Mapendekezo ya namna bora ya kuhamia Dodoma

East African

JF-Expert Member
Nov 27, 2013
704
989
Suala la kuhamia Dodoma sio gumu kama watu wanavyofikiri, pamoja na changamoto zake lakini litafanya tuwe na mji mwingine mkubwa angalau wenye watu hata milioni mbili siyo mbaya ili kuleta uwiano fulani.
Mapendekezo yangu.

1. Zihame ofisi zote za wizara; yaani tuna wizara zipatazo 20 hivi. hivyo mawaziri, makatibu, makamishna, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.

2. Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa makao yao makuu pia yaende.

3. Kuhusu ofisi za mabalozi zenyewe ziachiwe kuamua kila balozi ataamua kwenda au kubaki Dar.

3. Taasisi (parastatals) zibaki, mfano;- EWURA, TANESCO, TPA, TPDC, TIC EPZ, TRA head office, TCRA, NSSF, ATC TCAA na zingine zinaweza kubaki kwa kuwa hizi zinategemea biashara na makampuni.

Mathalani TANAPA ipo Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha utalii.

4. National housing isimamishe miradi ambayo bado haijaanza na iweke nguvu zaidi Dodoma hasa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi.

5. Reli ya kisasa iharakishwe Dar-Dom ili kufanya miji hii miwili mikubwa iwe na usafiri wa kuaminika. Mathalani reli ya standarge gauge ya Nairobi Mombasa itakuwa na speed ya kilometa 135 kwa saa. Hivyo Dar - Dom ni kilometa 500 hivi, kwa hiyo itachukua takribani masaa yasiozidi manne.

Na iwepo treni ya express Dom to Dar bila kusimama njiani na iwepo kila baada ya masaa mawili na wafanyakazi wa serikali walazimike kutumia hii pindi wanapoenda kikazi kati ya miji hii miwili. Mfano mhasibu anaweza kutoka Dar saa 12 na kufika Doma saa 4 na kumaliza shughuli na saa 10 akapanda train na kurudi.

6. Uwanja wa Dodoma badala ya kuupanua huu uliopo napendekeza hizo Bilioni 10 zilizotengwa zianze uwanja mpya wa kimataifa na utaongezewa fedha mwaka unaofuata.

Tukifanya hivi Dar itaanza kurekebishwa polepole na hata foleni itapungua sana na kupelekea biashara kukua. Pia kumbuka kuwa hata Dodoma pia itavuta wawekezaji wa viwanda na makampuni.

Kumbuka kuwa viwanda vinafuata mahali penye wanunuzi wengi. Hapa nashauri viwanda viwekwe mbali na mji ili kuzuia msongamano.

Haya ni mapendekezo yangu ya awali na tunaruhusiwa kuyaboresha na kuongeza mengine mazuri.

Karibuni.
Yakifanyika haya naamini hadi mwaka 2019 tutakuwa Dodoma na mji wa Dodoma utakuwa jiji zuri sana
 
Nakubaliana na kila sentensi yako. Umenena. Hili la kuhamia Dodoma ni muhimu sana. Faida kubwa ni kuchochea maendeleo ya mikoa mingine. Ama kweli Raisi tunaye.
 
Kuhamia Dodma inawezekana ila sio kwa muda mfupi hivyo miaka minne anaona mingi ila ni michache, kuhamisha serikali sio kama kuhamisha kitanda kutoka chumba x kwenda chumba yinataka mipango na bajeti
 
Tusiogope kuhama ili mradi Rais atekeleze kwa vitendo. Na changamoto haziepukiki, kwani hata mradi wa mwendo kazi ulianza kwa changamoto nyingi lakini angalau unafanya vizuri.
 
