Mapendekezo ya 'Ruti' mpya Dar

Mapendekezo ya 'Ruti' mpya Dar

singojr

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2014
Posts
5,314
Reaction score
6,896
Habari,

Jiji la Dar es salaam linakuwa na kutanuka kwa kasi sana. Lakini kuna maeneo yamefikiwa na barabara lakini hakuna huduma za usafiri wa Umma kuyafikia maeneo hayo.

Nimewahi kupendekeza ruti kadhaa huko awali na zikafanyiwa kazi hivyo napata hamasa ya kupendekeza nyingine kwa imani kuwa zitakuwa msaada kwa wakazi wa maeneo hayo.
1. Bunju-Kariakoo(Magari Makubwa)
2. Bunju-Posta(Magari Makubwa)
3. Madale-Makumbusho(kupitia makongo juu)
4. Kawe-Kimara(kupitia njia nne, matosa)
5. Mawasiliano-Kinyerezi/Segerea( kupitia Kimara, Bonyokwa)
6.Madele-Makumbusho(kupitia Tegeta kibaoni) hii ilikuwepo lakini sijajua kilichoiua.

Kwasababu kuna kituo kipya Mwenge kikianza baadhi ya ruti zinaweza kuanzia hapo pia. Hii itapunguza usumbufu na gharama kwa wananchi.
 
Habari,
Jiji la Dar es salaam linakuwa na kutanuka kwa kasi sana. Lakini kuna maeneo yamefikiwa na barabara lakini hakuna huduma za usafiri wa Umma kuyafikia maeneo hayo...
Mbezi Mwisho (Moro road) - Masaki
Buguruni - Makumbusho (kupitia Shekilango)
Kivukoni - Masaki kupitia Saint Peter

Nafikiri hakuna ruti nyingi zinazoishia Posta kwani Posta hakuna eneo kubwa linalofaa kuwa kituo kikubwa cha daladala.
 
Naongezea madale_mawasiliano kupitia makongo juu,madale _kariakoo kupitia matosa ,ubungo ,buguruni mpaka kariakoo

Asante kwa kuongezea naamini wataziona
 
Hili swala wahusika wapo humu tunaomba walifanyie kazi. Fikiria watu wanaoishi maeneo ya Goba akitaka kwenda msasani anatumia magari matatu. Yani goba makumbusho, makumbusho morocco, afu ndo wapate la kwenda msasani. Kwa wanaoishi madale ndo wanatumia magari manne kabisa
 
Niliisahau nyomi ya Msumi hivi kuna lami kule? Last time nilikuwa nawaona wakifika Mbezi Mwisho wananawa ili wasiende mjini na mavumbi
dah.....ni shida sana sijui huku waliiasi serikali au laaa
 
Kuna kipindi nilisikia kuna barabara itapita huko mpaka Mabwepande-Bunju
hamna dalili, kuna kipande kama km 4 hivi kinajengwa kwa level ya lami lakini sasa ni mwaka wa pili hamna hata dalili ya kwisha!!!!
 
hamna dalili, kuna kipande kama km 4 hivi kinajengwa kwa level ya lami lakini sasa ni mwaka wa pili hamna hata dalili ya kwisha!!!!

Poleni sana kwa nyomi ile panahitaji lami kuliko hata kule Tandale
 
Mpigi Magoe na Msumi sidhani kama wakazi wa kule wanaowahi kwenda maeneo ya kazi huwa wanamaliza usingizi wao. Ni mwendo wa kuamka saa 10 alfajiri
kwa sasa hamna maeneo ya dar yenye changamoto za usafiri kama ubungo watu wengi lakini barabara zote ni za vumbi
 
Back
Top Bottom