Mapenzi na maajabu yake

Sic March

JF-Expert Member
Mar 2, 2019
690
895
WanaJF,

Siyo siri leo nimestaajabu mapya kabisa katika mapenzi. Ilikuwa hivi:

Kuna 'pisi' moja niliitongoza ikanambia itanijibu nivumilie. Sasa kuna siku aliniambia hana pesa ya msosi, mimi nikakaza nikajisemea siwezi kubeba mzigo usionihusum, nikamkwepa kijanja hapo.

Movie inaanza, jana usiku namwambia nipe jibu basi, akaanza maneno meng oohh mimi nina mtu ananipenda ambaye yeye ananijali, ambae haruhusu mimi nishinde njaa, nampenda sana; lakini wewe hunipendi ndiyo maana uliniacha nishinde njaa.

Yaanisiyo siri nimecheka sana na hawa viumbe wa leo.

Sasa nikajiuliza mimi nimekosea wap hapo mpaka sasa, sina jibu aisee. Wana mnipe somo nilikosea wapi.
 
Unatizama na pakutoa, kuna mahali unakua unajua tu hapa, natupa pesa kwa shimo la choo.
Ulikosea kuto mpatia pesa ya chakula , ulitakiwa mtumia ata ulicho nacho ungeona majibu ya swali lako .siku nyingine usiwe na mkono mfupi saidia mtu tuu then subiri malipo
 
Jibu mbona rahisi we bwege. Ulimtokea akakuambia subiri atakupa jibu. Jibu likaanza kutolewa kwa vipimo,je unaweza kum-care mahala popote kwa chochote?. Akakujaribu tu nina njaa ili aone kama kweli we ni mwanaume. Wewe mwenyewe ukakimbia tena. Unasema ukamkwepa. Sasa hapo unajiuliza umekosea wapi? Wakati ni rahisi tu,we msosi wa buku mbili tu,ukakimbia?.
 
we ungemwambia tu unataka kumgonga alaf kila mtu apite na zake lakini wewe ulienda kama unataka awe mpenzi hapo kunatofauti, mpenz anakuwa amezaliwa ili uje kumlea.
 
Hizo comments za mwanzo sipingi lakini inategemea huyo binti kakupendea nini. Kuna uwezekano anataka uwe mwezeshaji wake hivo akakutupia mtihani huo kwanza. Hili sio tatizo kwangu kwani akipenda kula akubali kuliwa. Shida ilinitokea mmoja huyo anasali kwa Gwajima 3times @week nikataka kumeet nae eti hana viatu,suruali zao zile na hajasuka. Hapo visenti vya kula nilikuwa nampa, nikaamua tu kumwambia mwenyewe nina hamu sana hivo njoo tuexchange. Akaishia kusema mimi siko hivo, nilijua unaniita tupange maendeleo kumbe unataka tufanye na ndo kwanza hatujazoeana. Kilichofata block, sijawahi kumpenda binti kilaza hata mara moja
 
Yeah huyu jamaa alishindwa kujua kama lile ombi ni kipimo,,,,,,,,,,,,
Basi sio mwanaume I see. Kipimo kidogo tu hicho. Tena huyo msichana ana akili kumzidi yeye. Kipimo alichompimia ni size yake,kuhusu chakula
 
SK2016, Muondoeni kwenye chama cha ubaharia huyu bwege. Hata kuleta tu hii hoja dhaifu hii mbele ya meza,inabidi apewe za uso
 
Muondoeni kwenye chama cha ubaharia huyu bwege. Hata kuleta tu hii hoja dhaifu hii mbele ya meza,inabidi apewe za uso
Kweli kabisa.

Alafu anakimbilia kufungua uzi dhaifu kabisa mbele ya Mabaharia!
Dah! Wanaume tunapungua. Hiyo ilikuwa anajiongeza, anaanguka then refa anapitia VAR anafunika Penalty, unafunga bila kipa gorini!

Chukua Pepsi big hapo kwanza tupoze hii thread!
 
Basi sio mwanaume I see. Kipimo kidogo tu hicho. Tena huyo msichana ana akili kumzidi yeye. Kipimo alichompimia ni size yake,kuhusu chakula
Hahahahhahahahaha Kuna mtu nilimpima aniazime buku ishirini, tena nlipanga akinipa tu nakaa masaa kadhaa namrudishia then nimwambie nimeshasolve tatizo, khaaa akasema ooh mimi sichuniki, sijui bora nisioe blah, blah nyingiii..... Nikamwambia basi wewe hata siku nikiwa na shida hutoweza Kutoa msaada bakia kwako
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom