Kichuguu
Platinum Member
- Oct 11, 2006
- 15,555
- 19,430
Ndugu wanaJF, najua mada hii siyo siasa lakini bado ina maudhui ya siasa, hivyo nimeamua kuiweka hapa badala ya kuipeleka kule kwenye hoja mchanyiko au kwenye udaku.
Nitatoa background information ambayo ineonekana kuwa ndefu kidogo kwa sababu sipendi kufupisha quotes ninazofanya hapa ili kuepusha lile ninalotaka kuongelea, yaani upotoshaji wa post za wachangiaji mbalimbali. Msomaji anaweza kurukia moja kwa moja kwenye paragraph ya mwisho iliyo katika herufi nzito na kuepuka kusoma hii background information iliyoko katikati.
Kule Google Groups kuna discussion group ya Watanzania ijulikanayo kama wanabidii na website yao ni wanabidii.net. kwa wale wasioifahamu discussion group ile ni kwamba inajadili mada moto moto za kisiasa kama hii JF. Ila wachangiaji wengi pale wanatumia majina yao moja kwa moja badala ya aliases. Kinachonifanya niandike hapa ni kuhusiana na mjadala wa juzi uliofanyika pale ukiwa na kichwa cha habari kisemacho "Nionavyo Mimi....Uchaguzi wa Rais na wabunge vitenganishwe." Ingawa sikuomba wahusika ruhusa kutumia mjadala ule hapa JF, hata hivyo nitachomoa posts zilivyokuwa bila kuzifanyia editing yoyote ili kuzia nisipotoshe nia za wachangiaji wale. Katika mjadala huo niliotaja hapo juu, Mheshimwa Zitto alitoa maoni yake kama ifuatavyo
Nitatoa background information ambayo ineonekana kuwa ndefu kidogo kwa sababu sipendi kufupisha quotes ninazofanya hapa ili kuepusha lile ninalotaka kuongelea, yaani upotoshaji wa post za wachangiaji mbalimbali. Msomaji anaweza kurukia moja kwa moja kwenye paragraph ya mwisho iliyo katika herufi nzito na kuepuka kusoma hii background information iliyoko katikati.
Kule Google Groups kuna discussion group ya Watanzania ijulikanayo kama wanabidii na website yao ni wanabidii.net. kwa wale wasioifahamu discussion group ile ni kwamba inajadili mada moto moto za kisiasa kama hii JF. Ila wachangiaji wengi pale wanatumia majina yao moja kwa moja badala ya aliases. Kinachonifanya niandike hapa ni kuhusiana na mjadala wa juzi uliofanyika pale ukiwa na kichwa cha habari kisemacho "Nionavyo Mimi....Uchaguzi wa Rais na wabunge vitenganishwe." Ingawa sikuomba wahusika ruhusa kutumia mjadala ule hapa JF, hata hivyo nitachomoa posts zilivyokuwa bila kuzifanyia editing yoyote ili kuzia nisipotoshe nia za wachangiaji wale. Katika mjadala huo niliotaja hapo juu, Mheshimwa Zitto alitoa maoni yake kama ifuatavyo
baadaye mcahangiaji Lingsona akajibu Zito ifuatavyoHoja hii inaweza kuwa na maana sana ikijadiliwa kwa mapana yake. Nchi kadhaa Duniani zenye kufuata mfumo kama wetu mchanyato wa Rais na Waziri Mkuu mwenye madaraka kidogo wametengnisha Uchaguzi wa Rais na Wabunge. Rwanda, Rais anakaa Madarakani miaka 7 na anaweza kuoongeza mara moja na Bunge miaka 5. Hivyo hakuna kipindi ambacho kimoja kati ya Bunge na Urais havipo. Hii inatumika kwa nchi nyingi zilizokuwa chini ya Mfaransa. Marekani Useneta ni miaka 6, Ubunge miaka 2 na Urais miaka 4. katika uchaguzi ni nusu tu ya maseneta ndio huingia katika uchaguzi na hivyo Taasisi za taifa kuwepo muda wote licha ya kwamba kuna uchaguzi. Kila baada ya miaka 2 kuna uchaguzi Marekani ama wa wabunge, au rais au Maseneta. Mwaka 2008 katika uchaguzi
Mkuu wao walichagua nusu ya seneti na Rais. mwaka 2006 wakati democrats walipochukua Bunge na Pelosi kuwa Spika hapakuwa na Uchaguzi wa Urais.
