Haya haya hayaa! Kama kawa kama dawa ni wakati mwingine wa kutiririkaa! Aha ni mapenzi na ujinga... Yes ni mapenzi na ujinga kwa sababu huwezi ku-enjoy penzi la kweli kama wewe sio mjinga; na huwezi kudumu kwenye relationship kama wewe sio mjinga; mapenzi na ujinga ni marafiki wawili wanaopendana sana, huwezi kuwatenganisha. Wakati mwingine mpenzi wako anakukosea, lakini unaamua tu kusamehe, ingawa hukupenda kusamehe hilo kosa, lakini ujinga umefanya kazi yake na penzi linaendelea. So kubali kuwa mjinga hata usipoletewa zawadi na mpenzi wako, usikasirike endelea tu kuwa mjinga, bila kuwa mjinga mapenzi hayaendi. Hope wajinga wenzangu mmenielewa, tuendelee hivi hivi kuwa wajinga, tusipokuwa wajinga kila siku tutakuwa single; na kuwa single yahitaji moyo mgumu kama bati la South Africa.