Maoni ya Kambi ya Upinzani katika Bajeti 2013/14

Maoni ya Kambi ya Upinzani katika Bajeti 2013/14

Informer

Platinum Member
Joined
Jul 29, 2006
Posts
1,629
Reaction score
6,816
MAPENDEKEZO YA BAJETI 2013/14 YA KAMBI YAUPINZANI

i. Sheria ya Kodi ya Mapato, SURA 332.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kiwango cha chini cha kutoza kodi ya mapato ya ajira kwa mfanyakazi (PAY AS YOU EARN) kishuke kutoka asilimia 14 hadi asilimia 9 ya mshahara wa mfanyakazi.

ii.
Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147.
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kwa mapendekezo ya kuongeza kodi kwenye bidhaa za mafuta. Viwango vya sasa vya kodi na ushuru vibakie.

Kambi Rasmi ya Upinzani inapendekeza kodi mpya kwenye matumizi ya simu isikubaliwe na ibaki asilimia 12 kama ilivyokuwa zamani.

iii.
Sheria ya Ushuru wa Mafuta, SURA 220.
Katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuongeza kiwango cha ushuru wa mafuta (fuel levy) kutoka shilingi 200 kwa litahadi shilingi 263 kwa kwa lita sawa na ongezeko la shilingi 63 kwa lita. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni haikubaliani na pendekezo hili kwani lina madhara makubwa kwa maisha ya wananchi kwa kuwa linaongeza gharama za maisha kama vilekupanda kwa nauli, bei za vyakula nk. Hivyo Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kufutwa kabisa kwa ushuru mpya wa mafuta.

iv. Sheriaya Petroli ( Petroleum Act) SURA 392.
Katika sheria hii, Serikali inapendekeza kuanzisha tozo ya mafuta ya Petroli (petroleum levy) ya shilingi 50 kwa lita ambayo itakusanywa na Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa ajili ya kugharamia mahitaji ya Wakala wa Umeme Vijijijni (REA). Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA inapendekeza kufutwa kabisa kwa tozo ya mafutaya petroli ili kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha. Fedha za kwenda REA zipatikane kutoka kwenye kupunguza misamaha ya kodi.

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina mapaendekezo mengine ya kikodi kama ifuatavyo:

1. Kuondoa ongezeko la Kodi kwenye ngano, ili kupunguza mfumuko wa bei kwenye bidhaa zitokanazo na ngano kama vile chapatti, mikate, maandazi nk.

2. Kupunguza misamaha ya kodi hadi asilimia moja ya pato la Taifa

3. Kupanua wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya maendeleoya michezo (Sports Development Levy) ili kukuza michezo nchini na kugharimia timu za zinazowakilisha taifa katika michezo ya kimataifa. VAT inayolipwa hivi sasa kutoka viingilio vya michezo irekebishwe na kuwa ‘sports development levy'.

4. Kuongeza wigo wa kodi kwa kuanzisha tozo ya asilimia moja(1%) kwa bidhaa zote zinanazoingizwa nchini kutoka nje na tozo ya asilimia sifuri nukta tano (0.5%) kwa bidhaa zote zinazouzwa nje ya nchi kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya reli hapa nchini. (Railways Development levy on imports and exports).

5. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba kwa kuwa utaratibu wavitambulisho vya taifa umeanza na tayari sehemu fulani ya wananchi wamepewa vitambulisho na kwa kuwa kwa kupitia mfumo wa TIN na usajili wa magari kuna watanzania wengi sana wana rekodi za kikodi ni vema sasa sheria ya kodi ya mapato sura 332 ifanyiwe marekebisho ili kulazimisha kila mwananchi ajaze ‘tax return' awe au asiwe na kipato.

6. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza kwamba mfumo wa VAT ‘zero rating'katika jedwali la Kwanza ufutwe na badala yake kwa bidhaa zenye umuhimu na zilizopo kwenye jedwali la kwanza zipelekwe jedwali la tatu kama ‘specialrelief'.

7. Kambi ya Upinzani inapendekeza sheria ya Uwekezaji nchini, TIC, ifanyiwe marekebisho ili Misamaha yote ya kodi iwekwe wazi na kukaguliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (Transparency and Audit of Tax exemptions)ili kudhibiti matumizi mabaya ya misamaha ya kodi.

8.Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza mabadiliko ya Sheria yaMawasiliano (EPOCA) ya mwaka 2009 ili kuipa TCRA mamlaka ya kufanya ukaguzi wa uwekezaji unaofanywa na kampuni za simu hapa nchini kwa lengo la kuzuia ukwepaji kodi unatokana na kudanganya gharama za uwekezaji.

9. Kambi ya pinzani inapendekeza kuwa tozo mpya kwenye mobile money transfer litumike iwapo tu tozo kama hili litawekwa kwenye utumaji fedha kwa njia za benki na njia nyinginezo. Vinginevyo tozo hili ni la kibaguzi na linapendelea watu wenye uwezo mkubwa dhidi ya wanyonge na hivyo tunatoa wito kuwa pendekezo hili lisikubaliwe na Bunge.

10. Kambi ya Upinzani Bungeni inapendekeza Bunge litunge sheria kudhibiti matumizi ya ‘tax havens' yanayofanywa na kampuni za uwekezaji na haswa kwenye sekta za Mawasiliano, Madini, Mafuta na Gesi na nyinginezo. Tanzania ijondoe katika mikataba yote yakikodi na nchi ambazo ni ‘tax havens'.

