So niliimwambia nitamjibu baadae kidogo,
Akanisisitizia sana juu ya umuhimu wa sisi kukutana na
kuzungumza na hususani juu ya maisha ya mwanae mtarajiwa,
Shauku ilizidi kuniajaa nyie acheni tu!
Kiume nikamwambia anicheki baada ya nusu saa ntakuwa nshadecide
Hata nusu saa haikupita akawa amepiga tena
wakati huo najiandaa kwenda ibadani,
Nilimuuliza mume wako kwani yuko wapi?
Akaniambia yupo South Africa na atarudi Tz by Tuesday,
Nikamwambia anataka tuonane wapi?
Akasema nichague mimi sehemu ya kukutana, tena ikiwezana for the whole Monday night
Dar nilipata vigugumizi kibao sana na wakati huo huo
Nawaza ni wapi sehemu nzuri tunayoweza kuwa pamoja na kuzungumza kwa kina,
Mawazo yalinipeleka tuende Bagamoyo,
Ila sikujua ni sehemu gani, niliwaza kidogo ila baadae nikamwambie tuende Kibaha,
Kuna sehemu moja tulikuwa tunakutana kipindi tuna date,
Alifurahi nilivyomwambia hiyo sehemu
akanipa time atakayokuwa amefika na akaniambia atafika home
kwake kwanza kuweka baadhi ya mizigo
kwasababu kuna ndugu wa mume wake huwa anakuja kumpokea
mara zote pindi mumewe hayupo.
Nikamwambia haina shida ye aweke tu mambo yake
vyema,
Baada ya mazungumzo yale tuliagana na nikamtaarifu naenda kusali,
Niombee na mimi tena usimsahau na mtoto wetu,
ndiyo kauli aliyoitoa kabla hajakata simu..
Nikaenda zangu kanisani, nasalia pale Kimara.......
malizia bana
umemaliza au unaendelea?
naendelea...
naandika
Weka picha
malizia bana
...Nilitoka kanisani muda wa saa 6 mchana,
Mawazo yangu yote bado yapo juu ya ahadi ya jumatatu,
Niliwaza sana hadi nikaona kama siku haiendi, nilikaa kwenye kochi
kwa muda wa saa moja hivi,
Kuna mshikaji wangu alikuja pale na tukatoka kwa ajili ya lunch!
Siku mwambia chochote kile juu ya outing niliyokuwa nimepanga kutoka na ex wangu ambaye ni mke
wa mtu.
Tuliingia bar moja hivi na tulikaa sana pale, hadi usiku
tukisindikwa na vinywaji..
Nilirudi home na kujitupa kitandani, pombe kumkichwa
Na usingizi ulinichukua mazima,
Nilishtuka kama saa kumi hivi, kucheki simu kulikuwa na missed calls kama nane hivi
Tatu zikiwa ni za huyu ex wangu na nyingine za watu wengine tu!
Dah nikajaribu kupiga nikaambiwa haipo hewani!!
Basi nikaendelea kulala kwa saa moja tena,
Kutoka Kimara kuja huku Temeke kazini huwa
inanilazimu niamke mapema sana ili niwahi job
Nikaja kazini ila bado akili yangu inawaza juu ya mtoko wa baadae
Huwa tunamaliza kazi saa nane na nusu mchana,
Muda wakufunga ofisi ukafika no any call from my ex...
malizia bana
umemaliza au unaendelea?
aahh...kwahyo una bipu bipu habari yako..
malizia basi ndo nini? umeazishaje story huku ukijua mda wa lunch unakaribia na auwezi maliza ndo nin?
"Boss" alikuwa amempitia karibu, ilibidi asimame kidogo. Ataendelea tu "Boss" akiondoka.