Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC

Kumuita mwenzako mhuni unatakiwa uwe na ushahidi unaohalisika kudhibitisha, ili neno halitumiki hivi hivi kimasihara masihara hasa kwa mwandishi makini wa habari.
 
"tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti"

hapo kwenye red sijakuelewa kabisa ina maana TBC hawawaungi mkono CDM na ni kwanini wakati ni TV ya jamii, kama inapendelea upande mmoja ulitaka wana Arusha wawachekee? au ulitaka wawakumbatie? ni habari gani walikuja kuchukua? je walikuwa na ulinzi wa kutosha? sababu nasikia wao wanataka ulinzi tu, hiyo habari nimeisikia kwako kama ni yakweli nawapongeza wote waliofanya hivyo.
 
kwa maoni yaliyotolewa umeshajifahamu ni kwa namna gani hustahili kuitwa mwaandishi wa habari
iga mfano wa jenerali Ulimwengu,Tido,na wengineo wanaoheshimika utafika mbali
kwa ufupi tumefahamu kuwa kuajiriwa TBC lazima uwe mwana CCM na utangaze mazuri ya TBC pekee
kumbe TBC haipo kwa ajili ya umma bali kwa ajili ya chama tawala huku mkitumia kodi zetu
kueneza propaganda zenu badala ya kuwaa kio cha kumkomboa Mtanzania maskini.
mlaaniwe na mpoteeee ktk masikio na macho ya watanzania.Tunaisubiri Aljazeera swahili kuwa mkombozi wetu.
 
Nawaomba sana WANACHADEMA wenzangu tuachane na huyu kijana....kwanza anatupotezea muda.Tuna mengi ya kufikiri na kujadiliana..
Tungefurahi kama mkurugenzi wa TBC1 ama Katibu Mkuu Wizara wa Habari,Utamaduni na Michezo wangekuja hapa jamvini kujibu maswali tuliyonayo..Huyu jamaa hana majibu.
Nimemaliza.
 
Sikio la kufa halisikii dawa. TBC mnakera, mnatia kinyaa na mmekubali kutumiwa na mnatumika kwelikweli. Tunasubiria kifo chako TBC ambacho kiko kwenye karibu.
 
Kwanza aliyesema ni dhambi kuwa mwanachama wa CCM nani? Ningekuwa CCM wala nisingejikana na kuona haya maana hiyo ni haki yangu ya kikatiba.

ni dhambi kupindisha ukweli kwa maslahi ama yako binafsi au maslahi ya hao viongozi madhalimu wa magamba unaowatumikia mpaka kufikia hatua ya kutoheshimu 'core values' ya taaluma unayodai kuisomea (kama kweli umeisomea)
 
Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.
1. Nyie kama TBC mnawaunga mkono akina nani? Kama ni CCM basi mnastahili mlichofanyiwa; kwa kuwa hamna shirika na watanzania.
2. Mliwaomba hao 'wahuni' wawaoneshe kadi zao za uanachama? Siamini kama Chadema ina wanachama wengi kiasi hiki. Kila mtu akiipinga CCM anaitwa Chadema, na si watu waliochoka utawala wa CCM.
3. Kaka/Dada (Jina halioneshi jinsia) hii vita hautashinda ungali kanjanja, nenda kasome hata ka diploma ufunguke akili.
 
thibitisha kama hao ni wana CHADEMA! Huna maana Gamba wewe

ameshindwa kuweka sawa hayo yalitokea katika mkutano wa mbowe mara baada ya kesi ya lema uliofanyika makao makuu ya mkoa wa arusha ya cdm lakini pia ilishawahi kutokea katika mahakama ya mkoa wa arusha katika moja ya kesi za cdm
 
hilo ndilo lililonishangaza! Hao ndiyo waandishi wetu wasiokuwa na ethics! Mtu unatukana jamii nzima kwa ajili ya watu watatu! Nani muhuni kama si yeye

ni wale tu wanaowazuia waandishi wa habari wa tbc kufanyakazi,mbona ina eleweka
 
wewe unaejiita doto athuman ni popompo na sio mwandish, nenda kasome uwe mwandish makin unae jiamini, inaelekea unapewa vijiela na wanaume wenzio uandike upuuzi, wakazi wa arusha ni watu makini na wamekombolewa kifikra, wanamawazo endelevu ndo maana hawayumbishwi na siasa za udaku ambazo zimeingia hadi tbc, wako tayar wamuonyeshe lusinde akitukana na wala sio nasari akitoa hoja za maendeleo.
 
kuna tabia ya watu kupotosha hoja makini za watu humu ndani. chamsingi hapa nh kwamba bila kujali vyama hv mtu yoyote mwenye busara hawezi kushangaa kupingwa kimawazo na m2 mwingine kwani kila mmoja anamawazo yake nawangependa yaheshimiwe zaidi ya kwamba ni haki ya kikatiba. sasa mi binafsi sioni sababu ya kuchukiana au kujenga uadui eti kisa tunatofautiana kimawazo au kiitikadi. tuachane na siasa za maji taka na tujifunze kuheshimiana bila kujali tofauti zetu.
 
