Maonyesho ya burudani na michezo ya kielektroniki.E3

Maonyesho ya burudani na michezo ya kielektroniki.E3

Rog chimera

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2018
Posts
428
Reaction score
766
B0172A37-0C07-4F26-A22A-2803D1BC21E6.jpeg
1248C025-8974-4561-897A-9F3CB5C4DA8C.jpeg
7DDDD005-40AA-4A42-9FCD-8CCDD15179BE.jpeg
E3 ( electronic entertainment expo).ni maonyesho makubwa kabisa duniani kwa ajili ya burudani na michezo ya kielektroniki ( computer and console games).Maonyesho haya hufanyika kila baada ya takriban mwaka mmoja na hutumiwa na kampuni mbalimbali kam EA ,Bethsda,Sucker punch, Square Enix na nyingine nyingi zinazotengeneza michezo hiyo ( game developers and publishers) pamoja na kampuni zinazotengeneza vifaa vya kielektroniki vinavyotumika kuendesha michezo hiyo kama vile Microsoft, Sony, Nintendo n.k kuzindua na kutangaza michezo mipya, maboresho ya michezo iliyokwisha ingia sokoni pamoja na vifaa vya kielectroniki (hardware) vinavyotumika kuendesha michezo hiyo kwa wafanyabiashara na wapenzi wa michezo hiyo.Maonyesho ya mwisho yalifanyika mwezi June mwaka huu na michezo mingi ilizinduliwa na na taarifa mbali mbali kuhusiana na michezo hiyo zilitolewa. Hii ni sehemu ya kwanza ya makala hii sehemu ya pili itaelezea kwa kina michezo hiyo kulingana na makundi iliyomo . Karibu na Endelea kufuatilia makala hii.



Sehemu ya pili
Electronics Arts .EA. Na ushiriki wake E3 2018.
Kampuni ya EA ni moja ya makampuni makubwa duniani inayoshughulika na utengenezaji wa michezo ya ki eleckroniki na michezo yake maarufu ni kama Battlefield series, FiFa, Need for Speed, Madden NFL na kadhalika.

Katika maonyesho ya mwaka huu ya E3 EA ilizindua michezo ifiatayo:


FIFA 19.
FiFa 19 ni muendelezo wa mfululizo wa mchezo wa ki elektroniki wa mpira wa miguu toka mwaka 1993.Mchezo huu utakua sokoni kuanzia tarehe 28 mwezi September 2018 na utakua umefanyiwa mabadiliko kidogo ukilinganisha na ule wa 2018 FiFa 18 kama ifuatavyo:
Kuhusisha ligi ya Mabingwa Ulaya- kufuatia Kufikia tamati kwa mkataba wa haki miliki baina ya kampuni ya konami inayotengeneza mchezo kama huo wa mpira unaofahamika kama pro evolution soccer( PES )na mamlaka ya Mchezo wa Soka wa Uhalisia Barani Ulaya( UEFA), kampuni ya EA imejinyakulia fursa hiyo kwa kuingia mkataba na UEFA na kujipatia haki miliki za kutumia majina ya wachezaji na waamuzi, viwanja vya mpira , na maudhui mengine kama yanavyoonekana katika mashindano halisi ya ligi ya mabingwa barani ulaya.

Matumizi ya Mabadiliko ya hali ya hewa-injini ya frostbite ambayo ndio hutumika kuendesha michezo ya EA imekua ikiwezesha mabadiliko ya hali ya hewa ndani ya michezo hiyo ya ki elektroniki kubadili mfumo na matokeo ya uchezaji wa michezo hiyo kwa kuleta athari mbali mbali( ndani ya mchezo), kwa mfano, katika mchezo wa EA. wa vita wa Battlefield 1kwa kutumia silaha kama bunduki, injini ya frostbite imewezesha mabadiliko ya hali ya hewa ndani ya mchezo kama vile kutokea kwa upepo au mvua kumfanya mchezeshaji wa mchezo kupata tabu kulenga shabaha kwa ufasaha ,kurusha na kuongoza ndege za vita na kadhalika ili kuzidi kujenga na kuimarisha uhalisia wa mchezo.

Uwezo huu wa injini ya frostbite kuleta mabadiliko katika mfumo mzima wa uchezaji wa mchezo na matokeo yake ulikua bado haujawezeshwa kwenye mfululizo wa michezo hii wa miaka ya nyuma kama FIFA 18 na utaanza rasmi kwa FIFA 19.hali ya hewa ndani ya mchezo kama mvua na upepo na jua utaleta mabadiliko ya mfumo wa michezo na kuleta athari kama vile kuteleza kwa wachezaji wakati wa mvua, Upigaji wa pasi usio wa ufasaha na kuwahi kuchoka kwa wachezaji wakati wa jua.

Sehemu ijayo itaendelea kwa kuelezea mabadiliko mengine yatakayokuepo katika mchezo wa EA wa FIFA 19 na taarifa mbali mbali kisha kuzama katika michezo mingine iliyotambulishwa na EA katika E3 mnamo juni 12-14 mwaka huu. Endelea kufuatilia.
 

Attachments

  • 283D51E4-C924-4481-97D9-3C316F54926D.jpeg
    283D51E4-C924-4481-97D9-3C316F54926D.jpeg
    22.3 KB · Views: 95
  • 76DAF3F8-1D08-4605-9158-3861E9DF2A2F.jpeg
    76DAF3F8-1D08-4605-9158-3861E9DF2A2F.jpeg
    21.4 KB · Views: 102
Ingekuwa bongo hapa,nisingekosa aisee
 
Mkuu Alichosema Wa Hapo Juu Nimesema Na Mimi
 
Dah naona konami tena hakutakuwa na uefa kwenye pes.


Halaf jamaa zangu ubisoft vipi?
 
Mkuu inaonekana unapenda sana games hivi hii buzness ya game center kuna dogo anataka kuifanya ila nna waswas serekali za mitaa watamzingua, naogopa kumpa mtaji ukapotee huko
Fungua tu haina shida. Mbaya ni sare za shule kuingia kwenye biashara nadhani.
 
Daa wakuu ivi cd za ps 4 bei gani na je inawezekana kuweka games katika hdd ya ps4
 
Back
Top Bottom