Mapenzi,ndoa,roho,majini na binadamu

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,985
1,284
1464436822589.jpg

Ndoa nyingi huvunjika, na wapenzi wengi huachana kabla hata hawajafunga ndoa. Kabla ya ndoa kuvunjika na wapenzi kuachana hutokea visa vingi vya usaliti, ukigeugeu na chuki.

Mapenzi nini? Mahala pake hasa ni wapi? Asili yake wapi?Wakati gani usaliti hutokea? Wakati gani mtu anakuwa kigeugeu? Nini hasa chanzo cha chuki kwa wapenzi?

Hakuna maana moja ya mapenzi, ila vyovyote iwavyo mapenzi ni ile hali ya kuvumilia na kukubali mapungufu, udhaifu na karaha za mtu yoyote au hali yeyote au kitu chochote.

Mapungufu, udhaifu na karaha zinapokuwa za kiwango kikubwa na bado ile hali ya uvumilivu na kukubali ikaendelea kuwepo,basi hapo ujue kuwa kiwango cha mapenzi kiko juu sana, na kinyume chake ni kweli. Ukiona mtu yuko na mapungufu na mbaya zaidi ni kero kwako lakini bado wampenda basi ujue kuwa uko na mapenzina huyo mtu.

Mapenzi mahala pake ni moyoni; ambapo si lile pande la nyama lenye vyumba na mishipa ya kutoa na kuingiza damu, bali ni ile roho ambayo ndio asili ya nguvu zote zinazopatikana ndani ya mwili wa mwanadamu. Mwili wa mwanadamu tunaweza kufananisha na kompyuta.

Kopyuta imeundwa na mifumo miwili yenye kutegemeana ambavyo ni hardware na software. Vile vitu tunavyoweza kuvishika na kuviona ndio hardware na vile ambavyo hatuwezi kuviona wala kuvishika ni software. Software ndio huilazimisha hardware nini ifanye, na hardaware hupokea command toka kwa software.

Kwa upande wa mwanadamu kuna roho na mwili. Roho ndio huamuru kitu cha kufanya na katu mwili hauwezi kuiamuru roho kitu cha kufanya. Roho ni kama OS[Operating System] kwa kompyuta.

Kwa mujibu wa mapokeo ya dini za kikristo na kiislamu, mwili wa mwanadamu umeumbwa kutokana udongo, kisha mungu akupulizia pumzi yake kwenye hilo dongo hata likawa mwanadamu mwenye uhai.

Kama nilivyosema awali kuwa roho ni kama OS, na ndani ya OS huweza kuongezwa programu mbalimbali kulingana na uhitaji wa mtumiaji wa kompyuta, pia kwa mwanadamu pia huwa kuna viprogramu vidogodogo vinavyopatikana ndani ya ROHO.

Viproglamu hivyo vidogo vidogo ni kama vile vya kucheka,kununa, kuchukia, kutamani, kupenda, nk, Kila ROHO si lazima iwe na viprogramu hivi vyote, bali zingine huwa na hizi na hukosa zile na zingine hupata zile na hukosa hizi.

Kikubwa cha kufahamu ni kuwa mwanadamu hawezi kucheka kama hana hicho kiprogramu cha kumuwezesha kucheka, kama vile huwezi kuchezesha video kwenye kompyuta yako kama hauna programu ya kukuwezesha kuchezesha video. Watu wengine hawajui kununa na wengine hawajui kucheka pia, hiyo ni kwasababu hakuna kitu hicho cha kununa au kucheka kwenye roho zao. Upendo na chuki ni moja kati ya viprogramu vilivyopo kwenye roho.

SOUL MATE? Class mate humaanisha ni mtu ambaye umesoma naye darasa moja, naam, mlikutana huko darasani. Nini maana ya SOUL MATE? Hivi roho hukutana? Kwa mujibu wa dini ya kiislamu M/Mungu alianza kuziumba roho za viumbe vyote kabla hata ya kuumbwa ulimwengu na ziliishi miaka mingi kabla hata hazijatiwa au kupuliziwa kwenye miili ya viumbe hivyo. Hivyo basi huenda hizo roho zilikutana huko kwa mara ya kwanza.

Katika filamu ya kihindi inayoitwa Dil To Pagal Hai mtunzi ametueleza kuwa roho zimeumbwa katika jozi, yaani mbili mbli huku zikiwa zimenatana. Wakati wa kutiwa kwenye miili ya viumbe zikatenganishwa, moja ikatiwa kwa mwanaume na nyingine ikatiwa kwa mwanamke. Hizi roho mbili lazima zikutane, na kukutana kwenyewe ni kwa watu waliobeba roho hizo kuoana, na ndoa iliyofungwa na watu wenye hizi roho mbili[soulmate] katu hawawezi kuachana.

