mpya bila kutatua kasoro zilizosababisha tukashindwa kwenye uhusiano na mtu wa kwanza.
Hapo nadhani unaweza kuona kwamba wakati mwingine mapenzi siyo tata ila wenyewe tunayafanya kuwa magumu.Tuna mambo mengi, ya kifamilia, kikazi, imani, dini, kabila, tofauti za kimtazamo na matarajio ya kila mmoja. Hatuko sawa. Tunapoingia kwenye uhusiano, fikra zetu zinakuwa zimejaa lakini ajabu ni kwamba tunapoingia kwenye uhusiano hatuyapi kipaumbele katika kuyajadili na kukubaliana. Hisia za juu hutupeleka kama vipofu.
Uhusiano wa kimapenzi wa watu wengi huanza pale ambapo mtu anajihisi yupo mpweke na anahitaji kampani. Wakati mwingine inatokea kwa sababu mtu anakuwa anakabiliwa na presha ya kuwa na mwenzake kwa kigezo kwamba umri umekwenda. Si kwamba amemuona mtu mwenye sifa anazohitaji.Umri ni kigezo kimoja lakini inawezekana ikawa mtu anataka kuwa na mwenzake kwa sababu ya msukumo wa nafasi yake kwenye jamii au kimila. Pengine ni dada sasa wadogo zake wameolewa yeye bado yupo tu. Au ni kaka, kwa hiyo kama kiongozi wa familia anaona bora aoe mapema kabla ya wadogo zake.Kama umeingia kwenye uhusiano kwa sababu ya presha ya aina hiyo, utawezaje kuwa na matunda sahihi? Kichecheo cha uhusiano wa kimapenzi kinapaswa kuwa mapenzi.
Mnapendana, kwa hiyo nyoyo zenu zinavutana kuingia kwenye sayari spesho.Usiwe na papara, angalia mahitaji ya moyo wako, weka mbele matarajio yako. Fikra zako uziweke wazi. Unapotafuta mwenzi hakikisha husumbuliwi na presha yoyote. Jambo ambalo unapaswa kuamini ni kwamba aliye ndani ya mawazo yako utampata kama ukijipa nafasi.

Muhimu zaidi ni kwamba mapenzi hayatoshelezi kwa uwajibikaji wa nusu nusu. Yanahitaji nidhamu na utekelezaji wa moja kwa moja kutoka moyoni. Yanayomhusu mwenzi wako ni vema uyabebe kama yako, hivyo ndivyo uhusiano unavyotaka.

CRAAAAAP! hivo ndivyoo WEWE unavotaka.
 
Haya maneno yangependeza sana kama ungesema ni mtazamo wako
But umeyaweka as if it is gospel, unatuelimisha, sisi tushibe tu.

Nakuelimisha hasa wewe. Si unaona ninavyo kuthamini
 
It takes a long time to really get to know a person. watu wengi tunakuwa mislead by what we see in the beginning inakuja kutucost baadae after the what u expect na wot u get is different.
When a relationship is new, people tend to be on their best behavior. hivo hatutakiwi ku focus only on the positive side,we should try kujua weakness,limitation na bad habits!!!!!!!!!!!!

A person may be quite different after the relationship is established au baada ya ndoa
You need to see the person clearly, the good and the bad ili ikitokea uwe tayar aware!!!!!!
 
.... Kichecheo cha uhusiano wa kimapenzi kinapaswa kuwa mapenzi.

Hapa ndipo wengi hukosea. Mara nyingi kichocheo cha mapenzi kwa baadhi ya watu wa kizazi hiki ni Pesa, Elimu, Umaarufu, Umri kufika, Kulazimishwa kutokana na kupeana mimba, msukumo wa ndugu na marafiki nk. Ndoa au mahusiano ya namna hii huwa hayana mapenzi katikati, huunganishwa na vitu fulani fulani ..
Hatma yake ni kuwa na ndoa zilizojaa machungu badala ya amani, furaha, upendo na faraja ....

Usaliti pia huanzia hapa, maana mtu anajikuta anaishi na mtu asiyempenda wala kumvutia, ila kwa sababu anapata huduma fulani, basi anakuwa tayari kuolewa/kuoa au kuwa naye kimaisha, ila moyoni anakuwa bado single and available! Na matokeo yake, baada ya muda anaanza kuwa na nyumba ndogo au ki-serengeti ...
Huu ni mojawapo ya ukweli unaovuruga ndoa/mahusiano mengi ambao walio wengi hawapendi kuukubali .....
 
Nakuelimisha hasa wewe. Si unaona ninavyo kuthamini
Unanielimisha mimi? Umesoma jina langu kwanza?
Mimi ni Mwali, nimealikwa na aunty AshaDii!
haya mapenzi unayo sema hapa ni ya vitabu tu
Real life mapenzi is full of grey shades you know.
 
