Uchaguzi 2020 Maoni Yangu: CHADEMA tukubali Wanawake waende Bungeni

Mangisandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
2,652
2,272
Kwanza kabisa sikubali mchakato wa Uchaguzi wala matokeo! Ule haukuwa Uchaguzi bali uteuzi

Pamoja na hayo, nashauri chama changu pendwa CHADEMA tumuache mbunge wetu wa Nkasi, Idah, anendeleena ubunge. Pili Halima Mdee, Bulaya, na wanawake wote wa Viti Maalum waende Bungeni, kwa masilai ya taifa na chama pia. Tusikubali kuwaachia CCM Bunge peke yao.

Faida za chama ni kuwa na insiders wetu mle bungeni, ambao watatupenyezea ya kule na watapeleka ya kwetu hata kama yatakataliwa. Pia kuna ile milioni 1 kwa mwezi, Siyo mbaya tukiipokea! Siyo swala la kujali pesa, ni kwamba kiukweli pesa inatakiwa!

Mimi naipenda CHADEMA na napenda mabadiliko, lakini wamama waende kwanza bungeni wakati harakati zingine zina endelea!
 
Mbowe na yeye anaenda lini ubalozini au atatokea kwenye mpaka wa Kenya kuanzisha episode no 5.
CDM nyumbxxxxx fc aka Kaole sanaa group.
 
amekutuma Ester umsemee?

mwambie hakuna kwenda.atulizane tuli
 
Mbowe na yeye anaenda lini ubalozini au atatokea kwenye mpaka wa Kenya kuanzisha episode no 5.
CDM nyumbxxxxx fc aka Kaole sanaa group.
Mkuu hapa tunajitaidi kushughulikia swala la wamama kwenda bungeni, mambo ya ukimbizi, tutawaanzishieni uzi mjiachie mpendavyo!
 
Wakafuate nini? Hatuko tayari kuendekeza tumbo huku wafuasi wetu wakiwa wameuliwa, kuachwa na vilema vya maisha. Hii tabia ya kuendekeza faida ya muda mfupi ndio inasababisha watu kuendelea kunajisi chaguzi zetu, na kufanya mauaji kisa wapinzani watakubali kushiriki kwa vyovyote sababu ya pesa.
 
Mkuu hawa wakuu wa chadema ni pasua kichwa.
1-Kamati kuu ya chadema walikaa na kuamua kwamba chama HAKITAJIONDOA kwenye uchaguzi mkuu.
2-Watiani nia wa chama wakachukuwa fomu za kugombea nafasi mbalimbali.
3-Hapa pakaanza figisu,wagombea wengine hawakuwa na nia ya ubunge,bali walitaka kupiga hela kiulaini kwa kujaza vibaya fomu za kugombea
ili wapige mpunga kwa kuuza .
4- Chama hakikusaidia wagombea,kisecta,kikampeni,kiuchumi,na sehemu kubwa viongozi wa kitaifa hawakutembelea.
5-Baada wa viongozi wa kitaifa kupigwa chini,wanaamua kushinikiza waliopata wasuse,Hii haijakaa vizuri.
 
Waoombeeni wale waliogombea urais kupitia vyama vingine maana wallivyojipendekeza kwa jiwe walijua watapata angalau UDAS, sasa jana jiwe kasema hateui tena nafasi zimejaa. Njoja wote tuisome namba malipo ni hapahapa
 
Wakafuate nini? Hatuko tayari kuendekeza tumbo huku wafuasi wetu wakiwa wameuliwa, kuachwa na vilema vya maisha. Hii tabia ya kuendekeza faida ya muda mfupi ndio inasababisha watu kuendelea kunajisi chaguzi zetu, na kufanya mauaji kisa wapinzani watakubali kushiriki kwa vyovyote sababu ya pesa.
Tufanye nini sasa mkuu? Seriously, tufanyeje?
 
Waoombeeni wale waliogombea urais kupitia vyama vingine maana wallivyojipendekeza kwa jiwe walijua watapata angalau UDAS, sasa jana jiwe kasema hateui tena nafasi zimejaa. Njoja wote tuisome namba malipo ni hapahapa
Mimi sipo nao wale, lakini pia nafikiri ni vyema wanawake mashujaa wakaenda bungeni! Tuwe aangalau watu wa kuzungumza hata kama hawatasikilizwa! Ujue hata tukigoma jamaa wanafanya yao kwa miaka mitano!
 
Uchaguzi unarudiwa “wakubwa”wameamua na wanakuja kusimamia wenyewe
 
Mimi sipo nao wale, lakini pia nafikiri ni vyema wanawake mashujaa wakaenda bungeni! Tuwe aangalau watu wa kuzungumza hata kama hawatasikilizwa! Ujue hata tukigoma jamaa wanafanya yao kwa miaka mitano!

Kwani tulipokuwepo tuliwazuia kufanya yao?
 
Kwanza kabisa sikubali mchakato wa Uchaguzi wala matokeo! Ule haukuwa Uchaguzi bali uteuzi

Pamoja na hayo, nashauri chama changu pendwa CHADEMA tumuache mbunge wetu wa Nkasi, Idah, anendeleena ubunge. Pili Halima Mdee, Bulaya, na wanawake wote wa Viti Maalum waende Bungeni, kwa masilai ya taifa na chama pia. Tusikubali kuwaachia CCM Bunge peke yao.

Faida za chama ni kuwa na insiders wetu mle bungeni, ambao watatupenyezea ya kule na watapeleka ya kwetu hata kama yatakataliwa. Pia kuna ile milioni 1 kwa mwezi, Siyo mbaya tukiipokea! Siyo swala la kujali pesa, ni kwamba kiukweli pesa inatakiwa!

Mimi naipenda CHADEMA na napenda mabadiliko, lakini wamama waende kwanza bungeni wakati harakati zingine zina endelea!
Kwa jinsi mnavopenda helaa ni lazima muende la mtaendelea kupigana wenyewe kwa wenyewe. by the way tayari Lissu amerudi kwao, maana yeye ndio alikuwa kikwazo. Imeisha hiyooooooooooooooooooooooo
 
Hahaha chama hakitambui matokeo ya uchaguzi halafu kikubali viti maalumu?!

Huo utakuwa ujinga.

Chama kisikubali ujinga huu, hakuna faida ya kusaliti wanachama na wapiga kura wako.
 
Kwanza kabisa sikubali mchakato wa Uchaguzi wala matokeo! Ule haukuwa Uchaguzi bali uteuzi

Pamoja na hayo, nashauri chama changu pendwa CHADEMA tumuache mbunge wetu wa Nkasi, Idah, anendeleena ubunge. Pili Halima Mdee, Bulaya, na wanawake wote wa Viti Maalum waende Bungeni, kwa masilai ya taifa na chama pia. Tusikubali kuwaachia CCM Bunge peke yao.

Faida za chama ni kuwa na insiders wetu mle bungeni, ambao watatupenyezea ya kule na watapeleka ya kwetu hata kama yatakataliwa. Pia kuna ile milioni 1 kwa mwezi, Siyo mbaya tukiipokea! Siyo swala la kujali pesa, ni kwamba kiukweli pesa inatakiwa!

Mimi naipenda CHADEMA na napenda mabadiliko, lakini wamama waende kwanza bungeni wakati harakati zingine zina endelea!
Mimi naomba waendelee kuzira tu. Mbona Serikali za Mitaa walizira na matokeo wameyaona kwenye Uchaguzi Mkuu na wako poa tu?
 
Back
Top Bottom