Maoni yatolewayo na wanasiasa wajulikanao hapa JF yalindwe vipi?

Kichuguu

Platinum Member
Oct 11, 2006
15,589
19,486
Ndugu wanaJF, najua mada hii siyo siasa lakini bado ina maudhui ya siasa, hivyo nimeamua kuiweka hapa badala ya kuipeleka kule kwenye hoja mchanyiko au kwenye udaku.

Nitatoa background information ambayo ineonekana kuwa ndefu kidogo kwa sababu sipendi kufupisha quotes ninazofanya hapa ili kuepusha lile ninalotaka kuongelea, yaani upotoshaji wa post za wachangiaji mbalimbali. Msomaji anaweza kurukia moja kwa moja kwenye paragraph ya mwisho iliyo katika herufi nzito na kuepuka kusoma hii background information iliyoko katikati.


Kule Google Groups kuna discussion group ya Watanzania ijulikanayo kama wanabidii na website yao ni wanabidii.net. kwa wale wasioifahamu discussion group ile ni kwamba inajadili mada moto moto za kisiasa kama hii JF. Ila wachangiaji wengi pale wanatumia majina yao moja kwa moja badala ya aliases. Kinachonifanya niandike hapa ni kuhusiana na mjadala wa juzi uliofanyika pale ukiwa na kichwa cha habari kisemacho "Nionavyo Mimi....Uchaguzi wa Rais na wabunge vitenganishwe." Ingawa sikuomba wahusika ruhusa kutumia mjadala ule hapa JF, hata hivyo nitachomoa posts zilivyokuwa bila kuzifanyia editing yoyote ili kuzia nisipotoshe nia za wachangiaji wale. Katika mjadala huo niliotaja hapo juu, Mheshimwa Zitto alitoa maoni yake kama ifuatavyo

baadaye mcahangiaji Lingsona akajibu Zito ifuatavyo
Zito naye akajibu ifuatavyo

Jambo la kushangaza, ni kuwa gazeti la Tanzania Daima limetumia mjadala ule na kuandika habari yenye kichwa cha habari kisemacho

"Zitto: JK aongezewe Muda"

katika habari ile siyo tu kuwa mwandishi alipotosha mchango uliokuwa umetolewa na Zitto pale wanabidii.net, bali pia alitumia habari ile bila kuomba kibali cha Zitto mwenyewe au kwa moderator wa Wanabidii.net unless kama yeye mwenywe mwandishi ndiye moderator. Kitendo kile kimafnaya Zitto atangaze kujitoa katika group ile, na mpaka sasa ninapoandika bado wanajadiliana na kumwomba Zitto afikirie tena uamuzi wake. Kilichionishangaza ni pale mhariri wa Tanzania Daima bwana Absalom Kibanda (ambaye pia ni mwanachama wa Wanabidii.net) aliposema kuwa hakubaliani na tafsiri ya mwandishi wake kuhusu maneno yaliyotolewa na Zito lakini bado akamlaumu Zito kwa kusababisha maneno yake yawe yatafsiriwe vibaya na yule mwandishi; hakujilaumu kama mhariri kuwa aliruhusu kuchapishwa kwa habari isiyothibitika!!! na mbaya zaidi kwa maoni yangu ni kuwa mhariri hakukubali hata kuomba radhi kutokana kosa la mwandishi wake, badala yake kumtaka Zito atoe maelezo ya kufafanua alikuwa na maana gani katika post ile kama nilvyoonyesha hapa chini

Mimi pamoja na kuwa sina elimu ya uandishi wa habari, nilisoma thread ile yote na kuona kuwa Zito alikuwa akitoa mawazo pana ambayo hayakuwa yanamhusu mwanasiasa yeyote specific, i.e. Kikwete kama ilivyoripotiwa na tanzania daima. Na alikuwa ni mchangiaji tu kama ambavyo huwa tunachangia hapa mada mbalimbali zinazoanzishwa na watu mbalimbali.


Baada ya kusoma hayo huko Wanabidii.net, nikastuka kidogo kuwa hata sisi tuna wanachama wanasiasa hapa JF ambao hutumia majina yao kutoa mada mbalimbali na wanaweza na kuja kujikuta katika hali kama iliyomkuta Zito: post zao zikachukuliwa out of context na kuwekwa kwenye headline za magazeti. Ingawa nimewahi kuona mada zinatolewa hapa na kuwekwa kwenye forum nyingine lakini sijawahi kuthibitisha posts za wachangiaji wetu zikipotoshwa huko nje.

