Mapacha watatu wapata pa kukimbilia endapo watafukuzwa CCM

The Emils

JF-Expert Member
Apr 16, 2011
568
124
CCM ikiwatimua mapacha watatu tutawapokea-AFP Thursday, June 16,

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar CHAMA cha Wakulima Tanzania (AFP), kimeweka bayana msimamo wake kuwa ikiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kitaamua kuwafukuza mapacha wake watatu, chenyewe kitawapokea
na kumteua Edward Lowassa kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika
uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Mwenyekiti wa Taifa wa AFP, Said Soud Said ameiambia RAI wiki hii katika mahojiano maalumu yaliyofanyika katika eneo la Forodhani kwenye Ukumbi wa Ngome Kongwe mjini hapa.

Said amesema kimsingi CCM inajaribu kutaka kukamata kaa la moto kiganjani na hilo ni jambo la hatari kwao ikiwa itaamua na kuazimia kuwatimua mapacha hao watatu bila ya kupima upepo ulivyo.

Alisema mapacha hao wana haiba, mvuto na nguvu ya ushawishi wa
kisiasa kwa jinsi wanavyokubalika ndani ya umma hivyo chama chake hakitasita kuwapokea na kuwakaribisha kina Andrew Chenge, Rostam Aziz na Lowassa ili kuwa
wanachama wake wapya.

Tutawapokea kwa nderemo, shangwe, vifijo na hoihoi, hawa ni raia wenzetu, si wahamiaji wa nchi hii, tunaamini ni wasafi, waadilifu na wachapakazi hodari ila mbinu chafu za kisiasa zinawapaka matope wasitamanike kwa utashi wa maadui wao, alisema.

Mwenyekiti huyo wa AFP amesema
Lowassa ni tajiri mno katika siasa za
Tanzania asiyelingana na mwanasiasa
yeyote hasa katika kufikia kwake uamuzi wa kujiuzulu uwaziri mkuu na
kukaa pembeni ili kuipisha Kamati ya Bunge la Tisa ifanye kazi yake kwa
uwazi na hatimaye kubaini ukweli juu
ya sakata hilo ambapo yeye ilibainika
hakuhusika.

Nakuuliza mwandishi ni mwanasiasa yupi ndani au nje ya Serikali ya CCM aliyethubutu kufikia uamuzi uliofanywa na Lowassa, viongozi wengi wameboranga lakini wamebaki kuwa vinganganizi wa madaraka. CCM kabla ya kufikia hatma ya jambo hilo kwanza itafakari kwa kina athari na faida kabla ya kupitisha uamuzi huo wenye majuto kwao, alisema Said.

Anaongeza: Tuhuma pekee haitoshi kusimama kama ushahidi kamili na kufikia kuwaita au kumwita mtu fulani ni fisadi, makosa ya jinai, madai au mauajia yanahitaji ithbati ya vyombo vya kisheria hasa mhimili wa
mahakama.

Huu unaotaka kufanywa na CCM ni uonevu na ukatili usiostahili kwa raia yeyote kufanyiwa. Alipoulizwa ikiwa AFP na wanachama wake hawaogopi kuwapokea watu hao wanaoshukiwa kuwa kujihusisha na ufisadi, Said alisema hiyo ni hadithi ya kupika na hekaya ya kutengeneza ili kuwatia madoa ambayo kwayo hayana ukweli na ushahidi kamilifu.

Alisema ikiwa CCM itaamua kuwafukuza wanachama hao
wanotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya ufisadi vya kufikirika chama basi hicho chote kitamalizika kwa kuwa idadi kubwa ya wanachama na viongozi wake wana utajiri usioelezeka kwa namna walivyoupata.

Namkaribisha sana Lowassa na mapacha wake kwa mikono miwili
kuhamia AFP, waje haraka, hatutasita
kumtangaza Lowassa kama mgombea
wetu wa urais mwaka 2015, naamini
atashinda kwa kishindo na ndiye Rais
ajaye mwaka 2015 Tanzania, aliongeza Said.

Aidha, mwenyekiti huyo aliongeza
kusema kuwa watu wanaotuhumu
kwamba viongozi hao ni mafisadi
hawaelezi kwa yakini kile walichofisidi
wametenda kosa lipi ila mbio za urais
bila shaka ndizo zinazowagharimu na hasa Lowassa.

Alisema uwezo wa Lowassa ni
mkubwa na umeonekana wakati
akiwa Waziri Mkuu na kwamba rekodi
yake bado haijafikiwa na kiongozi
yeyote kati ya walioteuliwa na Rais
Jakaya Kikwete katika awamu ya nne. Huyu anafanana na Jacob Zuma wa ANC nchini Afrika Kusini.

Rais Jakaya Kikwete kama anapuuza nguvu za Lowassa kisiasa akubali kufanya mabadiliko ya katiba ya CCM kisha Lowassa, Fredrick Sumaye, John
Malecela na Rais Kikwete wagombee nafasi ya uenyekiti kama Lowassa
hakuibuka kidedea, alisema.

Rais Zuma aliwahi kumbwaga Thabo
Mbeki wakati akiwa madarakani na
yeye kuwa Rais wa ANC huku baada
ya kumshinda katika uchaguzi mkuu
uliokuwa na mbinde huko Polukwane
Afrika Kusini huku akiandamwa na kashfa za uuzaji wa silaha, rushwa na
ubakaji.

Habari zidi zinaeleza kuwa tayari Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania
Bara, Pius Msekwa amekutana kwa nyakati tofauti na wajumbe hao watatu wa NEC ya CCM katika Ofisi Ndogo ya CCM Lumumba huku Lowassa akisisitiza msimamo wake kuwa hajatenda kosa na hastahili kusulubiwa.

Tarifa zaidi zinasema kuwa Msekwa
alimweleza Lowassa na kumtaka aachane na mbio za urais lakini hata hivyo akashindwa kueleza sababu za kumkataza ambapo Lowassa alisema si dhambi ikiwa anataka kufanya hivyo ashinikizwe kuacha kutimiza haki yake ya kikatiba na kidemokrasia.

Hata hivyo, Mwenyekiti huyo wa AFP Said alisisitiza kuwa yeye na chama chake wanauelewa uthubutu, ubunifu na uhodari wa kupanga mikakati alionao Lowassa na wenzake katika kuhamasisha dhana ya maendeleo hivyo wakiamua kuhamia AFP itakuwa ni kama kuramba raha ya ushindi.
 
yaani ni sawa sawa na mchezaji kutoka English premier league na kuhamia ligi kuu ya vodacom Tanzania, au messi kuhamia timu ya Manyema we unategemea nini!?
 
hata cuf,tlp,udp watapokelewa ika hawatoki ccm wale yale ni maamuzi ya muendelezo wa ulopokaji
 
Sasa'vi CCM ni kama mfa maji anayetapatapa majini, kuendekea kuwaenzi mapacha watatu au kuwafukuza achilia mbali kuwapa onyokali imekwisha poteza kabisa mvuto wake kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom