Maoni ya Serikali tatu ni ya kishabiki na kinafiki

Maoni ya Serikali tatu ni ya kishabiki na kinafiki

Wewe unaona bunge la jamuhuri ni sahihi kujibadili na kujiita bunga la katiba? Bila jazba, ushabiki wwala matusi pls.


na mawazo ya serikali tatu aliyainject yeye....asituzingue uyu mzee naona ameichoka nchi....kwa mtu mwenye akili timamu huwezi kuruhusu mijadala ya kujadili serikali tatu vs serikali mbili.....maana lile lengo la msingi limesahaulika tumebaki kwenye vijembe...hawa UKAWA wanahofia kushindwa kwa hoja zao kutokana na uchache wao na CCM wanajivunia wingi wao...wote hawapo sahihi!!!usahihi ni kuweka kero za muungano mezani na kuzitafutia ufumbuzi bila kuathiri Muungano uliopo...hata mke akikuudhi au kugombana mnasuluhisha na sio kuvunja ndoa..serikali tatu zinalenga kuvunja muungano
 
Yaani pamoja na mijadala yote hii, midahalo yote na hotuba zote bado kuna watu wameshindwa kuelewa??

Ndio maana mkiulizwa kwa nini nchi yenu bado ni maskini huwa mnakosa jibu mujarabu...

Hakika umaskini wa akili huzua umaskini kwa Taifa.

hoja ya msingi umetoa mkuu.
 
Hebu tusaidie namna nzuri yakuuboresha Muungano bila kuwa na Serikali tatu nakila Upande ukilidhike...

una akili sana,hiindio ilipaswa kusimamiwa na hao UKAWA wenu...wasiporidhika waingine mtaani,but its toolate!! am sorry to say serikali 2 zitabaki palepale na kero zilezile kwa uzembe wa UKAWA
 
Wewe unaona bunge la jamuhuri ni sahihi kujibadili na kujiita bunga la katiba? Bila jazba, ushabiki wwala matusi pls.

hii sio hoja.ulitaka wakaandikie katoba kona baa? provided haiingilii shughuli za kawaida za bunge na ukizingatia ni temporary hakun atatizo.sem ajingine
 
una akili sana,hiindio ilipaswa kusimamiwa na hao UKAWA wenu...wasiporidhika waingine mtaani,but its toolate!! am sorry to say serikali 2 zitabaki palepale na kero zilezile kwa uzembe wa UKAWA

huwezi kuubadili mfumo ukiwa ndani ya mfumo. i hate democracy.
 
Binafsi sijaona wadai serikali tatu cha maana wanachotaka zaidi ya unafiki na ufinyu wa mawazo.

Ufinyu wa mawazo ni pale unapobakia katika situation uliyopo, na kuendelea ku experience matatizo uliyokuwa nayo, na kutofikiria out of the box, ni alternative ipi inayoweza kutatua matatizo yako
 
eti Tanganyika yetu!!Go back to 1961....wewe badala ya kutafakari serikali ilnafikishaje huduma muhmu kwako mwananchi unaeishi chini ya dola 1 per day unaiwaza Tanganyika yako na bendera ya Tanganyika umeshaitafuta...pole yako sana.....utasubiri sana ndugu yangu,you cant fight me join me!!

Sinihii serikali ndio imefanya watu waishi chini ya hiyo mnaita Dola 1 zaidi ya 50yrs tunahangaika na tatizo.lilelile Tunawezaje kutatua tatizo lililoshindikana kwa miaka mingi tukitumia njia ileile then tutegemee Matokeo tofauti Jamaa watume ya Katiba wamekuja na mawazo ya Serikali 3 km njia yakuondoa hilo tatizo wee unasema hapana tusaidie njia iliyobora zaidi ya Serikali tatu ila jambo moja Utambue mkataa kwao ni mTUMWA
 
Maoni ya serikali mbili unayong'ang'aniza yanatokana na takwimu gani za maoni ya wanach? Report ya utafiti gani inaku surport kwamba waTz wanataka 2 na si 3?

Maoni ya 3 ni ya kishabiki. Ya serikali mbili ni ya nini?

Sayans gani unayotumia ku conclude hivyo?

kila mtu yupo huru kutoa maoni yake kwa hoja na sio matusi.

critically thinking ukichunguza wale wote wanaodai serikali tatu wamejaa ushabiki,uzandiki na unafiki....

kikubwa hapa ni watanzania kujiuliza ni aina gani ya Muungano tulio nao,nakumbuka bwana Mwakyembe (Mb) aliwahi kuelezea vema sana aina ya Muungano tulio nao.Ifahamike pia Muungano wetu ni wa mambo yasiyozidi saba (7) I stand to be corrected.

jambo la msingi kabisa hapa ni kujadili kile kinachoitwa kero za Muungano zinazotokana na mambo haya saba na sio kuunda kitu kipya kwa maana ya kusolve kero izo...

Muundo wa serikali mbili unaoondosha kero izo (either kwa kupunguza hayo mambo saba ya muungano yawe manne) ndio iwe suluhisho la aina ya Muungano tuutakao..

napatwa na mashaka sana na wale wote waliotoa maoni ya Muungano wa serikali tatu,ni mawazo yaliyojaa ushabiki na unafiki wa kutotaka kuwazua kwa kina hatima ya kile wanachokililia...nasema tena ni mawazo ya kishabiki ambayo mwisho wa siku wananchi hao watakimbia na kuiacha serikali ikijifia kwa zigo la garama za uendeshaji...

tukae tutafakari kwa kina mambo y amsingi kama huduma muhimu za shule,hospitali na maji namna ambavyo serikali itatufikia na sio kushabikia kinafiki kuongeza ukubwa wa serikali...

hata hivyo,robo tatu ya wajumbe imetimia na bunge la katiba linaendelea kama kawaida na katiba itapatikana tu!!na kwa vile wengi ni washabiki maandazi wataipokea tu na kuendelea na majukum yao y akila siku
 
Hebu jionee na useme sehemu hiyo ya ushabiki au ukaisome rasimu vizuri usije ukajikuta wewe ndio unaandika kwa ushabiki.
 
eti Tanganyika yetu!!Go back to 1961....wewe badala ya kutafakari serikali ilnafikishaje huduma muhmu kwako mwananchi unaeishi chini ya dola 1 per day unaiwaza Tanganyika yako na bendera ya Tanganyika umeshaitafuta...pole yako sana.....utasubiri sana ndugu yangu,you cant fight me join me!!

Kukaririshwa maneno ni mbaya sana no ugonjwa Mkubwa kwa watz,hapo juu kuna rasimu ya 2 embu kaisome kwanza ina majibu ya uwajibikaji embu jifunze kusoma kwa kuelewa sio kukariri,nenda ukaisome sio unakuja na uharo wako hapa.
 
pole sana mkuu na kwa kweli nasikitika sana kama kijana kama ww unakuwa na mawazo ya kimchepuko kama hayo, kweli kuepusha na kutumia busara ya kuokoa uvunjifu wa katiba uliofanywa na zanzibar kwa tume ya mabadiliko ya katiba kwa kuweka mfumo wa serikali 3? kama cyo mbona rais hachukuliwi hatua kwa kuchekelea uvunjaji wa katiba ya jamhuri?
 
wewe ni mmojawapo wa hao mashabiki maandazi waliojaa unafiki na woga..at the end of the day u end up failing...anyway kero za Muungano unazijua wewe?how do u think serikali 3 will solve them problems

Kero kubwa ya muungano ni katiba ya Zanzibar ambayo inataimbua Zanzibar kuwa ni nchi na imemfanya rais wa Muungano aonekane kama Rais wa nchi jirani na hakuna hata lakitatu mmoja ambae ana weza akathubutu kugusia hilo.
 
nenda kasome vizuri aina ya muungano tulio nao,tatizo kubwa watanzania hawasomi,,,zaidi ya kusubiria msaada wa komangano LIVE ITV....ni serikali tatu Offline...yale mambo saba ya muungano ndio serikali ya tatu,..na ndio UKAWA wanataka yaundiwe serkali..hapo yalipo tu ni mzigo na kuzungumkuti now uyaundie serikali na yachangiwe mapato..hii sio akili timamu

Fafanua gharama zinaongezekaje hapo? Kwani fedha zinazotumika kuendesha hayo mambo saba ya muungano sasa hivi zitabadilika endapo ikitengwa ijitegemee?
 
