GREENGUARD MUNGIKI ya CCM waende wakarekebishe hayo yote walioyaanzisha wenyewe Igunga.
Nilitoa onyo kwamba hiyo siasa ya utekaji, kufyatu mirisasi ovyo vijijini, kumwagia watu tindikali na kusingizia wengine, kubaka wake za watu, kuchoma nyumba CCM washikawaafundisha vijana wao kuwa ndio njia sahihi na ya kileo zaidi basi tujue kwamba huyo mtoto hatoishia na madhambi haya kwa hicho kipindi kimoja tu bali hiyo dhambi itatuchukua zaidi ya karne kuifuta - vijana hao haramu wa CCM mwisho wa siku watamalizia kabisa biashara kwa kuelekeza hayo madhambi yote kwa chama chao wenye huko mbele ya safari.
Vijana magaidi jinsi uwaleavyo ndivyo wakuavyo, CCM mjue uhasama wa Igunga si jambo la utani hata kidogo; na mbegu hiyo itasambaa kwingineko kwa wale wenye ndugu zao mliowachomea nyumba, kubaka ndugu za, na kuwakata mapanga.
Taasisi za haki za binadamu bila shaka hivi sasa watakua wanakaribia kuweka kituo ukurasa wa mwisho kwenye ripoti zao. Na hilo nalo ni mtihani mpya kwa dhana ya utawala bora nchini na uwezo wa kuendesha FREE AND FAIR ELECTIONS katika zama za vyama vingi nchin.