Swali langu, je hapa JF tuna utaratibu gani wa kulinda michango original ya wanachama wetu (hasa wale wanaojulikana kwa majina yao halisi) isipotoshwe kwenye print media au kwa njia nyingine yoyote?

 
Sifikirii kama upo utaratibu wowote wa kulinda maandishi ya wanachama. Tatizo liko kwenye commitment kufanya hiyo kazi inachukua muda na pesa vile vile.
 
Zito alikuwa anatoa tu maoni yake, inahuzunisha sana hasa gazeti kama la Tanzania daima,

Zitto anaonekana kuyaingizia pesa magazeti mengi sana nchi hii, na mijadala mingi imekuwa kumwaribia yeye na kumuathiri kisaikolojia very same waandishi huwa tunawasifu wanafanya kazi vizuri

mtoa maada, kuzuia ni vigumu, because they can write in other language! wanachotaka wao ni pesa.

Kibanda unajua malengo yako, wewe ni mhariri wa hilo gazeti, tumeshakujua usipate shida sana kujitetea. wala kuandika lugha za kilaghai! Haujaanza leo na huyo mwandishi siyo mtoto !
 
Kwa nini yalindwe? Kwa nini watoa maoni wasisimamie maoni yao?

Omega Psi Phi? 'wewe ni mtu wa Kibanda nini', unaweza kutoa tafsiri sahihi ya neno aliloandika mtu pasipo kumuuliza??

Unaweza kucopy mananeo ya mtu, ukamchafua halafu ukarudi na kusema tulifikiri ulisema hivi???

Zito anailisha familia ya Kibanda, period! huo nao ni uanaume!

Umeona hiyo sentensi ya kwanza niliyoibold? imekaa sawa? iko wrong, siwezi kabisa kukujudge na kutoa tamko kwa watu milioni 40 kwa sababu Omega umendika kitu ambacho nadhani kinaendana na ninavyofikiri mimi!! This is insane! you can feel that,
 
Kwa nini yalindwe? Kwa nini watoa maoni wasisimamie maoni yao?

Kumbuka kuwa forum siyo press conference; hivyo siyo mahali ambapo mchangiaji anatoa maoni ambayo yana-reflect msimamo wake rasmi wa kuweka kwenye headlines. Michango minine hutolewa kulingana na flow ya discussion; siyo vizuri ku-single out jibu la mchangiaji mmoja na kulifanya kuwa habari kamili bila ya kuonyesha jinsi gani maoni yake yalivyokuwa ana-interact na ya wachangiaji wengine. Kufanya hivyo ndiko kunakoweza kusababisha upotoshaji wa mawazo ya wachangiaji kama ilivyotokea kwenye hili la Tanzania Daima na Zito kama nilivyoeleza huko juu ambapo gazeti lilishindwa kuona kuwa maneno ya Zito waliyoquote yalikuwa ni generic kujibu swali la Lingason na wala hakuwa specific kuwa anataka sasa hivi JK aendelee kama walivyoripoti.
Tunaweza kuwa na utaratibu ambao mfano, 2014 tunafanya uchaguzi wa Vijiji,
Mitaa na Madiwani. 2015 Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na 2016 Uchaguzi Mkuu wa
Rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa tunaanzia watakaochaguliwa mwaka 2010.
 

Inaelekea kuna tatizo la waandishi wetu wa habari na lakini pia wanasiasa hao wanaweza kutumia luxury ya anonymity na kubandika kwa kutumia majina bandia.
 

- Mkuu Mwalimu Kichuguu, hiii habari yako haijakaa sawa hata kidogo!Halafu wewe unaheshimika sana hapa. Lakini please tizama hapa chini, huko majuu huyu Senator haya maneno hakuyasema kwenye pres. conference lakini yamenukuliwa na tayari ameomba msamaha badala ya kususa na kutafuta visingizio vya kitoto, siasa ni professional kama zingine, zina miiko yake na process zake pamoja na sheria zake, kama huziwezi kuzifuata ni vyema kujitoa na kwenda kwenye field nyingine, soma chini hapa:-



- Sasa Mwalimu, unaona hawa wenzetu wanakubali na kuungama bila visingizio kama sisi!
Huyu Reid hakusema kwenye pres. Conference kama unavyodai iwe ili kunukuliwa, ila kwa kuwa ni politician aliyefikia lelvel ya kuwa kazini kwa taifa 24/7 kila anachosema hata awe wapi ni msimamo wake kama a national politician na ndio maana hapo juu unaona mtumzima hajaleta maneno mengi amekuba rsponsibility na kubeba msalaba!

