Mapendekezo ya CUF kwa JK kuhusu Katiba haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mapendekezo ya CUF kwa JK kuhusu Katiba haya

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MziziMkavu, Dec 6, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 6, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  5th December 2011


  [​IMG]
  Naibu katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF Bara Julius Itatiro akisisitiza jambo wakati akiongea na wandishi wa habari kuhusu kwenda Ikulu kuonana na Rais Jakaya Kikwete kuwasilisha mapendekezo yao kuhusu namna bora ya utekelezaji wa sheria ya mabadiliko ya katiba 2011 katika kuifanyia marekebisho (kulia)ni Naibu katibu Sekretariet ya Vijana Taifa Abubakari Kitoyo9Picha na Omar Fungo)


  Mazungumzo kati ya Rais Jakaya Kikwete na ujumbe wa serikali yake pamoja na viongozi waandamizi wa Chama cha Wananchi (CUF), yamezaa makubaliano kadhaa, ikiwamo wanasheria pande zote mbili kukutana ili kujadili namna bora ya utekelezaji wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba ya Mwaka 2011 kama ilivyopendekezwa na CUF.

  Pia pande mbili hizo zimekubaliana CUF iwasilishe mapendekezo rasmi serikalini ya namna ya kurekebisha sheria hiyo pamoja na mchakato wa mabadiliko ya katiba.

  Makubaliano hayo yalifikiwa na pande mbili hizo katika kikao cha pamoja kilichofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam, Desemba 2, mwaka huu.

  Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alisema katika kikao hicho, walimkabidhi Rais Kikwete mapendekezo na maoni, kuhusu namna bora ya utekelezaji wa sheria hiyo.
  Maeneo hayo ni pamoja na uteuzi wa Makamishna wa Tume ya Katiba pamoja na Sekretarieti yake; hadidu za rejea za Tume ya Katiba;

  uhuru mpana usio na vikwazo wa wananchi katika kutoa maoni na marekebisho ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na sekretarieti yake. Alisema maeneo, ambayo yanapaswa kuzingatiwa katika kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili kuifanya kuwa bora zaidi, ni pamoja na kifungu cha 6 (4) cha sheria hiyo.

  Mtatiro alisema kifungu hicho kimeweka sharti linalokataza kiongozi wa chama cha siasa wa ngazi ya taifa, mkoa au wilaya kuteuliwa kuwa mjumbe wa Tume ya Katiba.

  Hivyo, alisema wamependekeza marekebisho ya kuondoa sharti hilo, kwa vile wanaamini kuwa katiba licha ya kuwa ni waraka wa kisheria, pia ni waraka wa kisiasa unaobeba malengo na matarajio ya taifa.

  Pia wamependekeza watu watakaoteuliwa katika tume hiyo wawe waadilifu, wanaoheshimika na kuaminika mbele ya jamii, wawe na ujuzi na uzoefu wa kutosha katika masuala ya katiba wakiwa na uelewa mpana wa mambo ya sheria, siasa, uchumi na maendeleo.

  Alisema kuteuliwa kwa watu wa aina hiyo kutajenga heshima na imani kubwa ya tume mbele ya jamii na hivyo kuondoa wasiwasi na hofu zinazojengwa za kutokuwapo kwa nia ya dhati na ya kweli ya kupata katiba ya kidemokrasia inayoyotokana na Watanzania wenyewe.

  Mapendekezo mengine, ni Hadidu za Rejea za Tume ya Katiba kujulikana mapema na kufanywa sehemu ya sheria hiyo kama jedwali na pia ziwe zinatoa uhuru mpana na zisizobana kwa namna yoyote ili tume au wananchi watoe maoni yao kwa maeneo watakayoona yanapaswa kuzingatiwa na kuwamo katika katiba mpya.  CHANZO: NIPASHE


   
 2. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,827
  Trophy Points: 280
  CUF ni wehu na huyu itatiro. wao walipitisha muswada meaning waliuafiki kwa kutokuwa na mashaka nao. Sasa walikwenda kwa Kikwete kufanya nini. Wao wanaiga tu kufanana na CDM. After all CUF bara ni kama is non existent!!!
   
 3. KASHOROBANA

  KASHOROBANA JF-Expert Member

  #3
  Dec 6, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,249
  Likes Received: 406
  Trophy Points: 180
  Mtatiro unajidanganya kuwa tutadanganyika na porojo zenu, nyie mswada huu mliuafiki katika kikao mipasho cha bunge kilichoisha nov 2011, leo mna mdanganya nani??? Nyie mmechemsha nawashauri mkajiimarishe zanzibar huku bara tuliisha waelewa kuwa mnatumiwa na ccm kudhohofisha upinzani ivyo hamna chenu, kumbuka iwapo itatengenezwa katiba mbaya itawahathiri wote nanyi cuf mkiwemo, hivyo mjue hatudanganyikiiiiii....
   
 4. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #4
  Dec 7, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Masikini kafa/kafu mnasumbuka kweli na kopi endi pesti yenu.
  Mmekwisha kabisaaaaaaaaa na ndivyo tlp nayo ilivyokwenda na maji. Mtabaki Zanzibar na sisi huku Tanganyika tumeamua kuwapiga chini. Hamna jipya zaidi ya porojo za Mtatiro kila siku ili aonekane kuwa na yeye yupo. Hadhi yake huku bara ilishakuwa 0%
  .
   
 5. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipya kwa CUF/CCM B. Wanataka kuvunja ndoa yao na CCM?? Siwaellewi, watatue mgogoro wao kwanza...
   
 6. U

  UZEE MVI Senior Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  So why did you accept the muswada mia kwa mia kule mjengoni? Were doing comedy kule mjengoni or ur doing it in this speech?
   
Loading...