Usaliti? Kigeugeu? Mara baada ya M/mungu kupulizia pumzi yake kwenye mwili wa mwanadamu, baadaye na hii mara baada ya kutokea uasi mbinguni zikaingia pumzi zingine ngeni kwenye miili ya wanadamu. Pumzi hizi ni majini, au mashetani au mapepo. Hizi pumzi hufanya kazi kama roho ndani ya mwili. Nilisema huko juu kuwa roho huamuru mwili cha kufanya, hivyo na haya majini pia huamuru mwili cha kufanya.

Mkumbuke Hawa na Adamu hawakuwahi kufikiria japo kuusogelea ule mti wa kati, lakini baada ya pumzi mpya kumuingia hawa, si kwamba waliusogolea tu, lakini pia wakala na lile tunda. Roho ya mtu iliumbwa kwa mfano wa Mungu, na kiasilika haiwezi kutenda dhambi au kuacha kumtii Mungu, ila roho ngeni zilizo muingia ndio humfanya atende dhambi, ndio maana twaambiwa kuna pepo la uzinifu, uongo, wizi, na kubwa zaidi roho zetu halaumiwi kwa kutenda dhambi bali zinalaumiwa kwa kushindwa vita na shetani.

Kwakuwa ndani ya mwili tayari kuna roho, na kwakuwa hizi roho ngeni[majini] nazo huamrisha mwili, hivyo basi huwa panatokea mashindano mengi ya kiroho ndani ya mwili wa mwanadamu. Vita???

Mwili siku zote hutii ile roho iliyoshinda haijalishi hiyo roho ni ngeni au ile aloumbiwa mwanadamu. Mfano mwanadamu waweza kutoka kuoga kisha ukajikuta uko katika mtihani wa kuchagua nguo ya kuvaa, wakati mwingine waweza kuvaa nguo kabisa kisha ukajikuta waivua na kuivaa nyingine, ila hali ya kuchagua nivae hii au ile ni matokeo ya mashindano ya kiroho ndani ya mwili, Vita?

Hata katika kuchagua mpenzi pia hutokea mashindano ya kiroho ndani ya mwili. Unapochagua mpenzi na kuamua kuishi naye jua kuwa kuna roho imekushinikiza kufanya hivyo na si vinginevyo. Kwakuwa watu wote tuko na roho ngeni nyingi kwenye miili yetu, kwakuwa hizi roho hutofautiana nguvu kulinganana nyakati, na kwakuwa roho yenye nguvu kwenye wakati fulani ndio hutawala kipindi hicho, hivyo basi kiwango cha “mapenzi” ya mwanadamu kwa mwenza wake hubadilika kadiri roho zinazotawala mwili wa mwanadamu huyo zinavyobadilika;hapa ndipo usaliti na kigeugeu vinapozaliwa.

Wakati wampenda mwajuma elewa kuna kiprogramu[roho] ndani ya mwili wako kimekufanya umpende huyo mwajuma, hiyo roho ikizidiwa nguvu hata ikaingia roho ya kumpenda Asha lazima utamuacha mwajuma na kuanza kumpenda Asha. Hizi roho ngeni ndio hupelekea “soulmate” wakati mwingine zisikutane. Kama ile roho ya inayompenda Asha ikiendelea kutawala kwa muda mrefu hata mauti, basi huyo mtu atendelea kumpenda Asha hadi kifo chake.

Cha kuzingatia, ile roho inayomfanya John ampende Asha haiwezi kufaulu hadi Asha awe na roho inayompenda John. Ikiwa roho hizi ni "SOULMATE" basi mapenzi ya Asha na John hudumu daima, kama hizi roho si "soulmate" na hivyo mapenzi yao ni matokeo ya roho ngeni[majini] zilizopendana, kwa hivyo mapenzi hayo yatachuja na kupotea kabisa mara baada ya roho hizo kutolewa kwenye utawala na roho zingine.

Roho ngeni namaanisha majini au mapepo. Kila mwanadamu ana majini wengi na kila jini kuna mambo anapenda na kuna mambo anachukia, na kila jina kuna siku yake, mwaka wake na hata muongo wake wa kutawala. Pia kila jini ana nguvu zake za kikawaida alizoumbwa nazo na kuna majini wengine wana nguvu za ziada(uchawi)

MWISHO:
katika yote hayo juu, naomba rejea kitendo cha Kefa kumkana Yesu mara tatu, rejea usaliti wa Yuda Iskariote kwa Yesu, rejea vita vya maswahaba baada kifo cha Mtume Muhammad(s.a.w), pia rejea maisha yako kila siku. Utabaini bila jelezi kuwa usaliti, kigeugeu, mapenzi, urafiki, nk vinatawaliwa na majini na roho, na kwasababu hiyo miili yetu haina hiyari hata kidogo.