Last edited by a moderator:
Unanielimisha mimi? Umesoma jina langu kwanza?
Mimi ni Mwali, nimealikwa na aunty AshaDii!
haya mapenzi unayo sema hapa ni ya vitabu tu
Real life mapenzi is full of grey shades you know.

Ha ha ha! Mbavu zangu. Eti Mwali
Wewe Kugwi na tena kugwi mwenye uzoefu wa kutosha.
Eti mapenzi ya vitabu, tatizo wewe ujawai tu.
 
Ha ha ha! Mbavu zangu. Eti Mwali
Wewe Kugwi na tena kugwi mwenye uzoefu wa kutosha.
Eti mapenzi ya vitabu, tatizo wewe ujawai tu.
Sometimes hua unani-impress sana kwa uwezo wako
wakuongea pumba kwa confidence, bila hata kuyumba
Hapo unasema nina uzoefu wa kutosha
kisha unasema mimi sijawahi. :confused2::noidea:
Read your post before you hit the send button!
 
Tatizo lako unadandia treni kwa mbele.
Nilipo andika ujawai, umeelewa nini?
 
Tatizo lako unadandia treni kwa mbele.
Nilipo andika ujawai, umeelewa nini?
wewe ulimaanisha nini? ndio uandishi gani huo?
Kama unataka kusema kitu andika kikamilifu!
Unapoandika in a way that leaves 1000 interpretations
maana yake hata wewe mwenyewe hujui unacho maanisha!
"whatever is well thought of is clearly said...
and the words to say it flow with ease." Nicolas Boileau
 
lakini tafsiri ya neno "ujawahi" si iko wazi? inahitaji mjadala hiyo tena
ndio zake huyo! hua anaropoka kuandika,
halafu anajitafutisha tafsiri kuficha udhaifu
 
It takes a long time to really get to know a person. watu wengi tunakuwa mislead by what we see in the beginning inakuja kutucost baadae after the what u expect na wot u get is different.
When a relationship is new, people tend to be on their best behavior. hivo hatutakiwi ku focus only on the positive side,we should try kujua weakness,limitation na bad habits!!!!!!!!!!!!

A person may be quite different after the relationship is established au baada ya ndoa
You need to see the person clearly, the good and the bad ili ikitokea uwe tayar aware!!!!!!
a wonderful comment mumie Heaven on earth, ndio maana tunamuhitaji sana Mungu katika hili eneo la maandalizi ya ndoa na ndoa yenyewe
 
It takes a long time to really get to know a person. watu wengi tunakuwa mislead by what we see in the beginning inakuja kutucost baadae after the what u expect na wot u get is different.
When a relationship is new, people tend to be on their best behavior. hivo hatutakiwi ku focus only on the positive side,we should try kujua weakness,limitation na bad habits!!!!!!!!!!!!

A person may be quite different after the relationship is established au baada ya ndoa
You need to see the person clearly, the good and the bad ili ikitokea uwe tayar aware!!!!!!
BIla kusahau kua binadam tunabadilika
hata mimi wa leo sio mimi wa kesho.
#BuildResiliance
 
wewe ulimaanisha nini? ndio uandishi gani huo?
Kama unataka kusema kitu andika kikamilifu!
Unapoandika in a way that leaves 1000 interpretations
maana yake hata wewe mwenyewe hujui unacho maanisha!
"whatever is well thought of is clearly said...
and the words to say it flow with ease." Nicolas Boileau

Iwe fundisho kwako Mwali, siyo unajibu kitu ambacho ujakielewa. Ulipaswa uulize kwanza. Sijawahi nini?
Namashaka sana na wewe, hasa kabila lako
 
lakini tafsiri ya neno "ujawahi" si iko wazi? inahitaji mjadala hiyo tena

Mokoyo umempa Like Mwali wakati amechemsha mbaya. Neno ujawahi linaweza kuwa
Ujawahi
Kupendwa,
Kupenda
na kadhalika
 
Iwe fundisho kwako Mwali, siyo unajibu kitu ambacho ujakielewa. Ulipaswa uulize kwanza. Sijawahi nini?
Namashaka sana na wewe, hasa kabila lako
Siwezi kuuliza kila kitu wakati context ipo wazi kabisa
Ikiwa unataka kuleta wazo nje ya mada tunayo jadili
it is up to you kusema kua neno fulani linamaanisha nini
otherwise nitalisoma in the light of the discussion at stake
Inasikitisha SANA kua unaweza kuongea na member wa JF
hunijui, sikujui, na uka-extend speculations to an entire tribe
piece of advice: Stay away from speculation, stay away from generality
 
Back
Top Bottom