Mfumo huu unahahakisha kuwa Dola ipo - Mihimili- muda wote kwa mbili kati ya taasisi kutokuwa katika ucahaguzi na kuondoa uncertainty zozote.
Mjadala kama huu Tanzania nina mashaka hautakuwa na tija kwani watanzania huwa tunajikuta tunajadili watu badala ya masuala. Hoja kama hii ni rahisi sana kwa wanasiasa kuonyesha kana kwamba ama unataka wabunge waongezewe muda au Rais Kikwete aongezewe Muda. Na kwa kuwa sasa tumekosa statemen ambao wangeweza kuangalia mambo juu ya siasa kama Mwalimu Nyerere, mjadala kama huu utakufa kibudu.
Hata hivyo ni hoja nyeti sana katika kulinda Demokrasia ya vyama vingi na
katika kuhakikisha nyakati za uchaguzi Taifa halitetereki kwani Asasi za
Dola 2/3 zinakuwapo.
I would go for 6 years Urais and 4 years Ubunge.
Wanasayansi ya Siasa wanaweza kutusaidia faida na hasara za mfumo ambao tunaujadili na tukafanya mjadala huu mpaka mwisho na kutoa ripoti maalumu ya wanabidii kwa umma na mamlaka husika. Labda tunaweza kuwa chachu ya marekebisho ya mfumo wetu wa uchaguzi.
Zitto
Zito naye akajibu ifuatavyoKaka Zito
Shukrani kwa maelezo ya kina zaidi kuhusu suala hili. Ni wajibu wetu kuhuisha mijadala yenye tija kwa taifa letu hata kama kwa kuanzia haitakuwa popular!
Ili kuepuka kujadili watu, kama ulivyosema, tunaweza kusema lini utaratibu huo uanze, mathalani kwa rais atakayeingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu. Vivyo kwa wabunge, utaratibu mpya utumike baada ya bunge hili kumaliza muda wake, au hata baada ya uchaguzi wa mwaka 2015. Kwa kuweka benchmark tunaweza kuepuka hoja za kisiasa kwamba tuna agenda ya siri kumwongezea muda mtu fulani. Gharama ya muda na mchakato si kitu iwapo tija ya kufanya mabadiliko tunayoyatazamia na kuyaamini ni kubwa.
Pamoja na mjadala huu, suala la kurejesha uchaguzi wa madiwani kwenye chaguzi za serikali za mitaa halina budi kuhuishwa. Haileti maana, madiwani kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wakati wenyeviti wa mitaa/vijiji na vitongoji wanachaguliwa tofauti.
Nachangia.
Jambo la kushangaza, ni kuwa gazeti la Tanzania Daima limetumia mjadala ule na kuandika habari yenye kichwa cha habari kisemachoLingson,
Tunaweza kuwa na utaratibu ambao mfano, 2014 tunafanya uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Madiwani. 2015 Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na 2016 Uchaguzi Mkuu wa Rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa tunaanzia watakaochaguliwa mwaka 2010.
Ukishakuwa na daftari la kudumu la wapiga kura na Tume Huru ya Uchaguzi, gharama za uchaguzi huwa haziwi kubwa sana kama iwapo hakuna daftari na Tume ya uchaguzi mbovu kujaribu kupata fedha nyingi wawezavyo. Chaguzi za madiwani na wenyeviti wa serikali za mitaa z5naweza kabisa kuendeshwa na Kamati huru za Uchaguzi katika ngazi za Wilaya. Tatizo hatuna uaminifu katika masuala haya na ndio maana hata huu uchaguzi wa mitaa tumetaka usimamiwa na tume.
tatizo kubwa katika taifa letu hatuna mijadala ya kina na yenye kufika
mwisho kuhusu masuala yenye masilahi kwa taifa kwa ujumla wake.