Respect.


FMEs!
 

- Mkuu Mwalimu Kichuguu, hiii habari yako haijakaa sawa hata kidogo!Halafu wewe unaheshimika sana hapa.


Respect.


FMEs!


Mkuu imekaa sawa kabisa labda kama unataka nifafanue zaidi.

Katika forum hii wakati mwingine tunajibizana kulingana na premises zilizoko mbele yetu, hasa waanzisha mada au waunganisha mada. Mara kadhaa tumwahi kuandika post ambazo baadaye tunagundua kuwa premises tulizoletewa mbele yetu hazikuwa sahihi. Ndiyo maana nasema majibu ya mchangiaji mmoja katika forum siyo rasmi ya kuchukuliwa na kuwekwa kwenye headlines unless kuna uhakika kuwa premise waliyotumia ni sahihi kabisa. Kuna haja ya kumuuliza mchangiaji hata kwa PM kabla hujaziandika gazetini hasa kama unataka kutumia jina lake moja kwa moja. Personally nimewahi kuombwa ruhusa na watu kadhaa kuthibitisha post zangu na kutoa ruhusu wazitumie katika articles zao, nina imani kuwa hata wewe FMEs umeshawai kuombwa kuthibitisha na kutoa ruhusa ya namna hiyo.

Jambo jingine ambalo ndilo kubwa nilioongea hapo juu ni hilo la kusingle out post ya mchangiaji mmoja bila kuangalia jinsi alivyointeract na wachangiaji wengine; hiyo ndiyo recipe kubwa ya distortion.
 

- Hivi Mwalimu how sure are you kwamba anayeshuika hakuombwa, pamoja na kwamba sio hoja ya smingi sana, kwani hapo juu huyo Reid wamemuomba? Kwani Tiger woods aliposema maneno yake na wale wanawake alikwua kwenye pres. conference mkuu, ndio maana ninasema habari yako haijakaa sawa hata kidogo na sina mpango wa kulumbana na wewe maana unaheshimika sana hapa,

- Binafsi ninaheshimu sana michango yako hapa, kwenye hizi ishu za quotation za politician ukijali jina hutaweza kua muandishi wa habari hata siku moja!

Respect.


FMEs!
 
Kichuguu hoja yako ipo sawa kabisa..sijui wengine wasichokuelewa ni nini?
Hii ni mara ya pili sasa waandishi wanakuja kuchota news ya mchangiaji mmoja tu kwa maslahi yao binafsi. Kipindi cha nyuma waliwai kuchukua news ya huyo uyo Zitto alipomtetea Dr Idrissa Rashidi. Nionavyo mimi ni muhimu utaratibu ufikiriwe wa kulinda wachangiaji na waandishi ushwara. Vinginevyo JF itakuja kukosa michango ya ndani ya wanasiasa hao. Wao ndio wanaoshiriki siasa-ni vizuri kupata michango yao. Vinginevyo tutaishia kupata michango ya security officers na wabeba mikoba ya wanasiasa ambayo imejaa udaku na sometime wanakuja na issues za kuwalinda babwana zao.
 

Nafakiri ukiangalia tena kwa kina utaona kuna tofauti kubwa sana baina ya case ya Reid na hii case ya mwandishi wa habari kuchagua post moja au mbili za mchangiaji na kuziweka kwenye headline kama habari kamili huku akiacha interaction ya post hizo na zile za wachangiaji wengine including qualifiers na premises zilizotumiwa na mchangiaji.

Case ya Reid ni habari kamili wakati hii iliyokopiwa kwenye forum siyo habari kamili unless waandishi waipindishe ili kuifanya iwe habari kamili kama walivyofanya, na ndiyo maana wakapotosha.

Kwa kurekebisha tu, nitakubaliana nawe kwa kufuta neno langu la "press conference," lakini hoja yangu kubwa inabaki pale pale kuwa wasichuke post moja na kuifanya habari kamili bila kuiunganisha na premises zake zote na vile vile kupata uthibitisho kutoka kwa mchangiaji. Inawezekana mchangiaji akawa anatoa vipande vipande kabla ya kuungnsiha, wewe mwenyewe FMES umewahi kutuwekea post za namna hiyo na kuacha kuwa tunakufuatilia kwa siku kadhaa hadi unapomaliza mada yako.
 

