Mapendekezo yangu kuhusu Kikotoo cha Kodi bandarini

Mparee2

JF-Expert Member
Sep 2, 2012
2,610
4,327
Napendekeza Mamlaka ya Mapato waweke kikokotoo rahisi kwa walipa kodi kukielewa.

Mfano: Kuingiza gari (waweke categories kama tano tu hivi na bei yake ambayo itajumuisha kodi zote za serikali.

Labda kibaki malipo ya clearance agent peke yake na hata ikibidi na yeye ajumlishwe

Mfano: Ukiandika tu:
Toyota premio, cc 1450, mwaka 2007- ije bei 5,500,000 (all inclusive)
Nissan extrai cc 1990, mwaka 2005 ije bei 7200,000 (all inclusive)

Haya mambo ya kulipa kodi sijui sita? thus; baada ya kulipa main taxi ya serikali, bado unaambiwa tena ulipe, shipping line, port charge, wharf ace, car & plate number; naona hiyo ni kuongeza mlolongo na hivyo kuchangia upotevu wa pesa.

Kwanini wasijumlishe zoote halafu mtu akilipa inajigawa automatically kila moja inaenda account yake? Au hatuna wataalam wa kutengeneza hiyo program rahisi?

Ili kodi ilipwe vizuri, kunatakiwa kuwe na mfumo mzuri, rahisi na wawazi kwa walipa kodi
 
Hiyo all inclusive maana Yake hujaorodheshewa hizo Kodi ila unazilipa hizo Kodi.

Sasa kilichopungua Ni nini Sasa.
 

Used Motor Vehicle Valuation System - Used Motor Vehicle Valuation System

gateway.tra.go.tz
gateway.tra.go.tz

Unachoongea 80% kipo hapo
emoji1483.png
 
Mkuu hili linawezekana, Mamlaya ya Ushuru Kenya (KRA) wana mfumo wa namna hii. Ukiingiza gari kupitia Bandari ya Mombosa unafanya mwamala mmoja tu, hii ikifanyika hapa kwetu itapunguza mda wa kugomboa gari katika bandari yetu na pia kuongeza ufanisi.
 
Back
Top Bottom