Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Wahenga wanasema maajabu hayatoka, yataendelea kutokea. Tofauti na mapacha walioripotiwa katika kisa fulani ambapo mmoja wao alimuua mwenzake baada ya kuangukia katika penzi la mwanaume mmoja na mmoja wao tu kubahatika kuolewa na mwanaume huyo, mapacha wawili katika kisa hiki wamekubaliana kuchangia penzi la mwanaume mmoja bila ugomvi wowote.
Mapacha hao kutoka Afrika Kusini wamekubali kuolewa naye baada ya kuafikiana na maombi yao, na kwa kuwa ndoa za wake wengi zimeruhusiwa nchini mwao, ndoa hiyo ilifanyika kwa uwazi na kwa shamrashamra kubwa.
Kwa mujibu wa jarida la The Drum, kwa mapacha hao Owami na Olwethu Mzazi, ilikuwa ndoto yao ya muda mrefu kuolewa na mwanaume mmoja. Walieleza kuwa tokea utotoni walishirikiana kila kitu, waliosha vyombo, walicheza na kwenda shule pamoja. Na hata walioga pamoja.
Pacha mmoja, Owami, ameliambia jarida hilo:
“Siku zote tumefanya mambo pamoja… hivyo ndivyo tulivyolelewa na bibi yetu. Hivyo, tulipoamua kuolewa, tulisema kuwa mwanaume yeyote anayetaka kumuoa mmoja wetu, atamuoa mwingine pia.