Mapenzi na uungwana..................wanaume tuonyeshe mfano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi na uungwana..................wanaume tuonyeshe mfano.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by The Boss, Apr 21, 2010.

 1. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  Mimi nafikiri wakati mwingine ni bora
  kila mtu kabla hujaanza kuingia kwenye mapenzi
  na mtu ni bora kujua kwamba,
  masuala ya kugombana na kupata maudhi kwenye mapenzi
  ni mambo ya kutegemea na kutarajia......kilicho cha maana
  ni wewe mwenyewe kujifunza namna ya ku deal na ugomvi
  na maudhi yanayokuja na mapenzi.....it is part of any relationship.....

  Sasa basi cha kushangaza ni kuwa wapo watu wakiwa na ugomvi
  kidogo na wapenzi wao ni aibu tupu......
  Yaaani aibu mpaka kwa majirani au wapita njia.........
  Wengine ugomvi mpaka watu wanajaa kuwasikiliza na ukikuta
  yanayozungumzwa ni aibu ,aibu aibu........

  Pamoja na yote mimi naamini mwanaume ukiwa na msimamo na unajua
  kum handle mwenzio tangu mwanzo mambo mengi yasio faa yanaweza ku epukwa.....
  Hivi ni lazima watu wazima mfokeane mbele ya watoto????
  Au ugomvi mpaka majirani wanakuja kuwaamua??????
  Utakuta mtu anajaribu kumtukana mpenzi wake mbele ya watu as if
  na yeye hajitukani kwa ujinga wake.....

  Mimi huwa naona watu kama mmechokana ni bora kuachana kwa heri bila ugomvi
  na sio unakuta watu wazima,shule wameenda,pesa wanayo lakini
  ikifika jioni ni ugomvi,ugomvi mpaka wapita njia wanasimama kufaidi sinema ya bure...

  Ni kweli wanawake wana maudhi sana.but mwanaume ukiwa mstaarabu
  matatizo mengine yanaepukika........
  Tusisahau nobody is perfect...........................................
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  aibu zingine sio za lazima.................
   
 3. P

  PELE JF-Expert Member

  #3
  Apr 21, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 229
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kugombana ni part and parcel ya wapendanao lakini kugombana mbele ya kadamnasi ni aibu tupu hata kama hamtukanani matusi ya nguoni. Hata siku moja sitapoteza muda wangu wa kujibizana na nimpendaye kama hatuwezi kuongea kiustaarabu ili kumaliza matatizo yaliyokuwepo basi nitaingia mitini maana mtu anayebwata kwa sauti kubwa mpaka utui wa mdomo unamtoka na hakupi nafasi hata ya kutia neno mimi siwezi kuelewana naye ni bora kumuacha abwate mwenyewe na akishatulia tutaongea kiustaarabu. Je, na wale Wanaume wanaopiga wanawake zao kwa sababu ambazo hata haziingii akilini huwa wanafikiria nini hasa hadi kuwapa mikong'oto ya kutisha Wapenzi wao?
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  kumpiga mpenzi wako ni kujidhalilisha na kumdhalilisha mwenzio...........
   
 5. vkeisy2006

  vkeisy2006 JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 230
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 45
  ni kweli mara nyingi wanawake wanapenda sana kuongea....lkn ni vizuri vitu vikawa vinajadiliwa taratibu kwa masikilizano watu waelewane lakini uatakuta mwanamke hapewi nafasi ya kuongea.....mbabe anataka atakachoongea yeye ndo kiwe hicho hicho....hata kam kosa lake hv nanai atakubali hapo.....lazima marumbano yatokee lakini hata kama mtu unahasira vip jaribu kucontrol hasira zako lakini sio kutukanana mbele ya kadamnasi....na kupigana ni aibu tupu.....au unapomtukana mwenzako matusi ya nguoni mbele za wtu unajidhalilish awewe mwenyewe na huyo unaemtukana......thanx sana kwa alie anzisha hii topic i wish i can say more....lakin i can't.....
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  why not?
  Ongea vyote.........
   
 7. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Duh lakini wadada ndio mara nyingi hawana simile, bomba likipasuka wanatoa mpaka mambo ya sirini
   
 8. P

  Preacher JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2010
  Joined: Aug 25, 2008
  Messages: 328
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Dawa ya moto ni maji - mwenzako akipanda juu sana kwa maneno (kama moto) inabidi the other partner ashuke na kunyamaza kimya (kama maji) - hapo mtu kuongea mwenyewe mwisho ataona aibu na kunyamaza -hatimaye hasira zikimwisha muda wa maongezi utakuwepo.

