Maoni ya Zitto kuhusu Mashinji kujitoa CHADEMA na kwenda CCM

..kwa upande mwingine unaweza kusema Dr.Mashinji amekuwa MUUNGWANA.

..amefanya kazi ya Ukatibu Mkuu mpaka pale CDM walipoamua hawamhitaji tena ndipo akaamua kwenda CCM.

..Dr.Mashinji ni tofauti na wale ambao bado walikuwa ktk nafasi zao ktk chama au bungeni halafu wakaamua kuhama. Huo siyo uungwana hata kidogo.

Na pia amekuwa mkweli kiasi, amesema ni maslahi binafsi (mkate kwa familia yake) tofauti na wale wengine iliyokaririshwa kuwa inaenda kuunga juhudi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi ile tweet kwamba ana familia ya kulisha ni kweli katuma Mashinji au wanampakazia?
Anatakiwa kujiajiri au kuajiriwa ili kuikimu familia,kwani chakula cha familia yake kipo kwenye vyama vya siasa?Huko alikoenda ndiyo mahali sahihi kuwatafutia hao wanafamilia chochote?Wanalisha familia za wanachama?
Kilicho dhahiri ni kuwa hajahamiaa Bali karudi kwake,ametekeleza alichotumwa.
 
We ile orodha ilisomwa mwembeyanga na sio.mwembechai
Kuna heshima kwenye siasa?

Tundu Lissu, kwa mujibu wake yeye mwenyewe, ndiye aliyeiandika ile orodha ya mafisadi iliyosomwa na Dkt. Slaa pale Mwembechai.

Tundu Lissu huyo huyo, ndo akaja kumpigia kampeni ya urais mmoja wa watu alodai kuwa ni mafisadi: Edward Lowassa.

Dkt. Slaa alipojitoa CHADEMA kwa sababu ya kupinga ujio wa Lowassa, Lissu huyo huyo akaanza kumshambulia Slaa huku akimtetea Lowassa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Anatakiwa kujiajiri au kuajiriwa ili kuikimu familia,kwani chakula cha familia yake kipo kwenye vyama vya siasa?Huko alikoenda ndiyo mahali sahihi kuwatafutia hao wanafamilia chochote?Wanalisha familia za wanachama?
Kilicho dhahiri ni kuwa hajahamiaa Bali karudi kwake,ametekeleza alichotumwa.
Ile kauli, kama kweli kaandika yeye, ni mbaya, si kwa CHADEMA, bali hata CCM.

Kwa maana kajidhihirisha yeye hajahamia CCM kwa sababu za kiitikadi, kisiasa au kifalsafa.

Kahamia CCM kwa kufuata maslahi ya moja kwa moja.

Hilo maana yake huyu ni mamluki, ni malaya wa kisiasa. Kesho akija mtu mwenye kidau zaidi ya CCM anaweza kuondoka CCM.

CCM wakimpa uongozi hata wa kata watakuwa wamejidhalilisha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
..nadhani Mashinji amejivunjia heshima.

..haiwezekani kuyakana yote aliyoyasema, kuyatenda, na kuyapigania, wakati akiwa CDM kirahisi-rahisi namna hii.
''ni hatari badala ya EL kupelekwa jela anachukua fomu kugombea urais CCM''-Mbowe (May, 2015), ''Hatuwezi kumuacha mtu mwenye wafuasi milioni moja kisa Katibu Mkuu'' Mbowe (July, 2015).Huyu naye anaheshima?
 
Back
Top Bottom