Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,349
Ben ni mtoto wa mwisho katika familia ya watoto wanne, ana dada mmoja na kaka wawili. Akiwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika akisomea BA Hons Architecture katika chuo kikuu cha Makerere nchini Uganda. Wazazi wa Ben walisha staafu, hivyo makaka na dada waliwasaidia wazazi jukumu la kumsomesha Ben. Makaka na dada wote walikuwa na mafanikio mazuri tu katika fani zao.
Baba Vero ni kaka ambae alimtangulia Ben ameoa na ana watoto watatu. Mama Vero hakuwa mtu rahisi kuishi nae, wasichan wa kazi walikuja na kuondoka, katika mwaka mmoja alibadilisha wasichana wawili/watatu. Mume ake alikereka sana na jambo hili, alimwambia aache kazi akae nyumbani alee watoto wake. Sasa shost akiacha kazi pataeleweka kweli mjini? Aliwaomba wafanyakazi wenzake wamsaidie kutafuta msichana. Baada ya muda aliletewa salamu kuwa kuna msichana amepatikana huko kijijini lakini wazazi wake wamesema ni lazima wamkabidhi binti yao kwa mtu atakae ishi nae.
Mama Vero ilibidi afunge safari kwenda huko kijijini, alifika kwenye kijiji kidogo na kuelekezwa nyumbani kwa baba na mama Hilda. Baba Hilda ndiye alikua Mkatekista wa kijiji, Hilda alikuwa na umri wa miaka 14 na ndiyo kwanza alikuwa amemaliza darasa la saba, wazazi hawakuwa na uwezo wa kumwendeleza. Mama Vero aliaswa kabisa kuwa wanamtoa binti yao akiwa mdogo si kwamba hawampendi ila wanahitaji mtu atakae mwendeleza kwa njia yeyote pia awasaidie kumlea. Mama Vero aliahidi kumlea Hilda kama mtoto wake na makabidhiwano yalifanyika. Hilda alifungasha nguo zake na kuongozona na Mama Vero.
Hilda akiwa mtoto wa mkatekista, alishafundishwa kuwa sala ni sehemu ya maisha yako, hivyo asubuhi ni lazima kusali na kabla ya kulala, mchana ukumbuke kusali Angelus. Nyumbani kwa mama Vero kazi zilianza saa 11:00 asubuhi, Hilda alitakiwa aanze kuandaa kifungua kinywa cha watoto, awaamshe na kuwasaidia usafi wa mwili, awavalishe uniforms na kuwapa kifungua kinywa kabla hawajakwenda shuleni. Siku za kwanza alishindwa kusali asubuhi muda ulikuwa unampa mkono, kitendo kilichomuuma Hilda, alimuomba Mungu amsaidie katika jaribu hilo, bila hata alarm kila siku saa 10:00 asubuhi Hilda alijikuba yuko macho na alifanya ibada yake mpaka anamaliza na kwenda kuanza kazi.
Ben alikuja likizo kwa kaka yake Baba Vero wakati Hilda alishakaa pale kwa miaka minne, sasa Hilda ni kigoli wa miaka 18 na anapendeza sana. Baba na mama Vero wakienda kazini walimuacha Hilda na Ben nyumbani. Ben kama mwanaume alishindwa kuvumilia ule urembo wa Hilda, alianza kuziingiza, Hilda alitoa nje lakini kadir siku zinavyokwenda wawili hawa walizoeana mno. Baada ya wato wote kuondoka Ben alimsaidia Hilda kufanya kazi zote za ndani, walisafisha nyumba pamoja, walifua pamoja, walipiga pasi pamoja na maongezi yalizidi kunoga. Siku walioanza kufanya mapenzi hakuna aliyetemea, Ben alijikuta anaomba msamaha baada ya kugundua amevunjua bikra ya Hilda. Hilda alilia lakini alimpenda sana Ben na walikubaliana wataendela na urafiki Ben atakaporudi kutoka chuoni. Mama Vero alishtuka ule ukaribu wa Ben na Hilda, alianza kumwambia mume wake awe anamtoa Ben jioni, haya mambo ya kuosha vyombo na wadada wa kazi si mazuri kwake.