Alternative Budget proposals


  • [*=left]No commercial loans
    [*=left]Allocate 41% of internal revenue for development
    [*=left]Introduce special tax for promoting sports, all taxes charged currently on sports entry fees to be a sports development levy, eg VAT on entry fees to stadiums.
    [*=left]Ammend income tax legislations to make a mandatory for all Tanzanian residents to fill tax returns.
    [*=left]Introduce Railways development levy on exports (0.5%) and imports (1%).
    [*=left]Regulate the use of Tax havens by local companies and multinationals to curb tax evasion and tax avoidance through mandatory transparency of use and not signing tax treaties with tax havens.
    [*=left]Reform VAT legislation by deleting First Schedule which allow zero rating.
    [*=left]Ammend EPOCAl egislation to mandate TCRA to audit investments costs by telecommunications companies in order to curb tax avoidance.
    [*=left]Pay pension to all citizens over 60 years
    [*=left]Lower income tax for lowest income bracket to 9%
    [*=left]Reduce unnecessary expenses by cutting 30% of ‘other charges' for ministries and departments
    [*=left]More independent budget based on 75.8% internal revenue
    [*=left]Reduce tax exemptions to 1% of GDP. All exemptions MUST be transparently published and audited by CAG and audit made public.
    [*=left]Control price increase for important consumer goods
    [*=left]Increase minimum wage to TSH 315,000
    [*=left]No tax increase on diesel and petrol
    [*=left]No tax increase for wheat to avoid price increase for bread etc
    [*=left]No tax increase for mobile phone use

Download attachment kusoma zaidi
 

Attachments

[h=5]Alternative 2013/14 Budget proposals
o No commercial loans
o Allocate 41% of internal revenue for development
o Introduce special tax for promoting sports, all taxes charged currently on sports entry fees to be a sports development levy, eg VAT on entry fees to stadiums.
o Ammend income tax legislations to make a mandatory for all Tanzanian residents to fill tax returns.
o Introduce Railways development levy on exports (0.5%) and imports (1%).
o Regulate the use of Tax havens by local companies and multinationals to curb tax evasion and tax avoidance through mandatory transparency of use and not signing tax treaties with tax havens.
o Reform VAT legislation by deleting First Schedule which allow zero rating.
o Ammend EPOCA legislation to mandate TCRA to audit investments costs by telecommunications companies in order to curb tax avoidance.
o Pay pension to all citizens over 60 years
o Lower income tax for lowest income bracket to 9%
o Reduce unnecessary expenses by cutting 30% of ‘other charges’ for ministries and departments
o More independent budget based on 75.8% internal revenue
o Reduce tax exemptions to 1% of GDP. All exemptions MUST be transparently published and audited by CAG and audit made public.
o Control price increase for important consumer goods
o Increase minimum wage to TSH 315,000
o No tax increase on diesel and petrol
o No tax increase for wheat to avoid price increase for bread etc
o No tax increase for mobile phone use
[/h]
 
Hii ndo bajeti mbadala? Ama kweli ukishangaa tá musa utaona ya fraun.

Tatizo hujui nii maama ya bajeti, bajeti mbadala na mapendekezo. Haya ni mapendekezo kwenye bajeti. Nenda shule tena manake inaonekana huna unalolijua.
 
Tatizo hujui nii maama ya bajeti, bajeti mbadala na mapendekezo. Haya ni mapendekezo kwenye bajeti. Nenda shule tena manake inaonekana huna unalolijua.

naona sio wewe pekee uliesoma, ila kwa kuwa ni bajeti ya upinzani ni lazima ikuvurie
 
wana masikio lakini hawasikii,wana macho lakini hawaoni.HAO NI CHAMA CHA ZAMANI
 
imetulia hususani kwny kupunguza misamaha ya kodi,upotevu hasa mapato bandarini, gasi,madini.
 
Hayo ni mapendekezo ya kodi kwenye bajeti. Mbona mnavichwa vigumu kuelewa? Haki ya nani humu kuna vilaza mpaka basi. Mnachekesha sana aisee.


Shule ndogo. Wasamehe bure. Tehe, tehe, tehe!
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimesababisha vyombo vyote vya habari vya ndani na nje ya nchi kufuatilia kila kitakachosemwa na kifanywa na chama hicho.

Ikiwa ni wiki ya bajeti kuu ya serikali vyombo vya habari kwa ujumla vimeipa uzito mdogo sana na kusababisha hata wananchi kuipuuza kana kwamba hakuna kinachoendelea Dodoma

Badala yake habari kuu kwenye vyombo vyote vya ndani ya nchi ni kuhusiana na Mbowe,Lema na Chadema.Pia kitendo cha wabunge wa Chadema kuondoka wote bungeni kumesababisha wananchi kupuuza kabisa kufuatilia kinachoendelea humo.

Wakati mashirika ya habari ya nje ya nchi yakiandika na kutangaza kwa uzito bajeti za Kenya,Uganda na Rwanda imekuwa tofauti kwa Tanzania ambapo Chadema na viongozi wake ndiyo wanaoonekana katika habari za Mashirika hayo ya kimataifa.
 
Kweli bajeti yetu imedoda.Ninaangalia bunge la bajeti,wachangiaji wengi hawapo.Jenister Mhagama(mwenyikiti) amesema ataongea na wanadhimu wa vyama kwa nini wabunge hawapo.Nina wasiwasi wataahirisha mjadala mapema.Hata magazeti nchini hayajatoa nafasi kubwa mjadala wa bajeti unaoendelea.
Wabunge wa CDM naomba mrudi bungeni,tunapata upweke.
 
Wabunge wahamia kwenye mitandao badala ya kusikiliza bajet.
1.sita
2:mwigulu
3:rage na wengine weng.
 
Back
Top Bottom