Mapendekezo kuhusu ubora wa elimu

GODZILLA

JF-Expert Member
Dec 26, 2014
5,902
10,503
Mbali na jitihada za nchi kuhakikisha uandikishaji mkubwa wa wanafunzi mashuleni, ujenzi wa miundombinu ya shule, na mambo mengine mengi, yafuatayo ni baadhi ya mapendekezo ya kuboresha elimu:

1.Kupunguza maudhui yaliyomo kwenye silabasi

Nimefuatilia maudhui yaliyomo kwenye masomo ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari, mengi hayana umuhimu wala hayana relevance kwa nyakati zetu hizi.

Mambo kama miaka ya matukio, sijui kinjektile alifia bwawa gani, au mgunduzi wa mto nile anaitwa nani. Hayo maudhui sidhani kama yana tija yoyote.

Badala yake, mitaala na silabasi zijikite kutoa maudhui ambayo ni ya msingi mno (fundamentals). Vitu ambavyo ni very basic, short and understandable.

Hii itawafanya wanafunzi wasiwe makasuku wa kukariri miaka na mambo yasiyo na relevance.

Masomo kama historia, maarifa ya jamii, jografia, na uraia yamejaa irrelevant na unnecessary contents. Punguzeni hayo matakataka hayana msaada wowote.

2. Mitihani itumike kupima uelewa na sio kupima uwezo wa kukariri

Nimefuatilia mitihani mingi ya shule za msingi ni kama inalenga kupima uwezo wa kumbukumbu badala ya uwezo wa kiakili na kuakisi yaliyofundishwa darasani

Mfano :

-Mkwawa alifariki mwaka gani!?

-Nyerere alienda london mwaka gani?

Na matakataka mengine ya aina hiyo!

Mitihani itumike kumuwezesha mwanafunzi kutoa fikra zake huru, ni nini anachofikiria kuhusu jambo husika pamoja na uhusiano wa maudhui hayo na maisha ya kila siku. Do not test their memory! Haina maana.

3. Mkazo Katika Kiswahili na Kiingereza

Lugha ni changamoto kubwa na inaonekana kuna uzembe wa namna ya kufundisha. Kuna watu wanafika mpaka university hawawezi kuandika wala kuongea Kiswahili kinachoeleweka. Kiingereza ni utata zaidi.

Kwa dunia ya leo, lugha ndio nyenzo ya survival. Tujikite kufundisha stadi za lugha mashuleni. Language is of essence.

Tofauti na hapo tutaandaa wanafunzi wasioweza hata kufikiri.

4. Masomo ya stadi za kujieleza yawekwe

Ukimsikiliza mtoto wa kizungu wa darasa la pili utagundua ana uwezo wa kujieleza kuliko PhD holder wa Tanzania.

Unaweza kuwa unajua mengi sana, lakini kama huwezi kujieleza utaishia kuonekana mjinga sana. Ndio maana wakenya wengi wanatupiku fursa nyingi za ajira.

Tofauti na uwezo wao la lugha, lakini ni watu waliojengwa katika kujiamini na kujieleza.

Teach students how to articulate themselves and be CONFIDENT. Huko mashuleni watoto wanakuwa abused hawaruhusiwi hata kujieleza. Wanatandikwa viboko tu.

Wanafunzi wafunzwe kujieleza na kujiamini. Ni bora zaidi kuliko kukariri principles za sijui newton law of motion.

5. Vitabu vya nyambari nyangwine vipigwe marufuku pamoja na past papers

Haya ndio hatari zaidi. Yanawafanya wanafunzi kuwa makasuku. Wanakariri tu mambo wasiyoyaelewa mradi wamefaulu mitihani.

Forced labour, land alienation, low WAGES. HAPANA. THAT'S NONSENSE.

6. Specialization ianze kidato cha kwanza kwenda juu

Wanafunzi wapewe maeneo yao ya kitaaluma. Wasilazimishwe kusoma kila kitu.

Hii ikianza kidato cha kwanza kwenda juu inaweza kuleta matokeo chanya. Basics za engeneering, ufundi umeme, civil engeneering, languages, ufundi mbali mbali, basics za kilimo cha kisasa, nk. Believe me, this will work out 100% perfect!

Na haya yote sio lazima yawe technical mathematics or technical physics. Tunahitaji ujuzi sio kukariri principles za hisabati.

Sio lazima watu wasome majitu meeengiii...halafu wote wanaishia kuwa wakosa ajira!

MUHIMU NA LA MWISHO, Punguzeni unnecessary contents kwenye masomo. Kuna matakataka mengi mno yaliyoko kwenye silabasi.

Ubora wa elimu sio kukariri miaka ya wafu na majina ya wagunduzi wa milima.

Jioni njema!
 
