Mapenzi kitu ajabu sana.......

Mapenzi kitu ajabu sana.......

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Mapenzi kitu ajabu, ni shani yake Manani
Hayahitaji sababu, sababu ilo makini
Hujimwaga bubububu, bububu maji ya pwani
Watu wakataajabu, kilichokupata nini!

Hayahitaji dhahabu, mapambo mingi mwilini
Au wingi wa adabu, adabu za kizamani
Jamani mapenzi tabu, tabu yake huioni!
Mpaka uwe karibu, karibu yake mwendani!
Mapenzi yakikusibu, yakasibu mtimani

Wageuka kuwa zubu, kwa wingi wa hamkani!
Wataraba kama dubu, dubu lisilo makani
Bila wako mahabubu, hakika umashakani.
Mapenzi kama zabibu, zabibu mbivu mtini

Hata yawe ughaibu, utayafata kwa kani
Humsemesha na bubu, mapenzi akibaini
Wala hayana ubabu, ujana wa kizamani!
Mapenzi si madhehebu, ya fikira au dini

Mapenzi si ustarabu, si haiba wala fani
Mapenzi si ukatibu, cheo hakina thamani
Mapenzi yanaghilibu, ajabu hii jamani!
Hayana utaratibu, mapenzi ni maluuni!

Mapenzi kisebusebu, na kiroho mkononi!
Mapenzi ni merikebu, isiyo nahodha ndani!
Au punda mwenye nabu, hatari iso kifani.
Mapenzi hayana jibu, mapenzi si mtihani!

Mapenzi sio kitabu, cha kusoma darasani
Mapenzi si aghalabu, kuwa sawa duniani
Imechoka yangu nibu, kalamu naweka chini.
 
Wala usizeeshe,mwenzako bado kijana
Makoja usinivishe,akanituwa lawama
Hizi kama mishemishe,nawatuliza wanosoma
Ila kwako asante,kuona ni jambo jema
 
Kipi kinachokutisha,nambie nikibaini
Tamaa wajikatisha,nawe umejita queni
Malkia wanitisha,kwa kua hujiamini
Hebu punguza presha,woga hauna thamani
 
Fikiria kipuuzi, ingekuwa vipi kama yasingekuwepo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom