Hii taasisi ya kupambana na kuchochea rushwa tangie iundwe haijaweza kukidhi malengo. Tumeona rushwa imekithiri mpaka mwenye mamlaka ya juu kwenye nchi analalamika kwa wananchi. Ndugu zanguni watanzania tuna haja gani ya kuendelea kupoteza kodi zetu kwenye kitu kisichokuwa na maana. Hii taasisi imekuwa ikitengewa fungu kubwa sana lakini rushwa imeongezeka na iko waziwazi, askari wa barabarani wanapokea rushwa kweupee na kwenye foleni bila wasiwasi.
Naomba watetezi wetu wakina Deo Filukunjombe, Zitto Kabwe, Mnyika, Tindu Lisu(Jembe), Mch Msigwa, Mch Israel Natse na majembe wengine mupeleke hili swala likajadiliwe bungeni. Pia hapa tunaomba maoni yenu. Mzee wangu Hosea nakushauri urudi tuu chuo ukafundishe kama wewe ni mungwana na unaonea huruma kodi yetu.
Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums