Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni yangu dhidi ya "Baadhi ya wananchi wahuni" wa Arusha kujaribu kuzuia wanahabari wa TBC

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dotto Athumani, Apr 6, 2012.

 1. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #1
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pamoja na changamoto zinazoikabili tasnia ya habari nchini bado watanzania wanapaswa kuheshimu na kuthamini huduma ambayo wote tunajua mazingira yalivyo si tu Tanzania lakini bara zima la Afrika linapokuja suala la Uhuru wa vyombo vya habari. Kitendo kilichoripotiwa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kuwa, baadhi ya wakazi wa jiji la Arusha ambao kwangu nawaona ni "wakazi wahuni" kujaribu kuwazuia waandishi kutoka Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kufanya kazi yao kwa kigezo kuwa wanatoa taarifa za kupotosha hazina msingi na walipaswa kutafuta njia nyingine ya kuonyesha kwao kutoridhishwa na utendaji wa shirika hilo. Nachelewa kusema kuwa tabia iliyoanzishwa na baadhi ya wafuasi wa CHADEMA kuwaona kila wasio waunga mkono ni wasaliti haifai na wala haileti picha ya uvumilivu wa kisiasi ambao tungetarajia kuuona ukihubiriwa kwa vitendo na yoyote anajipambanisha na chama au jumuiya makini.

  NB: Huu ni mtazamo wangu binafsi kama mwanahabari, wala hakuna mahusiano na itikadi au maslahi ya shirika lolote.
   
 2. kanininyo

  kanininyo Member

  #2
  Apr 6, 2012
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe lazima utakuwa full magamba.
   
 3. Loy MX

  Loy MX JF-Expert Member

  #3
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 1,263
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  una ushahidi gani kama wanaoichukia TBC ni CDM???
   
 4. M

  Massenberg JF-Expert Member

  #4
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 1,173
  Likes Received: 1,061
  Trophy Points: 280
  Ungeandika hivi hivi pia kuhusu yanayofanywa na CCM kwa wale wasiowaunga mkono pia tungekuona una busara na akili zinazofanya kazi.
  Nyie mnapofanya upumbavu huwa siyo uhuni?
   
 5. H

  Hodarism Member

  #5
  Apr 6, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 89
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vita haina macho athumani
   
 6. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #6
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,962
  Likes Received: 1,284
  Trophy Points: 280
  Hao watu si wajinga,uchaguzi Arumeru mliandika barua kuomba ulinzi, kama mligomewa ya nini kwenda? Muwe na ulinzi wa green guards kote. TBC ni Taarifa na Burudani kwa Ccm
   
 7. Boniface Evarist

  Boniface Evarist JF-Expert Member

  #7
  Apr 6, 2012
  Joined: Nov 26, 2010
  Messages: 1,100
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Tena wewe ni mwanahabari halamu kwani umewezaje kuwataja CDM?
  potea na ki-certificate chako kinachowalinda Magamba.
   
 8. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #8
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Soma vizuri maelezo acha kupindisha maelezo yangu.
   
 9. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #9
  Apr 6, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  unapoita watu wa Arusha "wahuni" unamaanisha nini?
   
 10. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #10
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wewe unadiliki kutuita wahuni kwa hivyo vijisent ulivyopewa, we subiri tuingie kwenye kampeni ndo utajua sie nani,
   
 11. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #11
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwandishi wa habari anafanya kazi popote bila kujaribu vitisho ndo maana hii leo unapata habari kutoka sehemu za vita na ngumu kwa mtu wa kawaida kufikia. Tatizo wengi wenu mnahisi siasa ni uadui na kupotosha wengine. Mbona uongozi wa CDM hawakutoa malalamiko kuwa TBC wanaripoti habari isivyotakiwa?
   
 12. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #12
  Apr 6, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  arusha hawataki unafiki!
  TBC inatumia kodi zetu kutukandamiza halafu tuendelee kuwachekea?na bado hiyo ni rasharasha mvua kamili inakuja.
  Mara ngapi humu jamvini TBC inashauriwa kufuata professionalism lakini hawaelewi?
   
 13. K

  KAMANDA HANGA Senior Member

  #13
  Apr 6, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mwana magamba sio mwana habari! Mwana habari hapendelei bali anatoa habari zilizo za kweli bila kujari zitamfurahisha yupi na kuumiza yupi; sio kama wanavyofanya TBC.
   
 14. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #14
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwanza aliyesema ni dhambi kuwa mwanachama wa CCM nani? Ningekuwa CCM wala nisingejikana na kuona haya maana hiyo ni haki yangu ya kikatiba.
   
 15. L

  Lamusumo JF-Expert Member

  #15
  Apr 6, 2012
  Joined: Mar 23, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa anawaita wakazi wa arusha wahuni kisa wanaiunga mkono cdm,hizi njaa za wanahabari sijui ztaisha lini?
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  yani athumani unawezaje kutuita wakazi wa arusha wahuni!naomba ufute kauli
   
 17. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #17
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wewe kama unaanguka kwenye kundi la "Baadhi ya wananchi wahuni" basi hili ni saizi yako, linakuhusu siwezi kulifuta hata uje na panga.
   
 18. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #18
  Apr 6, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  je ni haki ya kikatiba kutuita wakazi wa arusha wahuni?
   
 19. Dotto Athumani

  Dotto Athumani Senior Member

  #19
  Apr 6, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni haki kabisa maana inawakilisha hisia zangu kwa watu wenye tabia isiyofuata sheria na kanuni zilizowekwa. Watakuwa ni WAHUNI TU hakuna jina lingine la kuwatosha.
   
 20. k

  kibananhukhu JF-Expert Member

  #20
  Apr 6, 2012
  Joined: Jul 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  TBC ni lazima ifanye utafiti ili ijue watanzania wanataka kuoneshwa na kusikia nn. Kinyume na hapo itakabili matatizo toka pande zote ikiwemo na serikalini. Sasahivi uwezo na ubora wa TBC upo chini ya kiwango. Hata uchanganyaji picha na maadili Ni duni. Juzi wameonesha picha ya Rais JK anang'ata mguu wa kuku "live" sikuamini. Huwa hairuhusiwi kabisa, ni aibu tbc. Hata waandishi wa somalia hawangelifanya vile.
   
Loading...