Baada ya Ben kuondoka, huku nyuma Hilda alianza kutapika, mama Vero alijua kinachoendelea, alimwambia Hilda akatoe mimba akiona aibu ile ahadi aliyowaahidi wazazi wa Hilda ya kumlea binti yao leo apate mimba mikononi mwake. Hilda alikataa kabisa kuua, mama Hilda alimwambia kama ni hivyo arudi kwao. Hilda alimpigia simu Ben na kumweleza, Ben alikua tayari kuacha shule arudi abebe majukumu yake, makaka wote na dada ilibidi wakae chini walifikirie swala lili. Mama Vero amekataa kabisa kukaa na Hilda, na anamwekea mkwara Ben asioe mdada wa kazi, "hivi huko university hakuna wasichana?" Kwa shobo anamuuliza Ben. Dada yake Ben aliamua kukaa na Hilda mpaka Ben atakapomaliza shule. Kaka na dada wakubwa waliamua kwenda kijijini kwa kina Hilda kuwafahamisha wazazi kilichotokea.
Katika kijiji anachotoka Hilda hakuna nyumba hata moja iliyoezekwa kwa bati, nyumba zote zimejengwa kwa udongo na kuezekwa kwa nyasi. Kaka na dada waliwapigia magoti wazazi wa Hilda na kuwafahamisha yaliyotokea. Mama Hilda alilia sana, yeye aliwaza kale ka binti kake ka miaka 14 leo anaambiwa kana ujauzito. Baba alikua mwelewaji aliwaambia Hilda akiwa kama mtoto wa kike, ni lazima apate mwenzake na kama yametokea katika hali hii na mhusika yuko tayari basi tuombee uzima.
Hilda alikaa kwa wifi yake, wifi alimpenda sana Hilda, alikua na tabia nzuri, mpenda dini na pia alikua msafi sana. Baada ya kukaa kwa wifi kwa miezi sita Ben alikuwa amemaliza shule na kurudi mjini. Ben na Hilda walikabidhiwa nyumba ya familia iliyoko Mbezi Jogoo wakaanzie maisha. Ben alipata kazi na alikwenda kutoa posa nyumbani kwa kina Hilda akisaidiwa na kaka mkubwa, baada ya hapo walifunga ndoa na Hilda harusi ile ya baada ya misa ya asubuhi. Ben alifanya kazi kwa mwaka mmoja tu baadae alianzisha kampuni yake kwa msaada wa kaka zake.
Hilda na Ben waliishi kama marafiki wakubwa, kila contract Ben aliyoipata waliiombea na Baraka zilizidi kuanguka katika kampuni. Ben alidesign nyumba ya wakwe zake, ilipomalizika baba Hilda alikuwa kama chief pale kijijini. Baada ya hapo Ben alidesign nyumba yake ya ndoto. Ilikuwa kubwa ya vyumba 14 vya kulala, ofisi yake, gym, ball room na mazaga zaga mengine.
Mapenzi ya Hilda na Ben yalikuwa makubwa mno, Ben aliapa hakuna usiku atakao lala mbali ya Hilda. Hata kama ana safari ya kikazi aliwaomba wakwe zake waje kukaa na watoto yeye alisafiri na Hilda. Hilda alikuwa msiri mkubwa wa Ben, malipo yote ya kazi yakiingia Hilda aliambiwa mama imeingia cheque ya milioni 300, Hilda akiwa innocent pia naïve wala hakuwa na tamaa ya pesa. Ben ndiyo alihimiza anunue vitu vya gharama. Kimbembe kilikuwa kule kwa shost mama Vero, hakuamini kabisa anachokiona, eti Hilda nae ameolewa katika ukoo huu? Yule aliekuwa anafua sidiria zangu? Dream house ya Ben ilikuwa gumzo kwa familia nzima lakini mama Vero alijitahidi asifike, kila akialikwa either jino lilikuwa lina muuma au amefiwa na shangazi yake