Mjadala uendelee
"Zitto: JK aongezewe Muda"
katika habari ile siyo tu kuwa mwandishi alipotosha mchango uliokuwa umetolewa na Zitto pale wanabidii.net, bali pia alitumia habari ile bila kuomba kibali cha Zitto mwenyewe au kwa moderator wa Wanabidii.net unless kama yeye mwenywe mwandishi ndiye moderator. Kitendo kile kimafnaya Zitto atangaze kujitoa katika group ile, na mpaka sasa ninapoandika bado wanajadiliana na kumwomba Zitto afikirie tena uamuzi wake. Kilichionishangaza ni pale mhariri wa Tanzania Daima bwana Absalom Kibanda (ambaye pia ni mwanachama wa Wanabidii.net) aliposema kuwa hakubaliani na tafsiri ya mwandishi wake kuhusu maneno yaliyotolewa na Zito lakini bado akamlaumu Zito kwa kusababisha maneno yake yawe yatafsiriwe vibaya na yule mwandishi; hakujilaumu kama mhariri kuwa aliruhusu kuchapishwa kwa habari isiyothibitika!!! na mbaya zaidi kwa maoni yangu ni kuwa mhariri hakukubali hata kuomba radhi kutokana kosa la mwandishi wake, badala yake kumtaka Zito atoe maelezo ya kufafanua alikuwa na maana gani katika post ile kama nilvyoonyesha hapa chini
Baada ya kusoma hayo huko Wanabidii.net, nikastuka kidogo kuwa hata sisi tuna wanachama wanasiasa hapa JF ambao hutumia majina yao kutoa mada mbalimbali na wanaweza na kuja kujikuta katika hali kama iliyomkuta Zito: post zao zikachukuliwa out of context na kuwekwa kwenye headline za magazeti. Ingawa nimewahi kuona mada zinatolewa hapa na kuwekwa kwenye forum nyingine lakini sijawahi kuthibitisha posts za wachangiaji wetu zikipotoshwa huko nje.
Swali langu, je hapa JF tuna utaratibu gani wa kulinda michango original ya wanachama wetu (hasa wale wanaojulikana kwa majina yao halisi) isipotoshwe kwenye print media au kwa njia nyingine yoyote?
Wanabidii
Ndugu zangu wasomaji wa mtandao huu ambao hakuna shaka hata kidogo umekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza utamaduni wa mijadala na utoaji wa mawazo tofauti.
Mimi ndiye Mhariri Mtendaji wa Tanzania Daima, Absalom Kibanda ambaye leo asubuhi nilizungumza na Zitto Kabwe kuhusu habari iliyochapishwa katika gazeti letu leo hii na kimsingi nikaungana naye kusikitika kwamba alikuwa amenukuliwa kwa makosa.
Katika mazungumzo yetu na baadaye katika mawasiliano ya simu, Zitto alinieleza wazi kwamba alikuwa na mashaka kuwa habari hiyo iliandikwa kwa nia mbaya dhidi yake na kimsingi akafikia hatua ya kufikiria kwamba, habari hiyo huenda ikawa na mkono wa viongozi wenzake ndani ya Chadema ambao amekuwa akivutana nao kwa muda mrefu.
Tukiwa katika mazungumzo nilimueleza wazi kwamba habari ile ilionekana wazi ikijenga taswira kwamba yeye alikuwa ameshaanza kula njama na viongozi wa CCM ili kumruhusu Kikwete aendelee kuwa rais hadi mwaka 2016 chini ua utaratibu wa kugombea kwa miaka sita hali ambayo inaweza kutafsiriwa na wengi kuwa itamuwezesha yeye Zitto kupata fursa ya Kikatiba kugombea urais kwani atakuwa amefanikiwa kutimiza umri wa miaka 40 inayotakiwa kikatiba.