Wale mnaokula tunda la masihara tunaomba juhudi zenu zielekezwe na huku kwenye mambo ya msingi!
 
Umeongea vyema mkuu, kuna siku tuliwahi kushirikishwa kama wadau wa elimu tukatoa maoni yetu tulichoambiwa ni kuwa serikali inajua fika kuwa mtaala uliopo si rafiki wa mazingira tulionayo but gharama hizo serikali haina. Nilibaki kucheka tuu
.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
5. ''Vitabu vya nyambari nyangwine vipigwe marufuku pamoja na past papers''

Kwanza nashukuru kwa maoni yako mazuri kabisa kuhusu elimu yetu

Maomba nichangie kuhusu hoja yako namba tano, umesema vitabu hivi vipigwe marufuku na past paper hapa ndo umekosea,

Asikudanganye mtu matokeo makubwa unayosikia kuhusu kuongezeka kwa ufaulu umechangiwa na huyu Nyangweni, nilipokuwa chuo kuna mhadhiri mmoja alikuwa anaponda sana vitabu hivi kuwa vimetuharibu lakini cha ajabu anaishia kukosoa tu bila kuja hata na pamphlet itakayosimama kama mbadala,yeye ni kuponda tu sijajua shida iko wapi, yaani hata walimu wengi sana vimesaidia vitabu vyake, na ukifuatilia kuna baadhi ya mambo kajitahidi sana kuyaandika ambapo hakuna / ni vitabu vichache mno vimeandika.

Tuacheni kulaumu, tunapaswa kupongeza kwa juhudi za wenzetu then tukosoe,leo hii naweza kukuuliza kwa baadhi ya masomo unitajie vitabu vilivyoandika topics kadhaa sure hutakuja na jibu lakn Nyangwine kaandika,mbaya zaidi hata walimu baadhi wanaviponda sana wakati kila siku huingia navyo darasani kusaidia kukaririsha watoto, kosoa then njoo na kitabu chako!

Kwani ni gharama kiasi gani zinazohitajika? How much money!? Bilioni ngapi zinazohitajika ambazo serikali haina?

This is a joke!
 
5. ''Vitabu vya nyambari nyangwine vipigwe marufuku pamoja na past papers''

Kwanza nashukuru kwa maoni yako mazuri kabisa kuhusu elimu yetu

Maomba nichangie kuhusu hoja yako namba tano, umesema vitabu hivi vipigwe marufuku na past paper hapa ndo umekosea,

Asikudanganye mtu matokeo makubwa unayosikia kuhusu kuongezeka kwa ufaulu umechangiwa na huyu Nyangweni, nilipokuwa chuo kuna mhadhiri mmoja alikuwa anaponda sana vitabu hivi kuwa vimetuharibu lakini cha ajabu anaishia kukosoa tu bila kuja hata na pamphlet itakayosimama kama mbadala,yeye ni kuponda tu sijajua shida iko wapi, yaani hata walimu wengi sana vimesaidia vitabu vyake, na ukifuatilia kuna baadhi ya mambo kajitahidi sana kuyaandika ambapo hakuna / ni vitabu vichache mno vimeandika.

Tuacheni kulaumu, tunapaswa kupongeza kwa juhudi za wenzetu then tukosoe,leo hii naweza kukuuliza kwa baadhi ya masomo unitajie vitabu vilivyoandika topics kadhaa sure hutakuja na jibu lakn Nyangwine kaandika,mbaya zaidi hata walimu baadhi wanaviponda sana wakati kila siku huingia navyo darasani kusaidia kukaririsha watoto, kosoa then njoo na kitabu chako!

Sent using Jamii Forums mobile app
Shida yangu ni huo ukasuku uliomo kwenye vitabu vya Nyambari nyangwine!

Kila kitu forced labour, land alienation, poor infrastructure.....

Hiyo ndiyo elimu? Huko ndiko kufundisha wanafunzi namna ya kufikiri na kupambana na mazingira yao?

Huu ni utani!
 
Lucas philipo, Na vitabu vyake kwa kiasi kikubwa ni ufupisho wa ma volume ya vitabu vya serikali. Kajitahidi kufupisha na kuongeza maudhui yasiyokuwemo kwenye vitabu vya serikali. Watumiaji ndiyo hawajielewi.
Hapana. Nyambari hatengenezi summary. Anatengeneza ukasuku!

We need to teach basics, lakini sio huo ukasuku.

Wanafunzi wanapaswa kufundishwa namna ya kufikiri na kuwa na utambuzi badala ya kulishwa points!
 