Siku nyingine nitafafanua uhusiano kati ya majina yetu na mahusiano mapenzi na ndoa. Kwanini watu wengine huchezesha herufi za majina yao au hubadili majina kabisa kwa lengo la kuimarisha ndoa na mahusiano.

PENZI JINI HATARI.
1
Penzi ni jini hatari, wa kutesa na kuua,
Huzibeba zote shari, za kiangazi na mvua,
Nina kuomba Qahari, miye asije niua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
2
Penzi mganga mzuri, huponya wanougua,
Hukusanya nyingi heri, za mwezi hata za jua,
Kwa idhini Ya Jabari, aponye changu kifua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
3
Mapenzi istiimari, hakika nimetambua
Baridi naona hari, meli mwenzenu mashua,
Asali kwangu shubiri, ninajuta kuyajua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
4
Mapenzi ni zingifuri, kwa mja anayejua,
Narauka Alfajiri, naswali naomba dua,
Yarabi penzi la siri, lisije kuniumbua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
5
Penzi si kama johari, huwezi kulinunua,
Si mchanga wa bahari, bure ukalichukua,
Thamaniye si mahari, mkaja hata jazua.
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
6
Penzi halina jabari, si chuma la kuinua,
Uwe bondia hodari, pia laweza sumbua,
Huba zataka sukari, moyo upate kutua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
7
Mapenzi jua qadari, uwaze na kuwazua
Alo lipanga Ghafuri, hakuna wa kupangua,
Hivyo hatuna hiyari, hata kama twaamua
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.
8
Mapenzi si kibatari, ni mshumaa tambua,
Nyonda apate fahari, mwenyewe unaungua,
Yengekuwa samsuri, wallahi ningeyavua,
Mahaba yanizuzua, mtima wata ghururi.

Dotto Rangimoto Chamchua(Njano5)
Whatspp/call 0622845394
 
So unaweza kuoa ambae sio soulmate?!ina maana km sio soulmate itakuwa mmeoana bila kupendana
Labda kwa tamaa tu ya vitu ambavyo ikitokea siku vikapungua au kuondoka basi na mapenzi yanapeperuka.
Mfano ulimuoa sbb mweupe siku akiungua moto basi mapenzi yameisha.
Labda umekubali kuolewa sbb mwanaume ana pesa siku zikiisha unamkimbia.
Au umependa mzigo huko nyuma ukaamua kuoa siku akikonda unamfukuza!
Ila mapenzi ya roho yaani soulmate hayazingatii mtizamo wa nje wa mtu bali ni mvutano wa kiroho za pande zote mbili.
Ni mara chache sana mapenzi ya kiroho bila kuwa na muonekano flani wa nje yaani appearance au attracted materials.
hapo nimeelewa kwamba unaweza kupenda mtu ambae ndio soulmate wako ila yeye kumbe ana soulmate mwingine.
wrong time at the wrong place
 
So unaweza kuoa ambae sio soulmate?!ina maana km sio soulmate itakuwa mmeoana bila kupendana
Labda kwa tamaa tu ya vitu ambavyo ikitokea siku vikapungua au kuondoka basi na mapenzi yanapeperuka.
Mfano ulimuoa sbb mweupe siku akiungua moto basi mapenzi yameisha.
Labda umekubali kuolewa sbb mwanaume ana pesa siku zikiisha unamkimbia.
Au umependa mzigo huko nyuma ukaamua kuoa siku akikonda unamfukuza!
Ila mapenzi ya roho yaani soulmate hayazingatii mtizamo wa nje wa mtu bali ni mvutano wa kiroho za pande zote mbili.
Ni mara chache sana mapenzi ya kiroho bila kuwa na muonekano flani wa nje yaani appearance au attracted materials.
hapo nimeelewa kwamba unaweza kupenda mtu ambae ndio soulmate wako ila yeye kumbe ana soulmate mwingine.
wrong time at the wrong place
kama ni soulmate hawez kupenda mwingine zaid yako labda tu,,, awe na jini mwenye nguvu,, jini mwenye uwezo wa kuamrisha mwili wake ufanye kitu tafaut na roho inavyotaka,,,,kadiri jini atakavyo tawala na kadiri huyo mtu atakuwa mbali na soulmate wake.

Ndio maana ukienda kwa mganga anadili na huyo jini,,, aidha kwa kumtoa au kwa kukupa jini mwenye nguvu zaid ya huyo ambaye ataenda sawa na matarajio yako.
 
Back
Top Bottom