Kamakabuzi
JF-Expert Member
- Dec 3, 2007
- 2,861
- 1,302
Suala hili ni pana sana.MAPARACHICHI YA TANZANIA YANAVYOUZWA NJE YA NCHI KWA KUPEWA URAIA MPYA
Si hivyo tu, bali wafanyabiashara nchini Tanzania wamekuwa wakiyauza bei kubwa maparachichi bora yaliyozalishwa nchini kwa kuwadanganya raia kwamba eti maparachichi hayo yanatoka Burundi.
Hali hiyo, haijaishia kwenye parachichi tu, ukitembea kwenye Soko la Sabasaba jijini Dodoma hususan kwenye majengo mazuri, utajionea mchele mzuri wa Tanzania umeandikwa Mchele wa Zambia.
Jambo jingine, Njombe imekuwa ikizalisha matofaha (apples/peasi) bora katika miaka ya hivi karibuni lakini wafanyabiashara huyachukuwa yale yenye ubora mkubwa na kuyaweka stickers kisha huzichanganya na apples zinazotoka Afrika Kusini na kuyauza matunda hayo kwa Watanzania kwa bei kubwa. Kwa wastani apple kubwa lenye ubora mkubwa linatoka katika mkoa Mkoa wa Njombe huuzwa kwa shilingi 300-500 lakini wafanyabiashara wakishayachanganya na apples za S.A huyauza kwa shilingi 1000.
Patrick Sanga,
Mkulima, Njombe
Kwanza ni ile tabia ya watu hasa sisi Watanzania kupenda vitu vya nje yaani mind zetu zinaamini kuwa kinachotoka nje ndicho bora. Mtu tena Mtanzania anaenda supermarket anatafuta nyanya kutoka south Africa, akiona za Tanzania hata kama ni nzuri, lile neno kuwa ni za Tanzania linamfanya azione kuwa ni inferior, kwa hiyo mjasiriamali mzuri anakuja na market strategy - chukua mali ya Tanzania ipe label ya SA, the unafanya mauzo ya kutosha tena kwa bei kubwa (hiyo ndiyo hoja ya pili)
Ni kweli kimataifa haileti picha nzuri maana inaonekana kana kwamba Tanzania hatuzalishi kilicho bora, lakini kwa upande mwingine kwa kuwa kinachouzwa bado ni kile kilichozalishwa Tanzania, na kama ni mazao ya kilimo basi mkulima ananufaika