Mimi naishangaa sana serikali ukigusia habari ya kubadili mitaala wao wanakimbilia kusema ni gharama na hawaweki waz gharama hizo n kiasi gani

Kwa hyo wapo radhi kuona elimu yetu ikiharibika kwakisingizio cha gharama ? watoto wao ndio wanaandaliwa kuwa watawala sisi huku tunaosomesha watoto wetu kwenye mitaala mibovu tutawaliwe milele na watoto wao

Tunahitaji sana mjadala wakitaifa kwakwel tikiwachekea watawala wetu tutaishi kilalamika milele huku wao wakipeleka watoto wao mitaala ya Cambridge na mingine yenye ubora

Bunge LA katiba limetumia mabilioni ya pesa na walichokifanya had Leo hatukijui lakn serikal haijasema kama walitumia pesa vbaya

Lakn kuhusu kubadili mitaala kwao n tatzo wanaliona. Majuzi baadhi ya wastaafu baada ya kushiba tena walishika madaraka ya juu Leo wanajidai kusema eti ooo mitaala ya elimu yetu haifai mbona waliokuwa madarakan kelele hzi zilipigwa na waliweza kichukua hatua lakn hawakufanya haya ? Kuna mambo yanakera had basi tumewaacha wanasiasa watuamulie hadi kwenye taaluma yetu matokeo yake ndyo haya

Hizo gharama ni shilingi ngapi?

Ama kisingizio tu?
 
-matumizi ya kompyuta yaanze kufundishwa shule za msingi. Huwezi amini kuna walimu wengi tu wenye shahada hawajui kutumia kompyuta.

-Alama za barabarani na sheria zake zianze kufundishwa shule za msingi ili kuwa na kizazi kilichostaarabika.
Tanzania madereva ndiyo wanafundishwa haya mambo.

-matumizi ya kengele yaondolewe, kengele igongwe kama kuna dharura tu! Watoto waandaliwe kujiongoza kufuata ratiba na kutunza muda.

Watanzania wengi kushindwa kuendana na muda, kwa kiasi kikubwa imetokana na kutegemea kengele mashuleni (hili nililichunguza muda mrefu kwa rika nililosoma nalo).

Ninayo mengi ya kueleza ila ngoja niishie hapa!!
Asante sana mleta mada.
 
KAtika kusoma kwangu sijawahi support au kuhangika na past papers. Ya nn na ina umuhimu gani. huwa nataka nikutane na swali ambalo me nitaliona ni jipya kwangu no matter what wenzangu wamelisolve na wanajua lilitoka mara ngapi huko nyuma.
Past papers kwangu sijazielewaga kwa kweli
 
Asante sana.
 
We mtoa mada unakosea elimu hii haipo kwa bahati mbaya, ukitaka kutawala milele taifa chezea elimu, Kama uelewi Soma nakala ya nyerere "EDUCATION FOR SELF RELIANCE",
 
Topic hii ni nzuri mkuu…

Sina la kuongeza, ulitoa hii 2020 sasa serikali imebadilika labda watakusikia,,,

Binafsi nadhani nimekariri kote huko Hata secondary, tatizo ukienda vyuo Vikuu vingine kama nje ya nchi lazima u struggle masomo manake hakuna kukariri ni kujieleza iwe coursework, presentations etc, sasa utoe presentation mbele ya watu 100 kwa kingereza,na wakati hujajengewa uwezo huo tangia utotoni ni ngumu.

Nimeona Hata vitoto vidogo vinaanza kujengewa uwezo kwenye play, kunakuwa na role play, sisi sijui tunakwama wapi…

Binafsi niliona mahali silaha utakayoweza kumpa mwanao ni KUJIAMINI , Sio fedha, wala elimu wala nini 🤣🤣🤣🤣, mtu akijiamini anakua tayari na challenges zozote, anakuwa mthubutu etc…. Hivyo mitaala ilenge kujenga watoto wanaojiamini, abuse mashuleni itolewe, uwezo wa kujieleza na kutafuta maarifa wenyewe ndivyo vitiliwe mkazo…

Sijui nilitaka kusema nini,,,,, hivyo hivyo 🤣🤣🤣
 
Umeongea vyema mkuu, kuna siku tuliwahi kushirikishwa kama wadau wa elimu tukatoa maoni yetu tulichoambiwa ni kuwa serikali inajua fika kuwa mtaala uliopo si rafiki wa mazingira tulionayo but gharama hizo serikali haina. Nilibaki kucheka tuu
.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mngewauliza kulikuwa na u lazima Gani wa kutoa hayo maoni yenu kama Haina fedha!!!???

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapana. Nyambari hatengenezi summary. Anatengeneza ukasuku!

We need to teach basics, lakini sio huo ukasuku.

Wanafunzi wanapaswa kufundishwa namna ya kufikiri na kuwa na utambuzi badala ya kulishwa points!
anatengeneza vitabu kutokana na mfumo wetu w kukariri tu ufaulu mtihani,Yuko sahihi,Tanzania hii jifanye kutengeneza concepts utafail paper.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom