comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Wana jamvi.
Wana jf
Salaam
Kutokana na maendeleo ya kidunia hasa kiulinzi baadhi ya nchi wanachama duniani wana majeshi ya pamoja mfano NATO kwa utekelezaji wa majukumu ya kimataifa, Hata nchi za Afrika Magharibi wana umoja wa majeshi yao ya ECOWAS ambayo hutekeleza majukumu yao katika nchi wanachama wao tu mfano baada ya uchaguzi wa Gambia na kupelekea Rais alieshindwa kugoma kuondoka madarakani, Majeshi ya ECOWAS yanajiandaa kuivamia kijeshi ili Rais alieshinda Adama Barrow akabidhiwe madaraka kwa amani bila kuvunja katiba.
Hivyo kuna haja jumuiya ya Afrika mashariki tuwe na jeshi maalumu ambalo litakua na utekelezaji wa majukumu maalumu tu, mfano kudhibiti maharamia kwa pamoja, kuingilia kati nchi mwanachama anapochokozwa na kuvamiwa na Majeshi ya nje ya Afrika Mashariki, kuingilia kijeshi nchi mwanachama yoyote anaetishia usalama wa mwenzake, kushauri kiongozi yoyote atakaeonesha nia ya kung'ang'ania madaraka baada ya muda kikatiba kuisha.
Aidha, Pia liwe na jukumu la kutekeleza majukumu ya taasisi za kiraia mfano kutoa msaada wa haraka kwa mwanachama yoyote aliekumbwa na majanga makubwa.