Mapenzi na kukopeshana!

ukimkopesha mpenzi wako au ndugu yako jiweke tayari kwa lolote litakalotokea ikiwa ni kutolipwa, kuvunjika kwa mahusiano na mafarakano katika undugu.

Ningekushauri usimkopeshe mpenzi au ndugu yako pesa. Ikiwezekana mpe tu.
 
dah mimi huwa nina aibu ya kudai madeni,
kama vipi naweza kumpa tu kama kumsaidia.
 
Hakuna kukopeshana wakati mnashea mapenzi,ni ngumu sana kumdai mwenza wako baada ya kuwa umempa pesa na wapenzi wengi huamua kutoa tu kama zawadi.
Ila kama ukichoka kuwa nae si vibaya kudai chako.
 
Si hela tu wanaweza kopeshana mambo mengi tu!
 
ukimkopesha mpenzi wako au ndugu yako jiweke tayari kwa lolote litakalotokea ikiwa ni kutolipwa, kuvunjika kwa mahusiano na mafarakano katika undugu.

Ningekushauri usimkopeshe mpenzi au ndugu yako pesa. Ikiwezekana mpe tu.
kabisa dear yaani kuna watu ni balaa
 
Ingekuwa vizuri kukopeshana, kuliko akakope kwa watu wengine ni bora kukopa kwa mtu wa karibu. Mimi huwa ninamkopa mama na ninamrudishia; watu wa nje hata baadhi ya ndugu huwa hawaamini kama huwa napata shida (wanaona kama nawasanifu tu).

Kwa mkopaji, ni bora kulipa kama kweli umekopa ila kama huna mpango wa kulipa basi omba na sio kutumia neno (kukopa)
 
mimi siwezi kumdai mtu kabisa so naogopa sana kumkopesha mtu .ila kama ni mpenzi wangu nitamuomba hela yangu.ila akinikopesha yeye dah akinidai sijui kama ni fair,si haki kumlipa mwanaume while ni mpenzi wako bana au?

Kwanini unatumia neno 'nikope' wakati unataka kupewa bila kurudisha?
Kama humaanishi unachokisema usitegemee naye amaanishe anachokisema.
 
inategemeana, kama ankutreat kama ATM, that is just another way ya kukuchuna. ila kama mko serious, hata wanandoa wanaweza kopeshana, na wakalipana tu, si unategemea za kufanyia nini?
 
ngoja nikukope
 
Siyakubali mapenzi ya kukopa, huo ni utapeli huyo. Mwache mpenzi wako ajitolee kukusaidi kama inahitajika bila wewe kuweka bango la kukopa, maana hatoweka matumaini ya kulipwa deni.
 
Si vziuri kukopeshana hasa kama anashida/anahitaji hela kwa ajili ya jambo muhimu ambalo litawanufaisha wote! ila sheria ya hela hairuhusu kumpa mwenzio hela hivi hivi atazoea vibaya

Kwa hiyo unampa ukimwambia umemkopesha na ajue kuwa anadaiwa na asipolipa hapewi nyingine, ingawa unajua hatakulipa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…