Huyu mwandishi wa habari kumbe ni kichaa mwacheni jamani ajichangie mwenyewe maake kama mtu hujarukwa akili lazima uone kuwa hapa kuna kasoro huna haja ya kubishana na watu waliowengi. Ukigombana na watu zaidi ya wawili kwa siku hebu anza kujitafakari kwa nini wewe umegombana?
 
Pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini bado watanzania wanapaswa kuheshimu na kuthamini huduma ambayo wote tunajua mazingira yalivyo si tu Tanzania lakini bara zima la Afrika linapokuja suala la Uhuru wa vyombo vya habari. Kitendo kilichoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao kwangu nawaona ni "wakazi wahuni" kujaribu kuwazuia waandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kufanya kazi yao kwa kigezo kuwa wanatoa taarifa za kupotosha hazina msingi na walipaswa kutafuta njia nyingine ya kuonyesha kwao kutoridhishwa na utendaji wa shirika hilo. Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.

NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi kama mwanahabari, wala hakuna mahusiano na itikadi au maslahi ya shirika lolote.


Nilidhani tunapingana kwa hoja na mtu makini anayeijua fani yake ikiwa ni pamoja na weledi wa kazi yake, kumbe tunabishana na MBUDA fulani hivi!!!
 
My take:

Baada ya kulumbana na kuvurumishiana maneno ya kashfa sasa naomba kuufunga rasmi mjadala huu (kwa upande wangu) kama ifuatavyo;

1. Michango yenu nimeithamini sana kwa kuwa ujumbe wangu umewafikia zaidi ya watu 3000 waliopita kuisoma thread hii. Natambua kuwa wengi mmeguswa kwasababu ya mapenzi yenu binafsi mliyo nayo iwe kiitikadi au kizalendo (kwa wakazi wa Arusha waliojihisi wamelengwa wao). Naomba ieleweke kuwa maoni haya ni yangu binafsi na sijatumwa ila nimewiwa kutoa maoni haya kwa kuwa waliotendewe hivi ni waandishi wenzangu na kama tutaendelea kuchekelea tabia hii isiyo ya kiungwana basi ipo siku hata hao wanaonekana wanapatia yatawakuta. Chombo cha habari chochote kinafanya kazi kwa mujibu wa sera zake za ndani, na waandishi ni watekelezaji wa sera hizo hivyo kuwahukumu kwa njia ya aina hii ni uonevu. Lakini pia njia ya namna ikiendelea kufumbiwa macho itabadilika na kuwa vurugu. Kumbukeni kuwa Waandishi pia ni raia wa tanzania, wanahaki kama mliyo nayo nyie, na wana uhuru wa kufanya kazi yao pasipo vitisho au hila. Inawezekana akawa kaka yako, Baba yako, Mama yako au hata mtu wako wa karibu, je unahisi utajisikiaje akadhurika kwa sababu tu anatekeleza majukumu yake bila kujali yuko mlengwa wa aina gani. Kama kweli kikundi cha watu kinahisi chombo fulani hakitendi haki basi vipo vingine vinaweza kutumika na wananchi watapima nani yuko sahihi au mnataka kutuaminisha kuwa watanzania wote ni maboga na wanaweza kuongopewa kirahisi na chombo kimoja dhidi ya vingine ishirini na?

2. Michango mingi imeelekezwa kwangu binafsi na sehemu nayofanyia kazi. Kwa wale walioninyooshea kidole moja kwa moja nakubaliana nao asilimia mia moja wako sahihi kwasababu njia niliyoitumia ililenga kuwaonyesha maudhi na kweli wameudhika na wameonyesha hivyo kwa kurejesha hisia zao kwa njia kama yangu. Ila wale waliohusisha maoni haya na sehemu nayofanyia kazi nahisi walikosa msingi wa mjadala, hata hivyo naelewa kwanini walichukua fursa hii kuihusisha na ofisi yangu, nataka kuamini kuwa wanaamini hapa palikuwa sehemu muafaka kutoa machungu yao kwa kiingereza nitasema "formal feedback". Nawashukuru pia na wala sina kinyongo nao, naomba na wao pia waondoe kinyongo na mimi na ikibidi waondoe kinyongo na kituo changu cha kazi. Hii ni nchi yetu sote, inawezekana nyie hamjafaidika na utawala wa CCM lakini mtambue wapo waliofaidika na hivyo wataendelea kuiheshimu CCM na kuitumikia hadi pale watakapoona kuna tatizo. Kutumia vitisho, maneno ya kashfa au lugha zinginezo hakutabadilisha mtazamo wao kwasababu watapima kwa kuangalia maisha yao binafsi kabla kununua hoja zenu ambazo nahakika lazima ziwe na mashika kwao. Hii ndo maana hata katika uchaguzi mdogo uliopita hapo Arusha wapo wana Arusha zaidi ya 26000 kati ya 60000 waliopiga kura wameichagua CCM.

3. Kuhusu la weledi wangu sitalizungumzia kwasababu jina langu si la kificho kama wengi wenu maanake unaweza kupata taarifa zangu kirahisi hata humu kwenye mtandao. Naamini maneno yote yaliyotumiwa dhidi yangu ni sehemu ya mnyukano wa hoja ambapo kila mtu ana hulka yake anaposhikwa pabaya. Wapo hata walionitishia usalama wangu, hilo nalipokea kwasababu mwandishi yoyote yuko tayari kwa kitakachomtokea anapokuwa katika utekelezaji wa shughuli zake. Hata leo nikiambiwa nikachukue habari vitani nitafanya hivyo bila ubishi maana huo ndo wajibu nilioamua kuufuata. ushauri wangu kwa wote waliochangia iwe kwa dhati au kwa upotoshaji tuvumiliane na tukubali kuwa wapo watanzania wanayo haki ya kuamini wanachoamini bila kushurutishwa au kubezwa, ndo demokrasia tulioichagua.

4. Naomba kusimamia kwenye msimamo nilioanza nao hapo awali, kuwa kitendo kilichoonyeshwa na baadhi ya wakazi wa Arusha ni cha kihuni na hakifai kuigwa wala kufumbiwa macho. Binafsi nakiunga mkono CHADEMA na ningependa siku moja wafikie hatua nzuri ambayo itatuletea maendeleo kama taifa, lakini kwa sasa Serikali iliyo madarakani ni ya CCM na mimi kama mwandishi naiheshimu sana CCM tena sana, kwasababu sehemu ya mafanikio yangu imetokana na fursa zilizotengenezwa na serikali hii. Yapo maeneo ambayo kama serikali imeshindwa kuyafanyia kazi na naamini wapo wenye nia ya dhati ndani ya serikali kuhakikisha wanaleta mabadiliko, hata hivyo kwenye msafara wa mamba hawakosi kenge. CCM ni chama kikongwe hivyo wapo wachafu na wasafi, kwangu mimi sitathubutu kuwaita wote ni wachafu kwasababu kundi fulani linalazimisha hivyo. Tuvumiliane na tutofautiane kwa hoja si uwezo wa kutoa kashfa na kuitana majina kwasababu hiyo sio siasa ambayo itawasaidia kuingia ikulu. Ni sawa na mtu anakuja kukuhubiria kuwa dini yako si sahihi wakati maisha yangu yote nimekulia na kuona namna watu wa dini yangu wanavyoendesha maisha, sitakuelewa lakini ukija kwa utulivu na ukanielewa napokosea naweza pia kwa utulivu nikakuelewesha napopaona pananifaa ndani ya kosa uliloliona wewe. Najua wapo watakao chukua kipande hiki na kutoa majumuisho, nasema ruksa ni haki yenu ya kikatiba.

5. Mwisho kabisa ni kwa wanachadema wote hasa vijana wenzangu. Tuige mfano wa waonatuongoza, njia wanazozitumia na hata njia wanazotumia kufikia muafaka. Viongozi wengi wa CHADEMA ni makini hukubali pale wanapoona kuna tija na husema kweli panapohitaji kusema kweli, hii ndo iliyokijengea heshima chama chenu. Sasa msilewe sifa kwa kazi walizoanzisha wengine na mkawaharibia dira yao. Tuzungumze kwa busara na pia lazima mkubali kuwa wapo wasiokubaliana na sera zenu, na wakijitokeza kuwaeleza chukueni muda wa kuwalewa na tumieni maoni yao kujijenga kisiasa sio kupandikiza chuki na vitisho. Tanzania ni kubwa, na siasa inatengenezwa hailazimishwi. Wote tunajua chama cha wananchi CUF kina ngome imara kule pemba na hakuna wa kupenya kirahisi, hivyo hata CDM inatambulika kuwa Ngome kuu iko wapi lakini haina maana huko kote hakuna wafuasi wa vyama vingine.

Kwa hitimisho hili sitaendelea na malumbano haya, na wanaotaka kuendeleza matusi na kashfa ruksa kufanya hivyo. Mimi ni mpenzi wa Arsenal, wakati fulani huwa timu yangu inaboronga sana kiasi napata hadi hasira lakini kinachotia hasira ni maneno ya washabiki wa timu zingine pinzani lakini sijawahi kufikiria kuhamia timu pinzani kwa kuwa timu yangu inaboronga. Huwa naamini kuwa ipo siku tutazinduka na kufanya vizuri. Maanake ni kuwa mtu anaamua kupenda kitu fulani ni rahisi kuwehuka pasipo kuangalia ukweli wa kinachosemwa. Kwahiyo kama wapo wataoshindwa kunielewa baada ya hitimisho hili sitashangaa....NDO MAPENZI YALIVYO.

Wasalaam!!
 
TBCCCCCCCCCC ni enzi ya TIIIDO Mhando acheni kabisa mimi kubadilisha chalel naona tabu, lakini sasa imerudi enzi zile za '' vikra za stone age; Enzi ya TID'o uwanja ulikuwa sawa lakini sasa unatia shaka.
 
Apple don't fall far from the tree. Anayeona wengine ni wahuni inaonekana anaakisi taswira yake mwenyewe... Tafakari chukua hatua
 
Back
Top Bottom