  Ndio maana Bible inasema katika kitabu cha Mithali "HASIRA HUKAA KIFUANI MWA MPUMBAVU"
  na Msemo wa Kiingereza ambao ni common unasema "NEVER URGE WITH A FOOL, PEOPLE MIGHT NOT NOTICE THE DIFFERENCE"
   
 9. K

  KABAZI JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2010
  Joined: Apr 19, 2010
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33

  Ni kweli kabisa hapa wanaume ndio tunaotakiwa kuwa wastaarabu zaidi. Kama ambavyo amani isivyo nunuliwa ni kwa struggle ndivyo yalivyo mapenzi. Wapenzi wanapozidi kukosoana na kusameheana ndivyo penzi linavyozidi kustawi.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Kuna mwanamke mmoja alikuta Condom kwenywe mfuko wa suruali ya mmewe badala ya kumuulizia huko huko chumbani akabeba Condoms zake na kwenda nje analia baba fulani ndo nini hiki yaani unataka kuniua huku kaning'iniza hiyo zana majirani kuanza kujaa tele ..mme alichofanya alimvutia ndani na kuanza kumpa kipigo cha mbwa mwizi.. bila ya kutoa maelezo ya Condoms
  mie nilicheka sana na kujiuliza Condoms kakuta ndani akiwa chumbani nini kilimtuma kutoka nje na kuanza kupiga mayowe?
   
 11. Loner

  Loner JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2010
  Joined: Mar 12, 2010
  Messages: 212
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ustarabu ni kitu kigumu sana na inategemea mtu hasira zako ziko je... Kama unalipuka ni ngumu kuwa muangalifu wa kelele na uko wapi... Laiki kujifunza PATIENCE is very important mtaishia wote kuonekana wajinga na wenye tabia za kitoto mbele ya watu...
   
 12. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Akina Mama jamani, hata mkiwa chumbani sometimes ukipigiwa simu tu ya ofisini na mfanyakazi mwenzio wa ofisi akiwa wa kike ni nongwa oooh kwa nini akupigie wewe tu? km ni boss wako utafanyeje? basi hapo kelele tuu mwanamke wako huyooo, mara oooh mnajuana kuweni na simile basi tusikilizeni kwanza
   
 13. Askofu

  Askofu JF-Expert Member

  #13
  Apr 22, 2010
  Joined: Feb 14, 2009
  Messages: 1,668
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 133
  Mimi sidhani kama mafahali wawili wanaweza kukaa zizi moja... na siku zote mwanamke mwenye busara hawezi kujibizana na mwanaume (au mtu yeyote) mbele ya kadamnasi. Kama alivyosema Preacher hapo juu, hapa busara inahitajika zaidi.
   
 14. p

  prosperity93 Member

  #14
  Apr 22, 2010
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  bibie umesema kweli.....wanawake kwa ngonjera hawajambo..ila kwa vile tuu wangu nampenda sana ndo maana naweza kuvumilia maneno ila hatubigani wala kutukanana ni majibishano yakawaida....
  hivi hadi leo kuna wanandoa tena wasomi wanaweza kweli kutoa matusi au kutukana dhidi ya wapenzi wao mbele ya kadamnasi....mimi sijaona hayo mambo muda mrefu sasa....
  hata mbele ya watoto wangu naogopa sana kumgombeza mama yao...kama baba lazima nionyeshe mfano mzuri ili watoto waweze kujifunza kutoka kwetu
  vkeisy2006...sema yote uliyonayo moyoni...
   
 15. m

  masho Member

  #15
  Apr 23, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  @the boss, kuna baadhi ya makabila mwanamke asipopigwa na mpenzi wake atalalamika kuwa mpenzi wake ampendi na isitoshe atadai talaka, ila kwa mimi hiyo kitu siipend na ninamwomba Mungu aninusuru na hilo kabisa
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Apr 24, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280

  wanawake wengine vipigo hutafuta wenyewe...
   
 17. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #17
  Apr 24, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  But mgogoro ni muhimu kwenye mahusiano coz inahusisha pande mbili zilizo na maslahi yanayogongana .Cha msingi ni heshima,kama watu wanaheshimiana basi pia njia yao ya kutatua matatizo itakuwa ya kulindiana hashima
   
 18. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #18
  Apr 24, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  huyo mwanamke ina maana yeye hapigiwi simu na mwanaume yeyote isipokuwa mpenziwe au ndugu yake?
   
 19. m

  masho Member

  #19
  Apr 24, 2010
  Joined: Apr 9, 2010
  Messages: 56
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  teh teh teh duh!!!! huyo mwanamke kweli hazimtoshi yaani kapatwa na atizo akiwa ndani akaenda kulilia nje??????????????? hakuwa na machungu yoyote bali aliamua kumdhalilisha tuu mumewe,
   
 20. Theodora

  Theodora JF-Expert Member

  #20
  Apr 24, 2010
  Joined: Dec 20, 2009
  Messages: 522
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  My secret weapon has always been silence. Silence is golden and divine. Lkn jamani kuna wale wanaitwa drama queens and kings na kugombana hadharani ni kawaida, na wala hawana cha aibu. Ustarabu comes from within not without, and you cannot teach somebody.
   
Loading...