Suala la kuhamia Dodoma sio gumu kama watu wanavyofikiri, pamoja na changamoto zake lakini litafanya tuwe na mji mwingine mkubwa angalau wenye watu hata mili 2 sio mbaya ili kuleta uwiano fulani.
Mapendekezo yangu.
1. Zihame ofisi zote za wizara; yaani tuna wizara zipatazo 20 hivi. hivyo mawaziri, makatibu, makamishna, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
2. Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa makao yao makuu pia yaende.
3. Kuhusu ofisi za mabalozi zenyewe ziachiwe kuamua kila balozi ataamua kwenda au kubaki Dar.
3. Taasisi (parastatals) zibaki, mfano;- EWURA, TANESCO, TPA, TPDC, TIC EPZ, TRA head office, TCRA, NSSF, ATC TCAA na zingine zinaweza kubaki kwa kuwa hizi zinategemea biashara na makampuni. Madhalani TANAPA ipo Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha utalii.
4. National housing isimamishe miradi ambayo bado haijaanza na iweke nguvu zaidi Dodoma hasa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi.
5. Reli ya kisasa iharakishwe Dar-Dom ili kufanya miji hii 2 mikubwa iwe na usafiri wa kuaminika. Madhalani reli ya standarge gauge ya Nairobi Mombasa itakuwa na speed ya kilometa 135 kwa saa. hivyo Dar - Dom ni kilometa 500 hivi, kwa hiyo itachukua takribani masaa yasiozidi 4. Na iwepo treni ya express Dom to Dar bila kusimama njian na iwepo kila baada ya masaa 2 na wafanyakazi wa serikali walazimike kutumia hii pindi wanapoende kikazi kati ya miji hii miwili. Mfano mhasibu anaweza Kutoka Dar saa 12 na kufika Doma saa 4 na kumaliza shughuli na saa 10 akapanda train na kurudi.
6. Uwanja wa Dodoma badala ya kuupanua huu uliopo napendekeza hizo Bil 10 zilizotengwa zianze uwanja mpya wa Kimataifa na utaongezewa fedha mwaka unaofuata.
Tukifanya hivi Dar itaanza kurekebishwa polepole na hata foleni itapungua sana na kupelekea biashara kukua. Pia kumbuka kuwa hata Dodoma pia itavuta wawekezaji wa viwanda na makampuni. Kumbuka kuwa viwanda vinafuata mahali penye wanunuzi wengi. Hapa nashauri viwanda viwekwe mbali na mji ili kuzuia msongamano.
Haya ni mapendekezo yangu ya awali na tunaruhusiwa kuyaboresha na kuongeza mengine mazuri.
Karibuni.
Yakifanyika haya naamini hadi mwaka 2019 tutakuwa dodoma na mji wa Dodoma utakuwa jiji zuri sana
Yani kwasababu umependekeza ndio unasema kuhamia Dodoma ni kitu rahisi na sio gumu? Hivi kwenye bajeti za wizara zote mwaka huu umesikia hata moja iliyotenga fungu la kuhamia Dodoma? Unafahamu kuna wizara nyingi wana idara ambazo kwa mwaka huu hawajapewa fedha za kuwezesha core activities? Unafahamu hata OC za wizara nyingi hazitoshi hata kulipia pango la ofisi kwa mwaka huu wa fedha Dodoma wataendaje? Wizara inayoongoza kwa kuwa na hali mbaya kifedha ni Ile iliyopo chini ya WAZIRI MKUU, nasubiri kuona muujiza gani atafanya. Maana bado watanzania wanasubiri Tanzania ya viwanda, milioni 50 kila kijiji leo tena tunaibuka na Dodoma.
 
treni ya high speed ni bei pia kama nauli ya kawaida basi 20'000 express train 40'000 au zaidi ya hapo kwenda na kurudi kwa week ? je hao abiria wachache watawezesha kurudisha gharama na kuwezesha mmiliki kupata faida

angalia running coast

acha wahamie jumlajumla tu dsm kuna nini bahari?

