Mapambano baina ya Wamasai na Wanakijiji

Mapambano baina ya Wamasai na Wanakijiji

Kimbori

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
6,618
Reaction score
5,407
Nimepata habari kutoka kwa watu wa karibu ya kwamba kuna mapigano yanaendelea kati ya Wamasi (wafugaji) na Wanakijiji katika kijiji cha Kisangesangeni, Kata ya Kahe, Wilayani Moshi Vijijini - Kilimanjaro.
Chanzo cha vurugu ni kitendo cha Wamasai kulisha mifugo (ng'ombe) kwenye mashamba na mazao ya Wanakijiji. Wamasai waliingiza ng'ombe baada ya kudai kupata kibali kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho kwa kulipa fedha. Wafugaji hao wamegoma kuondoka wakitaka warudishiwe hela, ambayo haijulikani ni kiasi gani au waruhusiwe kulisha mifugo katika eneo hilo mpaka mwisho wa mwaka kadiri ya makubaliano yatakapokoma. Pamoja na kuwepo kwa vurugu na uongozi kupewa taarifa, bado uongozi wa Kijiji haujaingilia kati ili kusuluhisha, hivyo kuwaweka Wanakiji katika hali ya taharuki.
Idadi ya mali iliyoharibiwa na wanakijiji waliojeruhiwa na kupelekwa hosptali bado haijatambulika.
 
Back
Top Bottom