Nyanya mbichi
JF-Expert Member
- Nov 10, 2011
- 3,716
- 2,218
Wahusika mnapinga sana kuhamia dom du
Train hizi ni nzur sana watu wengi watahama toka kwenye mabasi hvyo ushindani utapelekea mabasi ya hovyo yote kukosa abiria maana train itatumia muda mfupi zaidtreni ya high speed ni bei pia kama nauli ya kawaida basi 20'000 express train 40'000 au zaidi ya hapo kwenda na kurudi kwa week ? je hao abiria wachache watawezesha kurudisha gharama na kuwezesha mmiliki kupata faida
angalia running coast
acha wahamie jumlajumla tu dsm kuna nini bahari?
tafakari upya
mzee huu uzi ni unabii mtupu yanatimia, sasa hivi bila m10+ hupati kiwanja cha maana DodomaSuala la kuhamia Dodoma sio gumu kama watu wanavyofikiri, pamoja na changamoto zake lakini litafanya tuwe na mji mwingine mkubwa angalau wenye watu hata milioni mbili siyo mbaya ili kuleta uwiano fulani.
Mapendekezo yangu.
1. Zihame ofisi zote za wizara; yaani tuna wizara zipatazo 20 hivi. hivyo mawaziri, makatibu, makamishna, wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
2. Mahakama kuu na Mahakama ya rufaa makao yao makuu pia yaende.
3. Kuhusu ofisi za mabalozi zenyewe ziachiwe kuamua kila balozi ataamua kwenda au kubaki Dar.
3. Taasisi (parastatals) zibaki, mfano;- EWURA, TANESCO, TPA, TPDC, TIC EPZ, TRA head office, TCRA, NSSF, ATC TCAA na zingine zinaweza kubaki kwa kuwa hizi zinategemea biashara na makampuni.
Mathalani TANAPA ipo Arusha kwa kuwa ndio kitovu cha utalii.
4. National housing isimamishe miradi ambayo bado haijaanza na iweke nguvu zaidi Dodoma hasa kujenga nyumba za kuishi wafanyakazi.
5. Reli ya kisasa iharakishwe Dar-Dom ili kufanya miji hii miwili mikubwa iwe na usafiri wa kuaminika. Mathalani reli ya standarge gauge ya Nairobi Mombasa itakuwa na speed ya kilometa 135 kwa saa. Hivyo Dar - Dom ni kilometa 500 hivi, kwa hiyo itachukua takribani masaa yasiozidi manne.
Na iwepo treni ya express Dom to Dar bila kusimama njiani na iwepo kila baada ya masaa mawili na wafanyakazi wa serikali walazimike kutumia hii pindi wanapoenda kikazi kati ya miji hii miwili. Mfano mhasibu anaweza kutoka Dar saa 12 na kufika Doma saa 4 na kumaliza shughuli na saa 10 akapanda train na kurudi.
6. Uwanja wa Dodoma badala ya kuupanua huu uliopo napendekeza hizo Bilioni 10 zilizotengwa zianze uwanja mpya wa kimataifa na utaongezewa fedha mwaka unaofuata.
Tukifanya hivi Dar itaanza kurekebishwa polepole na hata foleni itapungua sana na kupelekea biashara kukua. Pia kumbuka kuwa hata Dodoma pia itavuta wawekezaji wa viwanda na makampuni.
Kumbuka kuwa viwanda vinafuata mahali penye wanunuzi wengi. Hapa nashauri viwanda viwekwe mbali na mji ili kuzuia msongamano.
Haya ni mapendekezo yangu ya awali na tunaruhusiwa kuyaboresha na kuongeza mengine mazuri.
Karibuni.
Yakifanyika haya naamini hadi mwaka 2019 tutakuwa Dodoma na mji wa Dodoma utakuwa jiji zuri sana
ulikuwa mzuri,,ninyie TU mliozoea kukaa Dar ndo mnaleta shidaSasa mbona MDA wote viongozi wako Dar 9 years baada ya Jpm kukurupuka na uamuzi huu? Serikali ni rasmi ina miji mikuu miwili ni nini faida Yake?