tafakari upya
 
Suala la kuhamia Dodoma sio gumu kama watu wanavyofikiri, pamoja na changamoto zake lakini litafanya tuwe na mji mwingine mkubwa angalau wenye watu hata mili 2 sio mbaya ili kuleta uwiano fulani.
Mapendekezo yangu.
1. Zihame ofisi zote za wizara; yaani tuna wizara zipatazo 20 hivi. hivyo mawaziri, makatibu, makamishna, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
2. Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa makao yao makuu pia yaende.
3. Kuhusu ofisi za mabalozi zenyewe ziachiwe kuamua kila balozi ataamua kwenda au kubaki Dar.
3. Taasisi (parastatals) zibaki, mfano;- EWURA, TANESCO, TPA, TPDC, TIC EPZ, TRA head office, TCRA, NSSF, ATC TCAA na zingine zinaweza kubaki kwa kuwa hizi zinategemea biashara na makampuni. Madhalani TANAPA ipo Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha utalii.
4. National housing isimamishe miradi ambayo bado haijaanza na iweke nguvu zaidi Dodoma hasa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi.
5. Reli ya kisasa iharakishwe Dar-Dom ili kufanya miji hii 2 mikubwa iwe na usafiri wa kuaminika. Madhalani reli ya standarge gauge ya Nairobi Mombasa itakuwa na speed ya kilometa 135 kwa saa. hivyo Dar - Dom ni kilometa 500 hivi, kwa hiyo itachukua takribani masaa yasiozidi 4. Na iwepo treni ya express Dom to Dar bila kusimama njian na iwepo kila baada ya masaa 2 na wafanyakazi wa serikali walazimike kutumia hii pindi wanapoende kikazi kati ya miji hii miwili. Mfano mhasibu anaweza Kutoka Dar saa 12 na kufika Doma saa 4 na kumaliza shughuli na saa 10 akapanda train na kurudi.
6. Uwanja wa Dodoma badala ya kuupanua huu uliopo napendekeza hizo Bil 10 zilizotengwa zianze uwanja mpya wa Kimataifa na utaongezewa fedha mwaka unaofuata.
Tukifanya hivi Dar itaanza kurekebishwa polepole na hata foleni itapungua sana na kupelekea biashara kukua. Pia kumbuka kuwa hata Dodoma pia itavuta wawekezaji wa viwanda na makampuni. Kumbuka kuwa viwanda vinafuata mahali penye wanunuzi wengi. Hapa nashauri viwanda viwekwe mbali na mji ili kuzuia msongamano.
Haya ni mapendekezo yangu ya awali na tunaruhusiwa kuyaboresha na kuongeza mengine mazuri.
Karibuni.
Yakifanyika haya naamini hadi mwaka 2019 tutakuwa dodoma na mji wa Dodoma utakuwa jiji zuri sana

