Mapenzi na maisha haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi na maisha haya

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by BRO LEE, Mar 27, 2012.

 1. BRO LEE

  BRO LEE JF-Expert Member

  #1
  Mar 27, 2012
  Joined: Dec 25, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  ===Naingia ofisi moja ya serikali nasoma ubao wa matangazo naona matangazo sita ni ya watumishi wanaoomba watu wa kubadilishana nao vituo vya kazi, wa2 hao c kwamba wanataka kurudi kwao bali wanataka kuwa na familia zao (mke/mme)===

  Naposoma matangazo haya nakumbuka wakati nilipooa baada ya harusi kila mmoja analazimika kurudi kituo chake cha kazi kuonana majaliwa, aidha ujiibe au usubiri likizo lini mara moja kwa mwaka!

  Naamini wapo wengi wanaoteseka na mfumo huu wa maisha,majukumu ya kusaka uchumi yameingia kati ya ustawi na afya za ndoa zetu.Nakutana na dada anahangaikia uhamisho ni mwaka wa4 anapigwa danadana atafute mbadala chozi linamdondoka ananiambia anataka kuacha kazi, namsihi asiache kazi kwanza kabla yajapata kazi nyingiene huko anakotaka kuhamia, kwa mwonekano ni dhahiri amechoshwa na haya mazingira.

  Kwa hakika si kazi rahisi hata kidogo kwa ndoa changa(chini ya miaka 5) kustahimili haya mazingira, watu wanapooana wanakuwa na matarajio mengi sana, kuwa na kampani, mshauri, mfariji n.k.

  Kutokana na umbali kwa sasa simu ndo zimechukua dhamana ya mapenzi yetu(zinatuunganisha), lakini wakati mwingine zinasababisha kukwazana na hata kugombana.mf. kuna mtandao mmoja unapiga cm unasikilizishwa mziki ukiamini yule uliyempigia simu inaiita..kumbe laah,utapiga mara nyingi mpaka unapata hasira huyu kaweka wapi simu.Ukimpata baadaye unaanza na lawama kumbe mtandao haukuwa mzuri tayari mmeshakwazana.Mtandao mwingine utaambiwa number busy na network busy, mawazo kila wakati yuko busy halafu wala hanitafuti kumbe mtandao.

  Natizama maisha ya vijana wengi waliooa wananinginiza ndoa vidoleni(pete) lakini mwisho wa cku wakirudi nyumbani hawana tofauti na mabachela, upweke unatawala wengine wanaanguka na kuanza mahusiano mengine,thamani ya ndoa iko wapi?

  Napenda kupata mawazo yako km ww ni mwasirika wa hali hii na namna unavyokabiliana nayo hasa kwa kuzingatia cku hizi mahusiano baina ya wana ndoa(wanaume) na mabinti yamekuwa yanaongezeka kiasi kwamba wengine wala hawajifichi inakuwa ni jambo linaloeleweka kwamba fulani anatoka na fulani.
   
 2. HorsePower

  HorsePower JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2012
  Joined: Aug 22, 2008
  Messages: 3,617
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  Ndugu umenena vyema. Uyasemayo ni kweli tupu. Ni kweli mahusiano na uvunjifu wa mahusiano na uaminifu kwa wanandoa wakati mwingine husababishwa na umbali baina ya wanandoa.
  Ni ngumu kumshauri mtu kuacha kazi kwa hali mbaya ya uchumi tulionayo watanzania. Jambo la kufanya, labda ni kujaribu kuwa waaminifu na kuwa wavumilivu, hebu tujifunze kuiweza miili yetu na kuepuka tamaa, labda pia tuongeze ukaribu na Mungu wetu pia, hofu ya Mungu ikitushika vizuri itasaidia uaminifu kuongezeka.
   
Loading...