Maoni: Msemaji wa Serikali akiongea kuwe na Mtaalamu husika kufafanua kiufundi zaidi

bryan2

JF-Expert Member
Jun 8, 2016
3,323
4,667
Natoa kama maoni na kawaida ya maoni yanaweza kuchukuliwa au kuachwa.

Kwa msemaji mkuu wa Serikali anapotoa maelekezo/ufafanuzi juu ya jambo flani ingependeza sana kama mhusika/mtaalamu zaidi wa idara au Wizara husika kuwepo kwa lengo la kufafanua kiundani zaidi.

Mfano unazungumzia kuhusu ndege zetu nzuri za Airbus kutoruka(grounding) kwa maelekezo ya watengenezaji ni vema wananchi wangeelezwa kitaalamu zaidi kuliko kusema hata nchi nyingine duniani zinafanya hivyo lengo ni kupunguza sintofahamu zaidi,pia mzungumzaji anapozungumza hatoi majibu/solution ya mada husika bali anakua kisiasa zaidi na vitisho vingi.

Wote tunakumbuka baada ya ndege za Ethiopia kupata ajali kampuni ya uundaji wa ndege ya Boeing alitoa waraka ndege zote za toleo lile zisitumike hata leo ukigoogle utapata sababu Je airbus nao wametoa sababu zao kitaalamu mimi na wewe hatujui.

Ukija kwa mambo ya Utalii iwe hivyo hivyo tena kuwe na mtaalamu zaidi mfano kuna ile ndege kubwa ilitua KIA mpaka leo watanzania hawajui ilitua kwa lengo gani kosa ni lile lile la msemaji kutokua na majibu ya maswali mazito na mwisho wake huishia kutoa majibu mepesi na vitisho.

Mkielewa dunia ya leo sio sawa na ile ya karne ya 15 ya Kina Vasco da Gama leo taarifa zinapepea zaidi, pia kuna vyanzo mbalimbali vya habari sio kama zamani tunategemea RTD tu ili kupunguza umbeya mwingi au tetesi ni vema taarifa husika ikagusa maeneo yote Muhimu.

Sidhani kama Msemaji wa Serikali amewahi kuzungumza bila kuwacha maswali mengi kwa wananchi baada ya speech zake nyingi kinachofwata ni wananchi kuhoji zaidi, kuna haja ya msemaji wa Serikali kubadilika na kutumia wataalamu zaidi na sio kumonopolize kila kitu.
 
Back
Top Bottom