Nilimtaka anipe muda wa kujadiliana na mwandishi wa habari ile, mhariri aliyekuwa katika dawati jana ambaye ingawa alinibrief kuhusu habari hiyo na kunihakikishia kuwa Zitto alikuwa ameyasema maneno hayo jana nilipaswa kuzungumza naye na kisha kupima hoja za pande zote mbili kuhusu suala hilo.
Baada ya kufanya majadiliano na wenzangu, nilikuwa ndiyo kwanza najipanga kuzungumza na Zitto na kumpa taarifa za upande wa pili kuhusu kile kilichoandikwa na namna ambavyo tungefanya kurekebisha kasoro hii.
Ni jambo la bahati mbaya sana kwamba Zitto anaonekana kukosa subira na ameamua kurusha malalamiko dhidi ya habari ile jambo ambalo kimsingi ni haki yake lakini akaenda mbele kusema wazi kwamba habari ile iliandikwa kwa nia mbaya dhidi yake na hakuishia hapo akasema hii si mara ya kwanza kwa gazeti hili kuandika habari ambazo anasema 'hazina ukweli wa kutosha'.
Napenda kuwahakikishia wanabidii na Watanzania wenzangu kwa ujumla kwamba, hitimisho la Zitto kuwa habari ile iliandikwa kwa nia mbaya dhidi yake si za kweli hata kidogo na Zitto mwenyewe analitambua hilo sana kwani ni mmoja wa watu wanaoufahamu vyema utendaji kazi wa gazeti hili pengine kuliko ilivyo kwa mwanasiasa mwingine yeyote.
Lakini kilichonisikitisha zaidi ni uamuzi wake wa kufikia hatua ya kutaka kujitoa katika wanabidii kwa sababu ya kuwapo kwa kile alichodai kwamba kuna watu wenye nia mbaya dhidi yake. Sentensi hii ni ushahidi wa wazi kwamba hadi sasa Zitto anaendelea kuamini kwamba gazeti lile liliandika habari kwa nia mbaya. Haiingii akilini hata kidogo.
Binafsi kama mhariri baada ya kumsikiliza Zitto na kisha kuipitia taarifa ya wanabidii alikotuma maneno yake, niliona wazi kuwapo kwa uwezekano mkubwa wa maneno ya Zitto kutafsiriwa kuwa yanamlenga Kikwete kama alivyotafsiri mwandishi na mhariri aliyesimamia uchapaji wa gazeti la jana. Zitto anatambua vyema namna nilivyo mvumilivu sana ninapopingwa kwa hoja ambazo ninazisimamia.
Kwa sababu hiyo basi kwa kuwa ninaheshimu uhuru wa watu kufikiri pasipo kuvunja sheria za nchi, ninamruhusu Zitto kuwasiliana ama na gazeti hili kufafanua kile alichotaka kusema akiondoa hoja yake kwamba habari ile imeandikwa kwa nia mbaya dhidi yake na/ au kuwasiliana na gazeti jingine analoloona litafanikisha azma yake ya kuisahihisha habari aliyoiandika.
Lakini zaidi ya hilo wakati bado tukiendelea kutafakari nini cha kufanya katika Tanzania Daima kumtendea Zitto haki ambazo tunaona hakutendewa katika gazeti hili, napenda kusema bayana kwamba anao uhuru wa kuchukua hatua zozote anazoona zinafaa kusafisha jina lake.