Mzee, hebu gngalia tena background information nilizotoa wakati nafungua mada kuhusu Zito kuombwa kuthibistiha habari ile.

Kuhusu case ya Reid habari kuu pale siyo ule ujumbe aliokuwa anataka kutuma bali uchaguzi wa maneno aliyotumia.

Kama reid angebadilisha maneno hayo akasema an "an eloquent African American" usingesikia habari hapo.

Case ya Tiger nayo huwezi kuiweka katika context ninayoongelea hapa.

Jambo kubwa hapa ni hizo dots kufanywa habari kamili kabla hujaziunganisha
 

- Muhimu ni kama amesema au hakusema, sijawahi kusikia Zitto akilalama kwamba hakusema, ila nimesikia akilalama kwamba aliyemnukuu hakuwa na nia njema, anyways sina mpango wa kulumbana na wewe na hii kesi maana kwangu ni black and white, either mwanasiasa amesema au hakusema, amesema wapi au amesema nini au kwa nini sio yote aliyosema siamini kwamba ni ishu, ila it is up you kuamini unavyotaka, sielewi mwanasiasa anavyoweza kuja hapa na ksuema maneno ambayo hayaamini just because sio pres. conference, sidhani kama tunahitaji wanasiasa wa namna hiyo bongo!

- Habari ikitolewa ana haki zote kisheria kusema hakusema na kuwafikisha wanaomtuhumu kwenye sheria. Anyways, thanks I am out maana tumeipitia hii ishu siku za nyuma sitaki kuirudia tena!

Respect.


FMEs!
 
siasa zimeingia stage tofauti nikiwa na maana sasa hivi siasa sio kwenye majukwaa, TV na redio pekee, bali pia online. Website ni vyombo vinavyoaminika kutoa habari. viongozi wanatumia you tube, face book, twitter n.k
mfano kwenye uchaguzi wa Irani viongozi walikuwa wanatumia twitter na facebook kutoa statement.
hamna ubaya wowote kwa mwandishi wa habari kum quote zitto, slaa, mnyika, mbowe, mo na wengine ambao wanatumia majina yao.
kama mtu ataki kuwa quoted then ujue huo mchango unawalakini

hata kama mtu ni security officer mchango wake utaeshimika kutokana na hoja yake lakini sio shughuli yake anayoifanya.
hayo mambo ya kulindana tena, tunarudi nyuma badal ya kwenda mbele
 
Nadhani kuna tatizo la kuelewana hapa tena, sidhani kama ni tatizo mtu kuwa quoted, mimi naona tatizo ni kupindisha ukweli wa kile alichosema huyo muhusika! That is the case kwa waaandishi wetu hapa Tz
 


(1) Mkuu wangu usiniangushe, hatulumbani. Ninachozungumza ni hii tabia ya waandishi kuchukua vipande vya posts na mwishowe kudistort intent ya mchangiaji wa forum. Kama umesikia Zito akilalama kuwa amenukuliwa vibaya basi ndiyo distortion yenyewe ninayoongea; isingekuwapo kama mwandishi angechukua effort ya kuwasiliana na Zito kabla ya kuweka p[ost hiyo kwenye headline.

(2) Nina imani kuwa wewe huko juu ya kuamini kwa mkato tu kuwa mwanasiasa kasema au hapana. Ni lazima unajua kuchukua habari kutoka pande zote mbili kama zipo na kuona kama yaliyosemwa kuhusu mwanasiasa huyo yana ukweli au vipi; ninakufahamu hivyo.


(3) Kilichonifanya niandike hii thread siyo swala la kumtetea mtu mmoja au vipi bali kuhusu health ya forum kama hii yetu. Endapo posts za wachangiaji wa namna hiyo zikindelea kuwa distorted na vyombo vya habari kuna hatari wote wataondoka na kama tunavyojua contribution za wanasiasa hawa kwenye forum hizi zimekuwa zinasaidia sana kwa namna mbalimbali. Hii siyo kwa Zito tu, leo hii tumeona jinsi informatio za Nape zilivyokuwa distorted hapa lakini mwenyewe akaja kuzisahihisha. Ninawaona watu wa aina hii kam hazina kubwa kwenye forum hii.


