Mapenzi matamu kweli, ila yamepelea neno YES. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapenzi matamu kweli, ila yamepelea neno YES.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Logo, Jun 8, 2011.

 1. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaman naombeni msaada wanaJf.
  Nina msichana ambaye nimempenda sana, ni muda kitambo nimekuwa nikiwasiliana naye kama rafiki yangu! Kiukweli huwa tunachat naye sana, hana kinyongo kabisa! Kuna siku nilimkosea baada ya kumtania nina mtu mwingine, kesho yake hakuwa na hamu kabisa ya kuchati na mimi, kila nilipomwambia kitu alitengua na kudai anaumwa au amechoka au anajisikia vibaya! Ukweli ulikuja kubainika kuwa nilikuwa namtania tu na haikuwa kweli. Alifurahi sana tuliendelea kuchati kama kawaida yetu!

  Muda umeenda mwishowe nikaamua kumweleza kuwa nampenda ili awe mke wangu! tulipanga siku ya kukutana na kuzungumza nae kuhusu hilo. Usiku wa kuamkia siku yenyewe aliniuliza kama nina mpenzi au nilishawahi kuwa na mpenzi, nilimwambia nilishawahi akaniuliza kwann mliachana nikamwambia alikuwa mwanafunzi so sipenbdi kumharibia masomo as why nilimuacha! Nilipomuuliza yeye kwanza alikataa kuniambia, lakini katika kumuomba aniambie aliniambia anamchumba ambaye anampenda sana na amejikommiti kiukweli kwake ila aliniambia hivi: ananipenda sana ila hana jinsi! mchumba wake hawajajitambulisha home kwao wala kulipa mahari, just uchumba wa vijana wa siku hizi! Aliponiambia hivyo niliumia sana nikaamua kupotezea, kesho yake mapema sana aliniandikia message nzuri sana iliyonifurahisha! nikaendelea kuchati nae. siku ya siku ilipowadia sikusita nilimweleza upendo wangu na kumwambia ukweli kuwa namhitaji sana awe mke wangu! Aliniandikia message baadae akasema amefurahi sana!

  Nimejaribu kila wakati kutaka kujua hatima sasa, mara nyingi anasema hana jinsi au anashindwa afanyaje au sio rahisi maneno ya kuonyesha tu kuwa anampenda sana jamaa! Amekuwa akionyesha love yake kwa action tu lakini kwa mdomo kusema YEs hata siku moja!

  1. Sasa je, huyu demu ananipenda kweli au ni mchezo tu mapenzi?
  2. Nifanyeje sasa ili nikubalike na kupewa utawala na hatimaye kumuoa?

  Natanguliza shukrani
  Logo.
   
 2. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  Kama tayari ana mtu wake wewe mwache bana. Kwanza hiyo habari ya yeye kuwa na mtu tayari ni ishara tosha kuwa hayuko kidete. Kama ambavyo anamfanyia huyo jamaa yake wa sasa, wewe ukifanikiwa kumchukua na wewe huenda ipo siku itakula kwako kwa mtindo huo huo. Sasa hebu fikiria, utataka hayo yakutokee? Mkuki kwa binadamu maumivu yake usipime.
   
 3. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Umenena kiranja wangu
   
 4. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu achana naye tu huyu! wapo wengi mno siku hizi jamani kama huamini uniPM nikuunganishie warembo wenye kujiheshimu!
   
 5. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lakini mkuu amenikaa kwa moyo sana, yaani sijui nijikazeje tu nimtupilie mbaliiiiiiiiiiiiiiiiiiiii:confused2:
   
 6. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  kiukweli ndo hivyo utakuwa na nafasi ndogo sana kwenye moyo wa uyo mdada
   
 7. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hapa nikazi kweli asante kwa ushauri wako mkuu
   
 8. HAZOLE

  HAZOLE JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 1,331
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  punguza kuchati naye bana wewe...... wewe unachatichati na wachumba za watu kwanini? kama mnajadili physics sawa ila kama biology achana naye. punguza...punguza then quit. kama anakutania, utajua kupitia kupunguza.
   
 9. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimelipenda jibu lako mkuu! so nikipunguza kama ananitania ataquit nayeye? au?
   
 10. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Jaman sisi wengine ndo tunawatafuta watu kama nyinyi wengine wanawachezea anyway!
   
 11. Futota

  Futota JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 524
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Hapana mkuu, I beg to differ from wachangiaji hapo juu.
  Unajua wanawake wanahusudisha sana kupata NDOA, hii ni hatua muhimu sana kwa ma-dame.
  Sasa wewe chakarika kwa kasi, weka dhana zako zote wazi kuwa una mpenda na unataka kufunga pingu za maisha naye.
  Na kwamba upo tayari siku yoyote kwenda kujutambulisha nyumbani kwao, huna kikwazo.
  In summary, wewe kula deep na mtoto, huyo mshikaji anaye sua sua hata pata kitu, wewe utachukua jumla, I tell U
   
 12. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  Kaka hapa ni mjini,usikubali pigana kiume,tumia cash,maneno matamu muonyeshe mapenzi pambana hadi umchukue huyo mtoto manake anvyosema hana maamuzi ina maana amewa grade we na jamaa level moja ni juhudi zako tu ndo zitakazokufanya umpate usimwache au kupunguza kasi...manake utakua umempa jamaa nafasi komaa we kidume bwana...vp ww!
   
 13. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  yes mkuu hapo umenena...jamaa anatakiwa kukomaa mm mwenyewe iliwahi kunitokea hii niliposhangaa akaolewa
   
 14. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,695
  Likes Received: 8,229
  Trophy Points: 280
  Mh! m getting mixed thoughts...samthng amiss here!
  be back soon..
  **Mmeshawahi kuonana uso kwa uso?
   
 15. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante mrembo subiri nimshughulikie kwanza wifi yako
   
 16. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu umenena sana! nimeipenda sana hii comment sasa waweza kunimegea nifanyeje kidogo angalau asituke na kuona kweli hii ngoma gari sana!
   
 17. C

  Chamkoroma Senior Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 6, 2010
  Messages: 187
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alichosema Futota ni kweli kabisaaa, asikudanganye mtu, uchumba siyo ndoa, kwahiyo kama unampenda kweli kula kubwa, jitokeze kwao, na kama alisha mpeleka jamaa basi itawekwa wazi nadhani atakukataza usiende kwao utajua basi anakupenda nusu lkn kama yuko serious atakubali na jamaa atabaki mdomo wazi inawezekana ana huyo jamaa anamwingine anajaribu kuwa thaminisha aamue yupi jaust be strong take courage have the lady on your chaest ma bro.
   
 18. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa kwanza mtoto anajiheshimu sana!
   
 19. Logo

  Logo JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 588
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asante sana mkuu ushauri bomba! Nifundishe kidogo na mauchawi ya kumfanyia ili achizike mazima
   
 20. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,498
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 160
  Hili jamaa kwa kutaka wengine waharibikiwe kimapenzi halafu lenyewe linyookewe! NN, una kiu kubwa mno ya mapenzi rafiki yangu, nadhani hujawahi kupendwa na msichana yeyote maisha yako yote, sababu ushauri wako kwa wengine, wanaume wenzako, always ukiuangalia sana, unakuwa uko inclined to the-all-negativities, kuonyesha kuwa unaona wivu wenzako kupendwa, au kuwa katika mapenzi ya dhati. Tafuta pace ya angalau kuwa unatoa ushauri positive kwa wenzio, at least mara moja kwa mwaka, siyo mbaya!
   
Loading...