Umenena vema ndugu yangu. Hilo ndilo linalotakiwa kwa dunia ya sas na siyo hiyo Historia yake. Haisaidii. Kwa sasa dunia yote inazungumzia uchumi wa viwanda (Industrial economy) ambapo bidhaa zote kutoka kwenye sekta zote za kijamii na kiuchumi kama vile elimu, kilimo, afya, maliasili, n.k sharti zizalishe vitu na watu wanaoweza kuishi na kuendesha maisha kwa kutegemea soko la viwanda kama mazao, viatu,nguo, ndala, mikanda, simu, vipuri mbalimbali, n.k.
Sasa huyu mwenzetu anatataka twende kinyumenyume badala ya kwenda mbele. Nilivutiwa sana na ubunifu wa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu ndugu Antony Mtaka ambaye mkoani kwake walianza kutebgeneza Chaki. Hivyo hata watoto wakimaliza shule wengine wangeingia kwenye shughuli hiyo na wengine shughuli nyingine. Sasa unakazania eti Historia ya kwamba fulani alikuwa Rais wa awamu ya tano na alijenga flyover ubungo. Baada ya hiyo Historia nini kinaendelea kwa huyu mwanafunzi?
Kwa kweli viapawa vya watoto huanza kutambuliwa, kukuzwa na kuendelezwa mapema kabisa katika umri wao mdogo na siyo kwenye utu uzima wa chuo Kikuu. Ndiyo maana tunakwama sana kuendelea kwa Sababu hata utafiti mtaala wetu unakazia zaidi kwa watu wa vyuo vikuu wakati hata ngazi za chini zingefanya kwa sehemu yao. Mtaalamu mmoja aitwaye Howard anasema binadamu wana vipawa tofauti tofauti (multiple Intelligences) kwa kufaidishana hivyo hata elimu itambue hivyo na isiwafundishe watoto wote kwa njia moja tu.
Wataalamu wa Elimu wapo wa kutosha kabisa na wanalijua hili ila wameamua kuwaachia na kwa kweli wamewazilia wanasiasa wafanye watakavyo. Na sisi jamii tukiendelea kuwasikiliza wanasiasa tunakipoteza kizazi hiki kabisa!