(4) kama jambo hili lilishajadiliwa, that is fine. I was just concerned kuliona kwa mara ya kwanza na ndiyo maana katika opening post yangu niliweka kama swali kwa vile sikuwa na uhakika kama liliwahi kujadiliwa au kuna utaratibu wowote wa kulinda post hizo.


(5) Kusubiri itokee distortion halafu wapelekane mahakamani ndilo jambo nililoongea kwenye aya namba (3) hapo juu.



Issue kubwa siyo kumlinda mtu asiwe quoted bali ninachotaka ni kuwa post za wachangiaji zisiwe damagingly distorted kwenye magazeti yetu.
 

Kwa mtazamo wangu,nadhani ni vyema watu tukawa careful in every sigle word we write here. Mantiki kwamba michango ichungwe au isiende magazetini haina tija. Kama mtu unaweza kuchangia JF au Forum yeyote basi ni dhahisi ungekuwa tayari kusema the same hata ungekutana na friends in the same non-official discussion pale manzese. Kwa sababu hiyo basi, tunachokisema ni kile tunachofikiria na kinabaki fact, ila tukumbuke "meaning of words are not in words but in people who uses the words". Mwandishi wa Tanzania daima yupo sawa.

Zitto ndugu yangu, kuliko kuhisi kila mtu anakufikiria vibaya, basi wewe SIMAMA NA USEME ULICHOMAANISHA SICHO and that is over kuliko kuendelea kuumia bure.

"Politics is a dirty game....play it careful"
 
Mwanasiasa anayo haki ya kutoa maoni yake juu ya jambo lolote na kutokana na utashi wake na kwa kufuata sheria zilizopo.


Hapa tatizo naweza sema lipo huku kwenye taaluma yenyewe ya uandishi wa habari, hasa kwa sababu kiwango cha waandishi wetu wanaopenda kucopy na kupaste habari kinaongezeka kwa kasi sana na kwa njia hii nchi kama nchi haiwezi kuendelea.

Tunahitaji kuwa na waandishi makini, sitegemei mwandishi wa habari anayeiheshimu na kuijua kazi yake akachukua mawazo ya mtu kutoka kwenye mitandao nakuyafanya kuwa ni habari sahii ya kuiandika na hasa bila kumuhoji muhusika/mchangiaji labda kama hilo ni gazeti la udaku.
Na kama ni gazeti la udaku basi sisi wasomaji tutaipokea habari hiyo kiudaku udaki hivyo tatizo naweza sema linaweza kutokuwepo.

Kwa kusema hayo, sioni haja ya kulinda maoni yatolewayo na wanasiasa wajulikano, tuwaweke huru waongee na wanahabari watusaidie kuheshimu sheria zilizopo na kufuata maadili ya kazi yao.

Nawakilisha


 

Nimeanza kuona ugumu wetu katika matumizi ya maneno. Wakati ni kweli kuwa kila mtu analoongea kwenye mtandao lazima litoke moyoni mwake na awe tayari kulisimamia, ndugu yangu unalokosea ni kuchukulia kuwa tunatetea maneno yaliyosemwa na Zito, hapana, tunachoongelea ni ule upindishaji wa yale yaliyosema na ZIto, na kuyachukulia nje kabisa ya mada. Nimekopi hapo ujuu posts zote zilizoandikwa na Zito kwenye forum ile: zilikuwa mbili tu. Hakuna hata moja iinayoonyesha kuwa Zito alisema JK aongezewe muda.

Inapotokea gazeti likaandika kuwa eti Zito alipokuwa kule JF alisema kuwa JK aongezewe muda, ni distrotion ambayo siyo tu inachafua jina la Zito bali pia credibility ya JF yenyewe. Maoni yangu ni kutaka posts za hapa JF zisiwe distorted kwenye media; wakiamua kuzitumia basi wazitumie kama zilivyotolewa na mchangiaji bila kuziwekea chumvi au pilipili yoyote. Sababu ya kuwataka wawasiliane na mchangiaji ni huko kutaka kuhakikisha kuwa wanajua fika kuwa wanalioandika linaendana na nia ya mchangiaji huyo siyo nia yao wenyewe. Ni posts chache sana kwenye forum ambazo ni standalone kwa nyingi hutolewa vikiwa ni vpande vipande vinavyoendana na mtililiko wa mjadala wenyewe, hivyo wakichukua vipande vichache tu inabidi wao ndio wawe waangalifuy siyo mchangiaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…