Suala la kuhamia Dodoma sio gumu kama watu wanavyofikiri, pamoja na changamoto zake lakini litafanya tuwe na mji mwingine mkubwa angalau wenye watu hata mili 2 sio mbaya ili kuleta uwiano fulani.
Mapendekezo yangu.
1. Zihame ofisi zote za wizara; yaani tuna wizara zipatazo 20 hivi. hivyo mawaziri, makatibu, makamishna, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
2. Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa makao yao makuu pia yaende.
3. Kuhusu ofisi za mabalozi zenyewe ziachiwe kuamua kila balozi ataamua kwenda au kubaki Dar.
3. Taasisi (parastatals) zibaki, mfano;- EWURA, TANESCO, TPA, TPDC, TIC EPZ, TRA head office, TCRA, NSSF, ATC TCAA na zingine zinaweza kubaki kwa kuwa hizi zinategemea biashara na makampuni. Madhalani TANAPA ipo Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha utalii.
4. National housing isimamishe miradi ambayo bado haijaanza na iweke nguvu zaidi Dodoma hasa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi.
5. Reli ya kisasa iharakishwe Dar-Dom ili kufanya miji hii 2 mikubwa iwe na usafiri wa kuaminika. Madhalani reli ya standarge gauge ya Nairobi Mombasa itakuwa na speed ya kilometa 135 kwa saa. hivyo Dar - Dom ni kilometa 500 hivi, kwa hiyo itachukua takribani masaa yasiozidi 4. Na iwepo treni ya express Dom to Dar bila kusimama njian na iwepo kila baada ya masaa 2 na wafanyakazi wa serikali walazimike kutumia hii pindi wanapoende kikazi kati ya miji hii miwili. Mfano mhasibu anaweza Kutoka Dar saa 12 na kufika Doma saa 4 na kumaliza shughuli na saa 10 akapanda train na kurudi.
6. Uwanja wa Dodoma badala ya kuupanua huu uliopo napendekeza hizo Bil 10 zilizotengwa zianze uwanja mpya wa Kimataifa na utaongezewa fedha mwaka unaofuata.
Tukifanya hivi Dar itaanza kurekebishwa polepole na hata foleni itapungua sana na kupelekea biashara kukua. Pia kumbuka kuwa hata Dodoma pia itavuta wawekezaji wa viwanda na makampuni. Kumbuka kuwa viwanda vinafuata mahali penye wanunuzi wengi. Hapa nashauri viwanda viwekwe mbali na mji ili kuzuia msongamano.
Haya ni mapendekezo yangu ya awali na tunaruhusiwa kuyaboresha na kuongeza mengine mazuri.
Karibuni.
Yakifanyika haya naamini hadi mwaka 2019 tutakuwa dodoma na mji wa Dodoma utakuwa jiji zuri sana

kwa miaka 4 na miezi nane ni ndoto. kunamambo mengi sana ya kuzingatia pia kiusalama na infrastructure zake

kile ki ikulu hakitoshi kabisa pia
 
G
Wachagga walivyoikamata Dodoma kweli hawa watu watabakia kuwa juu. Nimekaa Dodoma biashara nyingi kubwa kubwa zinamilikiwa na hawa watu na serikali inaenda huko ndio watazidi kunufaika.
Watanzania lini tutasahau ukabila? Mchagga akinufaika kuna ubaya gani? Mbona husemi waarabu na wahindi ambao baadhi yao wana 'makazi' mawili ndani na nje ya nchi.

Juzi jmosi siku ya kufanya usafi nilikutana na mfanya biashara wa kihindi ana kamgahawa city center. Tunafahamiana, akanisimamisha na kuanza kulalamika kuwa amekuwa harassed sana kwa kuwa alifungua mgahawa muda wa zoezi la usafi. Akanung'unika kwamba wao wanyabiashara ndio walipa kodi wakubwa kwa nini asiachwe kufanya biashara yake ya mgahawa maana wananchi wanahitaji huduma hiyo wakati wote. Akawa mkali akidai kama mambo yenyewe ni haya wanaweza kuondoka nchini na Serikali kukosa mapato!

Nilimshangaa sana mtu yule ambaye ameishi na kuendesha mgahawa huo kwa miaka mingi. Nikamwambia anaona taabu gani kutii agizo la Serikali kufunga mgahawa kwa saa kadha? Hakuwa na jibu la kuridhisha.

Mchagga aachwe ajitengenezee fedha popote nchini maana hana pa kwenda. Tanzania ni kwake hawezi kuwa mguu nani mguu nje ndani ya nchi yake..
 
Wachagga walivyoikamata Dodoma kweli hawa watu watabakia kuwa juu. Nimekaa Dodoma biashara nyingi kubwa kubwa zinamilikiwa na hawa watu na serikali inaenda huko ndio watazidi kunufaika.
AMEN na iwe hivyo
 
Mawazo mazuri.. Yani hapo hakuna sababu za kutohamia Dom. Maraisi watatu waliopita ni wa pwani kwa hiyo agenda ya kuhamia Dom haikuwepo vichwani mwao. Huyu wa sasa sio mpwani na anawazia serikali kiujumla. Ona JK alivyotaka kutengeneza bandari Bagamoyo na wakati zilizopo hazifanyi kazi na zina kina kirefu tu,hayo yalikua mawazo ya kipwanipwani. Magu kwa hili nakuapa tano,hamishia serikali yote capital city,asietaka aache kazi. Hakuna kubembelezana kwenye hili
 
Hili swala umelichukulia juu juu sana. Maneno ya JPM ni ndani ya miaka4, Unadhani ndani ya hiyo miaka hayo yote yatawezekana?

Ni jambo zuri kufanya Dodoma kuwa makao makuu ila hicho ndiyo kipaumbele chetu kweli kwa sasa? Tatizo la serikali siku zote ni vipaumbele. Hizo pesa zingeweza kufanya mambo mengi sana ya maendeleo yenye tija kwa taifa zima badala ya kuhamishia serikali to Dodoma ndani ya miaka minne.

Ningependekeza hili swala lisifanywe kwa haraka badala yake lifanywe taratibu na kwa umakini wa hali ya juu ili kuepusha kurudia makosa yale yale. Aidha ningependekeza ofisi na wizara mbali mbali zitawanywe kwenye mikoa mbali mbali ili kuleta uwiano, usawa na kukuza maeneo tofauti nchini.
 
Ni Kweli kabisa ulichosema...... Wachaga ni wengi sana Dodoma na wana miliki biashara nyingi sana kaubwa hapo Dodoma.....
Tunajadili serikali kuhamia dodoma,sio habari ya wachaga khaa!!
Kuhamia Dom si wazobaaaya chamuhimu tufanyemambo kwa kuzingatia umuhimu,gharama za kuhama nikubwa wakati huohuo tunashida nyiingi za mambo ya muhimu Kama maji,umeme,afya nk.
Nchi iendeshwe kwa maslahi na mawazo mapana ya wananchi ili matatizo makubwa yatatuliwe kwanza. Nionavyo nibora kuharakishia wananchi maji au hospitali kuliko kuharakisha kwenda dom
 
Nafikiri kuna sababu ilyopelekea Dodoma kuteuliwa na Mwalimu JK kuwa makao makuu ya nchi na sidhani kama hiyo sababu iliwekwa wazi na kujadiliwa kwa kina na kueleweka na sidhani kama watu wengi tunaijua sababu hiyo,alafu tujiulize mwalimu alifeli wapi kuhamishia makao makuu ya nchi kuwa dom pamoja na waliomfuatia?tukipata majibu hayo ndiyo tutapima na kuona kuhamia dom inawezekana na kama italeta tija kwa Taifa.Sipingi kuhamia dom ila nataka kujiridhisha na sababu ya msingi kuhamia huko na pia kama ni kuleta maendeleo basi iangaliwe mikoa yote hata kwa awamu kuipelekea maendeleo na kuifanya ichangamke kibiashara,kiuchumi na kijamii,tuwe kama Nigeria
 
Serikali haina uwezo wa kuhamia dodoma.
Muda uliobaki ni mdogo sana.
 
Fear of the unknown. Ndo kinachotusumbua. Mtoa mada ameongelea vizuri sana jinsi gani hii kitu iwe managed. Hilo la kuhama ni jukumu la Waziri na wizara yake. Tuwaachie wao. Watapata wapi pesa wataumiza wao vichwa. Mheshimiwa Raisi amepigilia msumari leo juu ya kuhama na Waziri Mkuu ashatoa agizo nadhani hakuna la zaidi hapa. Waziri mkuu anatangulia, Raisi akifuata sasa tuone nani anabaki.
 
Watu wanasema Miaka 4 ni midogo kana kwamba mpango huu ndio unaanza leo...
 
Back
Top Bottom