-
Mimi pamoja na kuwa sina elimu ya uandishi wa habari, nilisoma thread ile yote na kuona kuwa Zito alikuwa akitoa mawazo pana ambayo hayakuwa yanamhusu mwanasiasa yeyote specific, i.e. Kikwete kama ilivyoripotiwa na tanzania daima. Na alikuwa ni mchangiaji tu kama ambavyo huwa tunachangia hapa mada mbalimbali zinazoanzishwa na watu mbalimbali.Zitto
Nimekusoma na nimekuelewa. Mobini Sarya ni mwanabidii na nimelihakikisha hilo, na yeye ndiye aliyeandika habari hiyo. Sikubaliani kabisa na tafsiri yake ingawa naiheshimu kwani naweza kuona waziwazi alikoitoa kutokana na maandishi yako. Acha nikuonyeshe ushahidi wa maneno yako wewe mwenyewe.
"Tunaweza kuwa na utaratibu ambao mfano, 2014 tunafanya uchaguzi wa Vijiji, Mitaa na Madiwani. 2015 Uchaguzi Mkuu wa Wabunge na 2016 Uchaguzi Mkuu wa Rais. Hivyo tunaweza kusema kuwa tunaanzia watakaochaguliwa mwaka 2010."
"Mjadala kama huu Tanzania nina mashaka hautakuwa na tija kwani watanzania huwa tunajikuta tunajadili watu badala ya masuala. Hoja kama hii ni rahisi sana kwa wanasiasa kuonyesha kana kwamba ama unataka wabunge waongezewe muda au Rais Kikwete aongezewe Muda".
Kaka maeneo haya mawili ni rahisi sana mtu kama Mobini na wengine kuyageuza au kuyatafsiri kuwa yalikuwa na lengo la kumtengenezea njia Kikwete. Nadhani unatambua duniani kote kwamba wanasiasa mnashauriwa kuwa makini sana kwa chochote kile mnachotamka kwani kinaweza kutafsiriwa kinyume cha kile mlichokimaanisha.
Ukweli wa namna hii mara nyingi huwa ni mchungu kwa wanasiasa wengi na ndiyo maana wengi wamekuwa waangalifu sana kutoa maoni hadharani na kila wakati. Wewe mwenyewe ni shahidi mzuri kwamba maneno ya Dk. Slaa dhidi ya Kafulila kwamba kijana yule ni 'dagaa' yamemgarimu kiasi gani mzee yule na kwa kiasi gani maadui wa Slaa na Chadema wanayatumia kumvuruga Slaa na chama chenu.
Kumbuka maneno kama yale ya Kikwete aliposema kuwa "Urais wangu hauna ubia" yalivyotafsiriwa na kila mtu kwa namna na kwa tafsiri yake. Tanzania Daima kwa maelekezo ya mhariri wake ambaye ni mimi tumekuwa na desturi ya kufanya 'analysis' na wakati mwingine 'analysis' huwa zinafanyika katika mitazamo ambayo si sahihi.
Kwa sababu hiyo basi, majibu yangu kwako hayakubeba arrogance ya aina yoyote ingawa nilisikitishwa na uamuzi wako wa kulishambulia Tanzania Daima katika misingi isiyo sahihi (kwa mtazamo wangu). Naamini kwa dhati kabisa kuwa unatambua vyema kwamba habari ile hata kama ina kasoro ya tafsiri, haikuandikwa kwa nia mbaya hata kidogo. Tanzania Daima kama gazeti siku zote limekuwa likisimamia ukweli pasipo kujali machungu ya ukweli huo kwa ndugu, marafiki na jamaa zetu.
Najua na kutambua kuwa, umejijengea taswira ya kipekee kisiasa ambayo hautakuwa tayari kuona ikiharibiwa na mtu yeyote yule kwa namna yoyote ile. Na msimamo wako huu ambao ni wa msingi kabisa naamini kuwa ndiyo unaokusukuma kila mara kuipigania haiba yako hiyo ya kisiasa. Hivyo hivyo Tanzania Daima ni brand ambayo nimepambana sana kuifikisha hapa ilipo leo kwani inajenga taswira yangu binafsi na ya wenzangu wengine kama mimi.