kila mtu yupo huru kutoa maoni yake kwa hoja na sio matusi.

critically thinking ukichunguza wale wote wanaodai serikali tatu wamejaa ushabiki,uzandiki na unafiki....

kikubwa hapa ni watanzania kujiuliza ni aina gani ya Muungano tulio nao,nakumbuka bwana Mwakyembe (Mb) aliwahi kuelezea vema sana aina ya Muungano tulio nao.Ifahamike pia Muungano wetu ni wa mambo yasiyozidi saba (7) I stand to be corrected.

jambo la msingi kabisa hapa ni kujadili kile kinachoitwa kero za Muungano zinazotokana na mambo haya saba na sio kuunda kitu kipya kwa maana ya kusolve kero izo...

Muundo wa serikali mbili unaoondosha kero izo (either kwa kupunguza hayo mambo saba ya muungano yawe manne) ndio iwe suluhisho la aina ya Muungano tuutakao..

napatwa na mashaka sana na wale wote waliotoa maoni ya Muungano wa serikali tatu,ni mawazo yaliyojaa ushabiki na unafiki wa kutotaka kuwazua kwa kina hatima ya kile wanachokililia...nasema tena ni mawazo ya kishabiki ambayo mwisho wa siku wananchi hao watakimbia na kuiacha serikali ikijifia kwa zigo la garama za uendeshaji...

tukae tutafakari kwa kina mambo y amsingi kama huduma muhimu za shule,hospitali na maji namna ambavyo serikali itatufikia na sio kushabikia kinafiki kuongeza ukubwa wa serikali...

hata hivyo,robo tatu ya wajumbe imetimia na bunge la katiba linaendelea kama kawaida na katiba itapatikana tu!!na kwa vile wengi ni washabiki maandazi wataipokea tu na kuendelea na majukum yao y akila siku

Kama hoja ni kumtafuta mnafiki, basi mtu huyo ni mtoa hoja hii hapa jamvini na wale wote wanaopinga mawazo yaliyopendekezwa na wananchi wakati wa kukusanya maoni.

Kama ni kuondoa kero za muungano, jitihada hizo zimefanyika kwa miaka yote 50 ya muungano huo, lakini badala ya kuziondoa ndio kwanza zinaongezeka hadi kufikia hatua ya kuvunja misingi ya katiba hii iliyopo, huku viongozi waliopewa dhamana ya kuilinda wakibaki wakikenua tu meno (toothless), na Chama kilichopo madarakani kikikosa dira na dhamira ya kweli ya kutatua hali hiyo.

Matakwa ya wananchi lazima yaheshimiwe, na matakwa ya kichama na kimakundi yaheshimiwe huko huko chamani na makundini kwao.
 
Venue ya kuandikia si hoja. Wanaweza kuandikia popote pale maana sehemu haibadilishi wala kuongeza quality ya kinachoandikwa.

Unaona wabunge wa bunge la jamhuri wana sifa ya kuandika katiba? kwa maana ya weledi.

Pili nini maoni yako kuhusu composition ya tume ya Jaji na quality ya kazi ya kukusanya maoni, kupitia nyaraka anuai na hadi uandishi wa hizo drafts?

Tatu, kulikuwa na usahihi upi wa kuivunja tume ya Jaji kabla ya mchakato haujaisha na kuifuta tovuti ya tume?

Nne. Kama tume ya Jaji imefanya kazi vibaya, bunge la jamhuri limepata watu maoni mbadala ya wananchi linayotumia katika kuandika katiba?

Wabunge wa Jamhuri, wanasifa na uwezo wa kufanya scientific research hadi kuandika katiba?

Hata kama wanadai ni wawakilishi wa wananchi, na wakaonyesha report ya tafiti walizofanya zinazowapa maoni ya wananchi wanayoyajadili sasa hivi. Ni sheria gani inayowapa mamlaka ya kukusanya maoni wao wenyewe, kuandika rasimu wao wenyewe, na kujadili rasimu yao kama bunge maalumu la katiba?

Tuendelee mtu wangu kuchanganua hoja.

hii sio hoja.ulitaka wakaandikie katoba kona baa? provided haiingilii shughuli za kawaida za bunge na ukizingatia ni temporary hakun atatizo.sem ajingine
 
Back
Top Bottom