Ni kwa sababu hiyo siku zote nimekuwa sina sababu hata moja ya kumhurumia mtu yeyote ambaye kwa kujua au kutokujua anaamua kuidhalilisha brand hii (Tanzania Daima) kwa kuipachika sifa za uongo na za kuipaka matope. Ni kwa sababu hiyo kwa nyakati tofauti nimekabiliana ana kwa ana na yeyote anayejaribu kufanya kosa hilo kwa namna na njia ambazo wakati fulani huwa zinaniweka katika mazingira magumu.
Ninafanya hivyo kwa kuwa natambua kwamba baadhi ya watu, akiwamo wewe Zitto ni watu ambao brand hii (Tanzania Daima) imewapigania kwa wema na kuchangia mafanikio yao ya kisiasa kwa kiwango kikubwa pengine kuliko brand nyingine zote. Naweza kusema wazi kwamba, ni gazeti hili ambalo katika masuala ya msingi lilisimama na litaendelea kusimama nawe bega kwa bega hata kama kwa kufanya hivyo tutatofautiana na ndugu zetu, marafiki zetu na wakati mwingine wamiliki wetu. Tumelifanya hilo mara nyingi na tuombe maisha tutaendelea kulifanya hilo mbele ya safari.
Ni mwandishi na mhariri mpumbavu tu ambaye atashindwa kutambua mchango mkubwa wa Zitto katika maendeleo ya siasa za ushindani na demokrasia ya kweli ya vyama vingi. Ni mwanahabari mwehu ambaye anaweza akasimama leo na kupinga ukweli kwamba Zitto ni chachu kuu ya mchango wa kipekee wa viongozi vijana katika taifa hili.
Zitto na wanabidii wenzangu wengine wanapaswa kutambua hilo na ushahidi upo kwamba Tanzania Daima limekuwa na desturi ya kuomba radhi katika kila jambo kubwa ambalo hudhani tumelikosea na kwa kufanya hivyo wakati mwingine tumekuwa tukiingia katika matatizo makubwa ya kimtazamo. Wako waliotuita waoga, wanafiki, wazushi na kila aina ya majina. Na hata katika hili, tupo tayari kuomba radhi iwapo tutajiridhisha pasipo shaka kwamba tumefanya makosa.
Utabakia kuwa mwanasiasa wa mfano na wa kipekee kwangu. Ni kwa sababu ya kukuheshimu wewe binafsi ndiyo maana marafiki na maadui zako ndani na nje ya Chadema wanaheshimu na kutambua ukaribu wetu kwa kuwa nimekataa kuwa mnafiki.
Hata hivyo wewe unalitambua hili, kwa sababu ya dhamira safi ya kukujenga, kukukomaza na kukutakia mema nitakuwa wa kwanza kukunyoshea kidole pale ambapo mtazamo wangu na uchambuzi wangu utanithibitishia kuwa umekosea na hivyo hivyo nitakuwa wa kwanza kukutetea na kukupigania katika mambo ya msingi utakayofanya na kuyasimamia. Nimeyafanya hayo na historia itanilinda. Utabikia kuwa ndugu yangu, rafiki yangu na mwanasiasa wa mfano japo utakapoteleza au kuanguka sintakaa kimya.
Absalom Kibanda
Mhariri Mtendaji
Tanzania Daima
Baada ya kusoma hayo huko Wanabidii.net, nikastuka kidogo kuwa hata sisi tuna wanachama wanasiasa hapa JF ambao hutumia majina yao kutoa mada mbalimbali na wanaweza na kuja kujikuta katika hali kama iliyomkuta Zito: post zao zikachukuliwa out of context na kuwekwa kwenye headline za magazeti. Ingawa nimewahi kuona mada zinatolewa hapa na kuwekwa kwenye forum nyingine lakini sijawahi kuthibitisha posts za wachangiaji wetu zikipotoshwa huko nje.
Swali langu, je hapa JF tuna utaratibu gani wa kulinda michango original ya wanachama wetu (hasa wale wanaojulikana kwa majina yao halisi) isipotoshwe kwenye print media au kwa njia nyingine yoyote?